Cheo cha Udiwani kithaminiwe. Wanaogombea wapitie mchujo mkali

Sharbel

JF-Expert Member
Feb 20, 2020
1,076
2,242
Wasalaam wakuu.

Siku zote tumezoea kuwaona, viongozi mbalimbali kama Raisi na Waziri mkuu wakitembelea miradi mbalimbali ya kwenye halmashauri kukerwa na ubadhirifu ulipo huko.

Hata ripoti ya CAG iliyopita, imeonesha kuna wizi mkubwa tu huko kwenye halmashauri mbalimbali za nchi hii.

Lakini tuna madiwani ambao wamepewa nguvu ya kupanga bajeti ya halmashauri na kusimamia fedha za miradi ili zitumike kutekeleza miradi inayotakiwa (nimetaja chache tu).

Shida ni hii sasa, wengi wanaopata nafasi za udiwani wana uwezo mdogo, sio wadadisi, hawatambui mamlaka walionayo, na sasa imefikia hatua hata wananchi wanadharau hicho cheo.

Lakini kama madiwani wangetumia vizuri mamlaka waliyonayo basi wananchi wangeondokana na changamoto nyingi zinazowakumba.

Mfano halmashauri nyingi shida ya maji bado ipo, na hata kwenye hospitali za wilaya maji ni changamoto, lakini kuna mkurugenzi kuna madiwani wapo, na si ajabu halmashauri hiyo inakusanya fedha nyingi na vilevile inapokea pesa za miradi lakini maendeleo hakuna.

Hivyo kwenye chaguzi zijazo, kwenye udiwani wagombee watu wanaoeleweka, sio wale wanaotaka posho tu lakini kichwani hamna.

Asanteni.
 
Madiwani walipwe kwa kufuata utaratibu wa bunge na wenyeviti wa vijiji/mitaa walipwe kwa kufuata utaratibu unaotumiwa kumlipa Rais maana wote wanachaguliwa na wananchi kuwawakilisha na kusimamia maendeleo ya wananchi.

Baada ya hapo, tuwawajibishe!

Bila hivyo, unafikiri wataishije na familia zao na kila siku wapo ofisini kuhudumia wananchi bure?
 
Ni kweli usemayo, lakini hata wa bunge wanalipwa vuzuri mno lakini matokeo yake tunayaona hawana msaada kwa wananchi.
 
Madiwani walipwe kwa kufuata utaratibu wa bunge na wenyeviti wa vijiji/mitaa walipwe kwa kufuata utaratibu unaotumiwa kumlipa Rais maana wote wanachaguliwa na wananchi kuwawakilisha na kusimamia maendeleo ya wananchi.

Baada ya hapo, tuwawajibishe!

Bila hivyo, unafikiri wataishije na familia zao na kila siku wapo ofisini kuhudumia wananchi bure?
Mbona wabunge wanalipwa fedha nyingi kupita kiasi na hakuna cha maana wanachofanya?
 
Wasalaam wakuu.

Siku zote tumezoea kuwaona, viongozi mbalimbali kama Raisi na Waziri mkuu wakitembelea miradi mbalimbali ya kwenye halmashauri kukerwa na ubadhirifu ulipo huko.

Hata ripoti ya CAG iliyopita, imeonesha kuna wizi mkubwa tu huko kwenye halmashauri mbalimbali za nchi hii.

Lakini tuna madiwani ambao wamepewa nguvu ya kupanga bajeti ya halmashauri na kusimamia fedha za miradi ili zitumike kutekeleza miradi inayotakiwa (nimetaja chache tu).

Shida ni hii sasa, wengi wanaopata nafasi za udiwani wana uwezo mdogo, sio wadadisi, hawatambui mamlaka walionayo, na sasa imefikia hatua hata wananchi wanadharau hiko cheo.

Lakini kama madiwani wangetumia vizuri mamlaka waliyonayo basi wananchi wangeondokana na changamoto nyingi zinazowakumba.

Mfano halmashauri nyingi shida ya maji bado ipo, na hata kwenye hospitali za wilaya maji ni changamoto, lakini kuna mkurugenzi kuna madiwani wapo, na si ajabu halmashauri hiyo inakusanya fedha nyingi na vilevile inapokea pesa za miradi lakini maendeleo hakuna.

Hivyo kwenye chaguzi zijazo, kwenye udiwani wagombee watu wanaoeleweka, sio wale wanaotaka posho tu lakini kichwani hamna.

Asanteni.
mijini inawezekana, lakini vijijini bado sana yaani wakiona una vihelahela kidogo labda mwaka huo umevuna sana bas watakwenda na wewe suala la elimu na mipango si muhimu.

wanazingatia zaidi mahaba kwa mgombea na fedha alizonazo basi.
Na lijamaa likienda huko hutaliskia hadi miaka mi5 ijayo tena.
 
Ndio shida hapo, bado wananchi wengi wana uwezo mdogo kwenye kufikiri.

Ukitaka kujua tembelea vijiwe vyao ni stori za uwongo mwingi.
 
Wasalaam wakuu.

Siku zote tumezoea kuwaona, viongozi mbalimbali kama Raisi na Waziri mkuu wakitembelea miradi mbalimbali ya kwenye halmashauri kukerwa na ubadhirifu ulipo huko.

Hata ripoti ya CAG iliyopita, imeonesha kuna wizi mkubwa tu huko kwenye halmashauri mbalimbali za nchi hii.

Lakini tuna madiwani ambao wamepewa nguvu ya kupanga bajeti ya halmashauri na kusimamia fedha za miradi ili zitumike kutekeleza miradi inayotakiwa (nimetaja chache tu).

Shida ni hii sasa, wengi wanaopata nafasi za udiwani wana uwezo mdogo, sio wadadisi, hawatambui mamlaka walionayo, na sasa imefikia hatua hata wananchi wanadharau hicho cheo.

Lakini kama madiwani wangetumia vizuri mamlaka waliyonayo basi wananchi wangeondokana na changamoto nyingi zinazowakumba.

Mfano halmashauri nyingi shida ya maji bado ipo, na hata kwenye hospitali za wilaya maji ni changamoto, lakini kuna mkurugenzi kuna madiwani wapo, na si ajabu halmashauri hiyo inakusanya fedha nyingi na vilevile inapokea pesa za miradi lakini maendeleo hakuna.

Hivyo kwenye chaguzi zijazo, kwenye udiwani wagombee watu wanaoeleweka, sio wale wanaotaka posho tu lakini kichwani hamna.

Asanteni.
Na walipwe vizuri ndio maana badala ya kusimamiwa Fedha za Halmashauri nao wanakuwa sehemu ya upigaji na udokozi
 
Tabia ya udokozi haiwezi koma hata ukamuongezea mshahara kiasi gani, lakini sina maana ya kuwa wasilipwe vuzuri
 
Wabunge Huwa wanadokoa nini kuisimamia Serikali? Manaa nature ya Bunge ndio hivyo hivyo na Baraza la Madiwani.

Sana sana Serikali ndio huwahonga wabunge na sio waomkudokoa pesa za Miradi.Iwe hivyo na Kwa madiwani walipwe vizuri Ili wasimamie Halmashauri vyema.
 
Ni kweli usemayo, ndio maana kwakuwa hamna malipo mazuri ndio maana wanawapata watu ambao wanaendana na hayo malipo.

Si vizuri kusema ni low quality lakini ina niladhimu niseme hivyo
 
Back
Top Bottom