Mashaxizo
JF-Expert Member
- Jun 13, 2013
- 6,707
- 3,355
Siku moja Yesu alitoka na Yuda kwenda kutangaza dini, walichukua mikate mitatu, mikate aliibeba Yuda, wakaanza safari, walipofika mbali, Yuda alihisi njaa, akavumiliaaa, mwisho akashindwa, kwa kificho akaula mmoja, walipofika mbele Yesu akamwambia Yuda toa mikate tuile, kutolewa ni miwili badala ya mitatu, Yesu akauliza uko wapi mmoja, Yuda akasema hajui, wakaacha kuila ile iliyobaki wakaendelea na safari, kufika kivuukoni Yesu alimtaka Yuda kusema ukweli, akikataa mamba watamla coz ni muasi, Yuda akasema "fanya wasinile nitakupa ukweli baada ya kuvuuka, walipovuuka Yesu akamuuliza 'nani kala mkate? Yuda akasema "simjui" wakaendelea na safari wakafika kijiji flan wakakaribishwa mbuzi, walipomaliza kula Yesu akakusanyiwa mifupa ya yule mbuzi, akaipiga kirungu mbuzi akafufuka, akamgeukia Yuda na kumtaka aseme ukweli, Yuda alikataa tena. Wakaendelea na safari, usiku ukaingia wakalala njian, Yuda aliamka mwanzo, akatupia macho huku na kule, kwa mbali akaona Mji, bila ya kumuamsha Yesu, akaamua kwenda na akakichukua kile kirungu cha Yesu alichofufulia mbuzi, kufika ktk ule mji, aliona tafrani, mara huyu kenda kule huyu kenda huku, akauliza 'kunani?' akaambiwa Mfalme wetu yuko mahututi, akaomba apelekwe, kufika tu, akampiga kile kirungu, yule Mfalme akafa papohapo. Ayaa majanga! Akahukumiwa kunyongwa, akawekwa ktk tanzi kusubiri masaa tu ili anyongwe. Upande wapili, Yesu alipoamka kutomuona Yuda wala kirungu chake, akaangalia huku na kule akaona ule mji, akajua Yuda yuko pale, alipofika akakuta watu wamezunguka, akauliza 'kunani' akapewa mchapo, akaamua kwenda kumuona huyo Muuaji, kufika ni Yuda, Yesu akamwambia Yuda 'sema nani kala mkate au nakuacha unakufa' Yuda akasema 'hapa siko huru, kamfufue Mfalme halafu nitakwambia ukweli' Yesu akamfufua, Yuda akatolewa kitanzini, akasema hajala mkate. Duh!
Wakaendelea na safari, wakapita ufukweni, Yesu huku Yuda kule, Yesu alikusanya mchanga virundo vitatu, akavipiga kirungu vikageuka dhahabu. Akamwita Yuda, akamwambia nimeokota dhahabu tugawane, Yesu alimtaka Yuda agawe. Yuda akasema 'kimoja changu, kimoja chako na kimoja tunagawa katikati' Yesu akasema 'hapana kimoja chako, kimoja changu na kilichobaki tutampa aliekula mkate' wana JF kazi kwenu Yuda alisemaje?