CHEO BILA KITABU

CHEO BILA KITABU

Kiwalani finest

Senior Member
Joined
Jul 6, 2024
Posts
116
Reaction score
85
WATU HAWAITAKI KABISA ELIMU YA VITABU
ILA
WANATAKA VYEO
KWA SABABU GANI !?!?
KWA SABABU NI WEZI WALIOVAA NGOZI YA MWANAKONDOO HUKU WAKIWA NI MBWA MWITU.


Nilisikika katika Ulimwengu wa kiroho huko Usingizini nikibwata kuwakemea wezi wenye sura za kiutu huku wakiwa Mashetani yaliyovaa miili na Kisha kuwaendea watu wayachague wakidhani ni binaadamu kumbe ni Mashetani .
Nikaanza
Suala la Elimu ni agizo la Mwenyezi Mungu kwa Wanaadamu .
Tunapotaka kuongoza watu tujuwe kazi ya Uongozi ni kazi ya kumtumikia Mwenyezi Mungu.
Haiwezekani Kama wewe ni Binaadamu na Wala sio Shetani ukaomba Uongozi huku ukiwa hujibidiishi kusoma ilani katiba Kanuni Miongozo na Taratibu za kimfumo
Unaishi kwa kufoka foka na kutegemea Machawa Wapotoshaji Kama nyenzo zako za Uongozi.
Ukifanya hivi unatoka kwenye ubinaadamu na unakuwa Shetani uliyevaa mwili wa kibinaadamu huku ukilazimisha uheshimike huku wewe ukiwa huna heshima na Mwenyezi Mungu anayesisitiza watu wasome wawe na Elimu.
Tukisoma Biblia Takatifu Mithali 4:13 Mwenyezi Mungu anatueleza
Mkamate saana Elimu usimuache aende zake
Mshike
Maana Yeye ni Uzima wako
Mwisho wa kunukuu
Ndiyo Maana Viongozi huapa kwa Mwenyezi Mungu ya kuwa wataikamata Elimu iliyoko kwenye
Maandiko Matakatifu
Kwenye ilani katiba Kanuni Miongozo na Taratibu za kimfumo.
Viongozi wanapoikiuka ahadi Yao waliyomuahidi Mwenyezi Mungu hutoka kwenye utii wa Mwenyezi Mungu na kuwa Mashetani.
Biblia Takatifu Ayubu 22:21 inatueleza
Mjuwe saana Mungu ili uwe na Amani ndivyo mema yatakavyo kujia
Mwisho wa kunukuu
Kumjuwa Mungu ni kufuata Maelekezo yake .
Leo hii tumekataa Maelekezo ya Mwenyezi Mungu kuhusu Elimu tumeamua hisia za vifua vyetu na msaada wa Machawa viwe mbadala wa Maelekezo ya Mungu.
Tusome katiba ya CCM 1977 toleo 2022 ibara 05(04) Kisha tusome Kitabu Cha Nukuu za kiswahili za Mwalimu uk 153
Mwandishi anasema
Mwl Julius Kambarage Nyerere aliwahi kusema
Elimu ni kitu ambacho Sisi sote tunapaswa kuendelea nacho toka siku ya kuzaliwa mpaka siku ya kuiacha Dunia.
Mwisho wa kunukuu
Tunapoiacha Elimu ya ilani katiba Kanuni Miongozo na Taratibu za kimfumo tukaweka watu wasiosoma ili wawaongoze wasomi Kisha kukimbilia kwa watumishi wa Mungu kujifanya Kama tuko nao huku tukikataa Maelekezo ya Elimu iliyojaa haki na usawa ndani yake tunakuwa tunatoka kwenye himaya ya Mwenyezi Mungu na kujisajiri kwa Shetani kwa tamaa zetu zilizojaa Ubinafsi wa kutumia uelewa Mdogo wa Binaadamu wenzetu Kama kisa Cha kuwaibia Mali zao kwa hila za kishetani Shetani .
Biblia Takatifu 1Wakorintho 3:16-17
Inatueleza
Hamjuwi ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu na ya kuwa Roho wa Bwana Mungu anakaa ndani yenu !?
Kama mtuakiharibu hekalu la Mungu atamharibu mtu huyo kwa Maana hekalu la Mungu ni Takatifu ambalo ndilo Ninyi .
Mwisho wa kunukuu
Tunaongozwa na watu walioharibu na kulikaidi hekalu wasiosoma huku tukiwalinda na kuhamasisha Machawa yatushangilie kana kwamba tunatenda haki kwa Ujinga tuufanyao wa kuwalea wasiostahili.
Tukisoma Biblia Takatifu Wagalatia 6:3
Tunaelezwa
Maana mtu akijiona kuwa ni kitu naye si kitu
Ajidanganya nafsi yake
Mwisho wa kunukuu
Tumejiona ni watu boora kiasi kwamba hatutaki Tena kuwasikiliza Mafukara kwa vile tuwaibia tukakataa kusoma Mapato na matumizi wananywea .
Biblia Takatifu 1 wakorintho 10:15
Inatueleza
Nasema Kama na watu wenye akili
Lifikirini Ninyi ninenalo.
Mwisho wa kunukuu
Tunapomkataa Mwenyezi Mungu Maelekezo yake kuhusu Elimu tunaondokewa na akili tunakuwa maboya yenye kulazimisha kuheshimiwa huku tukiwa hatustahili kuheshimiwa kwani kumheshimu mtu anayemkiuka Mwenyezi Mungu kwa makusudi ni sawa na kulazimisha kujiita Makafir mchana kweupe.
Biblia Takatifu Hosea 4:6
Inatueleza
Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa
Kwa kuwa Wewe umeyakataa maarifa Mimi Nami nitakukataa wewe.
Mwisho wa kunukuu
Tumewakataa Wenye Eimu ya kimfumo na kuwakubali wasiosoma huku tukijuwa hatutendi haki tumekuwa Makafiri tujifichao kwenye kujitamkisha neno Mwenyezi Mungu huku tukimtumikia Shetani.
Wanafiki wavaao vizuri tuliokwisha kataliwa na Mwenyezi Mungu na kuwa Mafirauni wenye mionekano ya utu wema.
Kwa matendo yetu haya maovu tujuwe
Tusipojisahihisha kuiona
Pepo kwetu itakuwa hakuna.
Shekhe Othman Khamis Juma
Imam Masjid Mwinyiamani
Nakumbuka Tarehe 05/03/2025
Alisema
Nani kalazimisha Waislam wasome Dini !?!
Nani kalazimisha !?!?
Amelazimisha Mwenyezi Mungu Subhahanahu Wataalla.
Ikiwa kusoma ni lazima na Aliyelazimisha ( kusoma) ni Allah ,
Na Waislam kusoma hawataki ( kwa ) makusudi ,
Haya ,
( Je) Mungu kaheshimiwa ( au) kavunjiwa heshima !?
Wewe ukiwa ni Mtawala
Ni Mfalme ,
Ni Imam,
Ni Baba nyumbani ,
Siyo !?
( Halafu ) umetoa amri yako ya lazima pale nyumbani itekelezwe,
Kisha Familia wakaafikiana wote kuto kutekeleza .
Ukirudi unakuta hawakufanya amri yako ( je watakuwa) wamekuheshimu ( au) wamekudharau !?
Maneno haya yanaumiza lakini lazima tuambiane tu.
Waislamu mumeamuwa kumdharau (Mwenyezi) Mungu Subhahanahu Wataalla.
Mmefanya Jambo la kusoma Kama ( vile) ni ( Jambo la) khiari yenu tu
Na kukataa Kuna Aina mbili tu
Kuna kukataa kwa dhahiri
Na kukataa kwa kujificha .
Yaani ni Kama umekubali lakini kwa Uhalisia umekataa
Mwisho wa kunukuu
Viongozi hushika Qur aan kuapa tukimaanisha kuikubali Elimu ya Dunia na Akhera
Tukipata Uongozi tunanogewa dhulma
Mtu akitamka haki tunamfanya adui kwa ule utamu wa kuwadhulmu Mafukara wasiojielewa ulivyotunogea .
Tumemuasi Mungu na kumkaribisha Shetani ndiyo maana hata tukikumbushwa pale tulipopaendea Kinyume muda wote tunakuwa ni wakali .
Mafukara wanateseka Sisi tunacheka tulao Milo mitatu huku tukipanga mipango ya miaka mingi mbele blla kurekebisha maumivu yawaumizao Mafukara kisa tu Sisi na familia zetu
Tunakula Milo mitatu
Tuna magari
Tunaishi kifahari kiasi Cha kuwaona Mafukara Kama uchafu wa dampo.
Tunawaza kuboresha kesho zetu kana kwamba tuna ubia na Mwenyezi Mungu
Tumepoteza akili hatuna akili Tena tumekuwa Kama mahayawani tuliotokwa utu kwa utamu wa dhulma .
Shekhe Othman Khamis Juma
Nakumbuka Tarehe 05/03/2025
Alisema
Ukimsikiliza vizuri saana
Bwana Mtume Mohammad SAW
Anatueleza kwamba mtu yeyote anayeitegemea kesho ...
Anaihesabia kesho ...
Huyo mtu Hana akili
Hana akili
Usiniangalie Mimi ( ukanishangaa kwa maneno haya )
Sisemi Mimi
Kasema Mtume Mohammad SAW
Unaweza ukajikuta umenilaumu
Siyo Mimi
Mtume kasema
Mtu yeyote anayeitumainia kesho huyo mtu Hana akili .
Mwisho wa kunukuu
Tusikuwa na akili
Tunaona
Viongozi baadhi
Wakikiuka Viapo na Taratibu za kimfumo
Tunawaacha wazidi kukiuka
Tunasubiri kuwachukulia hatua baada ya miaka mitano kwenye Chaguzi
Hatuna akili
Tusome Sasa
Tuachane na hisia Binafsi
Tufuate Maandiko Matakatifu kila mtu kwa imani yake, ilani, katiba, Kanuni Miongozo na Taratibu za kimfumo
Tuache Ujinga na Upumbavu wa kuwachukia wanaojuwa na kuwakumbatia wasiojuwa huku kwa Unafiki tukitangaza mbele ya Jamii ya kuwa Sisi ni watenda haki hiku tukiwa hatuna hata harufu za haki
Unafiki.
Usijione Kama vile umri umekwenda ukakata tamaa
Elimu haina uzee
Tujipange tusome ili tutekeleze amri ya Mwenyezi Mungu ya kututaka tusome .
Shekhe Othman Khamis Juma
Imam Masjid Mwinyiamani
Nakumbuka Tarehe 05/03/2025
Alisema
Mimi najuwa asilimia 85 ya Masahaba wote wa Mtume Mohammad SAW wamesoma wakiwa watu wazima
Asilimia 15 Masahaba wakiwa vijana
Na (Masahaba) wengine ( umri wao ) Mtume wanamzaa
Ni Mtoto wao
Lakini (walitii)
Walikwenda kupiga goti ( kusoma kwa sababu ) wanataka kumjuwa Mola wao .
Ikiwa Wewe huendi kusoma kwa sababu ya umri wako tutakuuliza
Wewe ni Bora kuliko Masahaba wa Mtume Mohammad
( Je) umewazidi ubora !?!
Mwisho wa kunukuu
Tuwaondowe Maboya yaliyokivamia Chama .
Makada kwa ufukara wao wenye Elimu ya Chama wamekaa pembeni huku Maboya yaliyopenya kwa Rushwa yakikalia nyadhifa huku yakizitia unajisi kwa vile hayana yajualo kuhusu Maandiko Matakatifu ilani katiba Kanuni Miongozo na Taratibu za kimfumo
Yapo kiwizi wizi kuihujumu nchi huku yajitamkisha neno Mwenyezi Mungu iliikuwahadaa Wanyonge walio wengi wasiokuwa na uelewa wa masuala ya nchi huku Michawa iliyosoma ikakufuru na Michawa mijinga ikishangilia bila kupima mambo kwa mujibu wa ibara katiba Kanuni Miongozo na Taratibu za kimfumo
Nikashtuka Ndotoni katika Ulimwengu wa kiroho huko Usingizini huku nikiwa kimya.





Kidumu Chama Cha Mapinduzi





Mathias Mugerwa Kahinga
 
Back
Top Bottom