Chenji mjini issue, Bank Of Tanzania, whyyyyy????

Buyaka

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
1,643
1,786
Ushawahi kushindwa kununua maji ya mia tano kwa sababu muuzaji hana chenji ya elfu mbili? Unataka gazeti muuzaji anakwambia chukua mawili, vinginevyo chenji hakuna.

Katika pitapita zangu katika nchi za watu sijawahi kuingia dukani hata siku moja nikaambiwa hatuwezi kukamilisha hii transaction kwa sababu eti hakuna chenji.

Lakini kwa hapa Tanzania chenji ni issue, mpaka masela wameamua kuuza hela barabarani. Hivi Benki Kuu inashindwa nini kuchapisha hizi jelo na buku na masimbe ya 50, 100 na 200 na kuyatawanya kwenye mzunguko wa hela? Inaonekana haya ma elfu kumi kumi yaliyosambaa hayakidhi mahitaji ya mtu wa kawaida na wa chini kwa sababu cash flow ya wengi ni transactions ndogo ndogo. Lakini mafisadi ambao ndio wanatengeneza hizo hela wao wanadunda na mekundu mekundu, hivyo kwao sio tatizo. Wanabaki kuwachimbia mkwara wauza chenji badala ya kutatua kiini cha tatizo.

Tutajengaje uchumi wa nchi wakati tunajingenezea wenyewe mazingira ya kukinza biashara, what the eff is wrong with BOT?
 
Back
Top Bottom