Sharbel
JF-Expert Member
- Feb 20, 2020
- 1,103
- 2,265
Wasalaam wakuu.
Siku zote tumezoea kuwaona, viongozi mbalimbali kama Raisi na Waziri mkuu wakitembelea miradi mbalimbali ya kwenye halmashauri kukerwa na ubadhirifu ulipo huko.
Hata ripoti ya CAG iliyopita, imeonesha kuna wizi mkubwa tu huko kwenye halmashauri mbalimbali za nchi hii.
Lakini tuna madiwani ambao wamepewa nguvu ya kupanga bajeti ya halmashauri na kusimamia fedha za miradi ili zitumike kutekeleza miradi inayotakiwa (nimetaja chache tu).
Shida ni hii sasa, wengi wanaopata nafasi za udiwani wana uwezo mdogo, sio wadadisi, hawatambui mamlaka walionayo, na sasa imefikia hatua hata wananchi wanadharau hicho cheo.
Lakini kama madiwani wangetumia vizuri mamlaka waliyonayo basi wananchi wangeondokana na changamoto nyingi zinazowakumba.
Mfano halmashauri nyingi shida ya maji bado ipo, na hata kwenye hospitali za wilaya maji ni changamoto, lakini kuna mkurugenzi kuna madiwani wapo, na si ajabu halmashauri hiyo inakusanya fedha nyingi na vilevile inapokea pesa za miradi lakini maendeleo hakuna.
Hivyo kwenye chaguzi zijazo, kwenye udiwani wagombee watu wanaoeleweka, sio wale wanaotaka posho tu lakini kichwani hamna.
Asanteni.