Chenji na karaha za konda


Nakuunga mkono kabisa katika hili. Lakini pia kuna wale abiria ambao haweki nauli yake karibu hadi konda adai ndo ataanza kusukumana na abiria wengine katika harakati za kuitafuta hiyo nauli hivi kuna ugumu gani mtu kupanda daladala ukiwa na nauli yako mkononi au sehemu ya karibu?

Sometimes ndo mana tunafuatwa na vibaka wanatupora mabegi/ wallets maana mtu hadi afungue lipochi lote kibaka anaona simu, nyekundu anaziona n.k
 
nikisikia wakisema konda napata kichefu chefu kabisa maana yale makwapa ni balaaa...........
 
na matusi usiseme....pesa yako mwenye lakini unatukanwa kama kawa......
 
kweli abiria wengine wamezidi...we mtu unatoka kwako asubuhi na mapema unafika kwenye gati unampa konda 10,000 sasa hapo si unataka ubaya kwa babaubaya? ustaarabu ni kitu cha muhimu sana kwenye jamii yoyote ile na sio kukomoana
 
Abiria tuache kulalamika na tukubali ukweli kwamba, Hao Makondakta na Madereva wa hivo Daladala wameajiliwa. Na kwamba mwisho wa siku (Jioni/usiku) wanapeleka gari na pesa kwa tajiri yao (Mwenye gari ama msimamizi). Siku inayofuata, wanachukua gari (Bila pesa, si walishakabidhi jana yeke, isitoshe wanapewa kiwango kwa siku), Hivo wanapochukua gari wanaanza hiyo siku bila pesa, sometimes hata mafuta ni yakutosha trip moja tu then wanajaza kutokana na pesa walizokusanya kwa abiria.

Huku kulalamika jamani hatuwatendei haki hata kidogo. Isitoshe huwa inafikia wakati wananunua chenji (mfano, Noti ya Tsh 1000 ananunua kwa change ya Tsh 900). Hesabu ya tajiri jioni iko pale pale, haijalishi kanunua change ama kamlipa mpiga debe.

Hutaki usumbufu, nenda na hela inayotosha nauli tu, vinginevyo jiandae na hizo kejeli na matusi. Sasa wewe unampa Tsh 10,000 asubuhi asubuhi, nauli Ths 300 jamani, unategemea nini? Mbona mchana huwa sio wakorofi? (Ni kwa sababu wameshafanya kazi ama maduka, vibanda n sehemu zingine za kupata change zinakuwepo).

Ni hayo tu.

lizy
 
Ah ah ah ah ah... umenikumbusha mdada mmoja, "alijitia kumkaripia konda wakati wa kutoa nauli kuwa pesa yake ipo mbali. Konda kamsubiri wakati wa kushuka mdada akajitia kasahau, kupiga hatua mbili konda kamshukia kuchuwa nauli. Mdada wa watu akatumia dakika kumi nzima kusaka nauli kwenye kipima joto chake... Mwisho mdada akamwambia konda... ai jamani si unisamehe tu... hela yenyewe ipo mbali jamani na mimi nina haraka... konda akamshupalia akamwambia ...una haraka una har1sha, towa pesa bana wacha kunirembulia mimacho kama kinyonga karamba ugoro hapa...mpaka mdada wa watu akatoa pesa uku uso kaukunja ...!"

Kwa ukweli kazi ya ukonda na dereva wa daladala, ni moja ya kazi ngumu sana, hawa jamaa wanapata ukichaa wa muda, kwa sababu ya kukosa usingizi wa kutosha, hawa jamaa wanalala nadhani masaa matatu tu... Wanaamka saa tisa za usiku na wanamaliza kazi saa sita usiku. Unafikiria watakuwa na akili nzuri kweli?
 
Abiria ndo mnachangia kuwafanya makonda wakorofi kwa nn usiweke nauli yako peupe au kuishika mkononi unataka mpaka konda adai mara kumi ndo utoe?
 

X-PASTER yaani umenichekesha hadi nimetoa machozi..... huyu konda matusi haya kajifunza au kabuni mwenyewe? Eti haraka unaharisha na kinyonga karamba ugoro duh .... huyu dada hatakaa asahau kamwe!
 
Tatizo la makonda walio wengi ni inferiority complex,inawafanya wawe jinsi walivyo.Usafirishaji ni biashara kama ilivyo duka na biashara nyingine.Wanapaswa kujua wanadili na watu direct hivyo wanatakiwa watumie kila strategy za kibiashara ikiwa pamoja na customer care.Kama ni konda makini kwa nini usiandae chenji zako jioni kabisa ili asubuhi usipate shida na ukizingatia unakuwa umeshajua tatizo la chenji lipo?

Na hii tabia huwa inaambukiza kwa sababu kijana akija kuanza kazi anakuwa mpole sana,lakini subiri baada ya wiki moja akianza kubadilisha mboga.

Tatizo hili la customer care sio kwa makonda tu, ni kwa watanzania wengi wanaofanya biashara na hata wale wanaofanya kazi ya kuhudumia jamii moja kwa moja.

Tubadilikeni wa TZ tuwe na mtizamo wa kibiashara zaidi na sio kuridhika na vimafanikio vidogo
 
Bangi si mchezo, abiria wote unawaona ka sisimizi!

All in all kazi ya konda ni ngumu sana usipime kabisa, wengine hamlipi hata nauli humu mnajikausha hasa kwenye daladala zetu za kusimama.

Mkuu Fidel wewe daladala zote za kutoka ubungo kwenda kimara/mbezi ni staff ndo maana unawatetea sana makonda bana!!.
 
.Kama ni konda makini kwa nini usiandae chenji zako jioni kabisa ili asubuhi usipate shida na ukizingatia unakuwa umeshajua tatizo la chenji lipo?

Ziondaughter:

Je unaweza kutuambia hawa makonda waandae vipi hizo change in advance? Kumbuka mwisho wa siku/kazi wanakabidhi pesa kwa Tajiri/mwenye gari/Msimamizi. Sasa sijui waandae hizo change kutoka wapi labda?
 

Ndugu MziziMkavu shukran sana kwa kutupasha habari kuhusu Kero za makonda asubuhi asubuhi.

Yafuatao ni mchango kwa ufupi kuhusu suala hilo.

Mimi kama mpenda usawa awali ya yote napenda kusema kuwalaumu makonda pekee yao itakuwa kuto watendea Haki na ni kuwa vunjia Heshima.

Haki itatendeka tukiangalia pande zote za sarafu kisha kutoa hukumu sahihi.

Nionavyo mimi binafsi ni Ma-Konda na Ma-Abiria asubuhi asubuhi watoao Stenzi na Denzi wote ni wenye kulaumiwa sio makonda pekee yao.

Nasema hivi kwa sababu Makonda kutoweka chenji kwa ajili ya abiria ya kwanza na pili hadi wa tatu ni wenye kulaumiwa.

Na Ma abiria kutokwenda na chenji 10300 pia wanastahili lamawama na fundisho.

Nataraji kwa ufupi huu nitaeleweka kwa undani kama sivyo tuendelee kujadiliana hadi kufika kilele cha hitimisho.

Wenu katika Utu
Mpenzi wa Islam.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…