Chenge, Tibaijuka, Kilaini walipuliwa mabilioni ya IPTL

Chenge, Tibaijuka, Kilaini walipuliwa mabilioni ya IPTL

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
78,513
Reaction score
167,153
Dar es Salaam. Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imewataja vigogo wa serikali, wanasiasa na viongozi wa dini watatu walionufaika na uchotwaji wa Sh306 bilioni katika Akaunti ya Tegeta Escrow na jinsi baadhi walivyotumia mifuko ya plastiki kuzibeba.

Akisoma maoni ya kamati hiyo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Zitto Kabwe aliwataja waliochukua fedha hizo kutoka kwa mkurugenzi wa VIP, James Rugemalira na kiwango walichopokea katika mabano kuwa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti na Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge (Sh1.6 bilioni) na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka (Sh1.6 bilioni).

Wengine ni aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini ambaye pia ni mbunge wa Sengerema, William Ngeleja (Sh40.4 milioni), aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona (Sh40.4 milioni), Mbunge mstaafu wa Sumbawanga (CCM), Paul Kimiti (Sh40.4 milioni), aliyekuwa mjumbe wa Bodi ya Tanesco, Dk Enos Bukuku (Sh161.7 milioni).

Alisema majaji walioingiziwa fedha ni Jaji Profesa Eudes Ruhangisa (Sh404.25 milioni) na Jaji A.K Mujulizi (Sh40.4 milioni).

Kwa upande wa watumishi wa umma, Zitto alisema kuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usajili wa Vizazi na Vifo (Rita), Philip Saliboko (Sh40.4 milioni), aliyekuwa Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji (TIC), Emmanuel Daniel Ole Naiko (Sh40.4 milioni) na ofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Lucy Appollo (Sh80.8 milioni).

Askofu Kilaini atajwa
Zitto alisema, “Kwa upande wa viongozi wa dini ambao waliingiziwa fedha na Benki ya Mkombozi ni Askofu Methodius Kilaini (Sh80.9 milioni), Askofu Eusebius Nzigirwa (Sh40.4 milioni) na Padri Alphonce Twimannye Simon (Sh40.4 milioni).

Aliongeza, “Kamati ya PAC ilithibitishiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru kuwa baadhi ya watu walienda kugawana fedha kwenye benki tajwa (Mkombozi) wakiwa na mifuko ya rambo, sandarusi, maboksi, magunia na lumbesa.”

Mkurugenzi Rugemalira
Zitto alisema Mkurugenzi Mtendaji wa VIP Engeneering, James Rugemalira alipata mgawo wa Dola za Marekani Sh75 milioni kutoka katika fedha zilizokuwa kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow na kuzigawa kwa watu mbalimbali.

Rugemalira ambaye alikuwa na hisa 3 kati ya 10 za kampuni ya IPTL, alichukua kiasi hicho cha fedha na kukipeleka katika Benki ya Mkombozi inayomilikiwa na Kanisa Katoliki.

Zitto alisema Rugemalira alionekana kuhusika na IPTL pale alipofungua shauri mahakamani kuomba kuiondoa IPTL kwenye ufilisi na kisha kuuza hisa zake kwa kampuni ya PAP.

Alisema baada ya uamuzi wa Kahakama Kuu kutolewa Septemba 5, 2013, fedha za Escrow zilitolewa kwa haraka na kupelekwa katika benki hiyo baadaye kugawiwa kwa vigogo hao.

Kamati hiyo imekabidhiwa taarifa za Benki za Stanbic na Mkombozi ambazo zimeonyesha namna ambavyo fedha zilichukuliwa na watu na kampuni mbalimbali.

Ripoti hiyo ya PAC iliyosomwa jana ilikuwa na kurasa 116 na maneno 16,979.
 
Legend
6c83222e842fae6769d4260f6f743279.jpg
 
Hawa wote waliopokea pesa za wizi ni wa kutia rumande ili waunganishwe na kesi ya wezi singa Rugemarila bila kumsahau yule mnikulu Shaban Gurumo na mke wa kizito Ikulu aliyedaiwa kupokea kati ya bilioni 2 mpaka 5 za pesa za wezi.
 
Mwizi mwingine wa pesa za Escrow huyu hapa.

MAJIBU tata ya Mnikulu, Shabani Gurumo mbele ya Baraza la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma yalizua mshangao kwa wananchi waliokuwepo.

Pia utetezi huo ulizua mvutano mkubwa kati ya Gurumo na wanasheria wa sekretarieti ya maadili, kwa upande mmoja, na pia mvutano kati ya wanasheria hawa na wakili wa Gurumo, kwa upande mwingine.

Mwansheria: Majina yako kamili ni yapi kiongozi?

Gurumo: Naitwa Shaban Rajab Gurumo.

Mwanasheria: Kiongozi, unaweza ukaliambia Baraza hili unafanya kazi gani?

Gurumo: Kazi yangu ni mnikulu. Nasimamia watumishi wote wa ndani ya Ikulu; nasimamia ukarabati wa majengo yote ya Ikulu; naratibu ikulu ndogo zote nchini; napokea mabalozi wapya kutoka nchi za nje; na ninaandaa tafrija zote za ikulu zinazomhusisha rais.

Mwansheria: Kiongozi, akaunti namba 00110102645401 iliyofunguliwa Benki ya Mkombozi 04 Februari mwaka 2014 ni ya nani?

Gurumo: Akaunti hiyo ni yangu. Niliifungua baada ya rafiki yangu James Rugemalira kunielekeza nifungue akaunti katika benki hiyo?

Mwansheria: Kiongozi, tarehe 05 Februari 2014 akaunti hiyo ilipokea shilingi 80,850,000. Hiyo fedha ni mali ya nani?

Gurumo: Hiyo fedha ni mali yangu halali.

Mwansheria: Kiongozi, hiyo fedha ulipewa na nani?

Gurumo: Nilipewa na rafiki yangu aitwaye James Rugemalira.

Mwanasheria: Kiongozi, wewe na James Rugemalira mlifahamiana vipi na tangu lini?

Gurumo: Sikumbuki vizuri. Lakini nadhani nilimfahamu tangu zamani kupitia daktari wa familia yangu aitwaye Fred Limbanga, ambaye nimekuja naye hapa leo kama shahidi.

Mwansheria: Kiongozi, kwenye nakala ya Ankara za benki uliyowasilisha katika ofisi za sekretarieti ya maadili inaonekana fedha hizo zilitoka kampuni ya VIP Engineering and Marketing Ltd na sio kwa James Rugemalira. Unasemaje kuhusu jambo hili?

Gurumo: (Anatazama nakala ya ankara kwanza). Ndio leo nimeligundua jambo hili. Hapo kabla sikuwa nimechukua muda kuisoma ankara hii. Muda wote nilijua fedha zimetoka kwa James Rugemalira.

Mwansheria: Kiongozi, hiyo fedha ulipewa kwa ajili gani na ziliambatana na masharti gani?

Gurumo: Sikuambiwa ni kwa sababu gani na hakuna masharti yoyote niliyopewa kuhusu matumizi yake. Naomba akaulizwe James Rugemalira.

Mwanasheria: Kiongozi, James Rugemalira alikuingizia fedha hizo kwa sababu uliziomba au hapana?

Gurumo: Sikumwomba James Rugemalira fedha. Na sijui kwa nini aliniwekea fedha hizo. Hata aliponiambia nifungue akaunti benki ya Mkombozi ili aniwekee fedha sikumwuliza fedha hizo ni za nini. (Kicheko kutoka kwa wananchi).

Mwansheria: Kiongozi, kwa sasa karibu fedha yote umekwisha kuitumia. Uliitumia katika mambo gani na kwa nini?

Gurumo: Niliitumia katika matumizi mbalimbali yakiwemo matibabu ya ugonjwa wa kansa uliokuwa unamsumbua mke wangu.

Mwansheria: Kiongozi, fedha hizo ambazo umekiri ni mali yako, uhalali wake unatokana na nini. Ni mshahara, posho, faida katika biashara, urithi, kuokota, zawadi au kitu gani?

Gurumo: Sio mshahara, posho, faida katika biashara, urithi, au zawadi. Pia hazikuokotwa. Ni fedha nilipewa tu. (Kicheko kutoka kwa wananchi).

Mwansheria: Kiongozi, unawezaje kutumia fedha nyingi kiasi hicho bila kwanza kutafiti sababu fedha hizo kuingizwa katika akaunti yako?

Gurumo: Sikuwa na hofu yoyote kwani James Rugemalira ni rafiki yangu kwa zaidi ya miaka kumi sasa.

Mwansheria: Kiongozi, kwa mujibu wa sheria ya maadili ya viongozi wa umma, umewahi kutoa taarifa ya fedha hizi kwenye sekretarieti ukionyesha kwamba ni miongoni mwa mali yako mpya?

Gurumo. Tayari. Nilifanya hivyo tangu 29 Desemba, 2014 kupitia fomu maalum. Fedha hizi zimetajwa kwenye ukurasa wa kumi na saba. (Anaonyesha nakala ya fomu aliyoijaza).

Baada ya kikao, MwanaHalisi Online ilipata fursa ya kungea na wanasheria wa sekretarieti ya maadili kuhusu maana ya neno “zawadi” kwa mujibu wa sheria. Swali hilo pia nililielekeza kwa wakili wa Gurumo.

Kwa upande wake, Gurumo alisema neno hilo halina fasili rasmi katika sheria za Tanzania. Lakini, wanasheria wa shekretarieti walikuwa na maoni tofauti.

Walisema, “Gurumo amekiri kwamba fedha zile ni mali yake. Mali inaweza kupatikana kupitia mshahara, posho, biashara, urithi, kuokota, au zawadi. Gurumo amekanusha yote haya. Kwa hiyo fedha hizo anazimiliki kwa mujibu wa kanuni gani?,” walihoji.
 
Wafunguliwe mashtaka fasta na wakakae selo!
 
You be come the first place to comment in thread
Swissme
Mkuu swisme,
Umeteleza kidogo rekebisha hiyo ngeli kabla ma SISIEM hayajaja,

Hongera kwa kamati ya bunge, kazi nzuri.
 
Izi ni figisu figisu tu za Zitto na CCM anayotumikia sasa.....af kwan ilkua shs ngap...mara 309bn...mara 306bn...which is which???...Mkamateni na huyo mstaafu wenu kama mnataka tuwaamini kwenye hili
 
Hawa wote waliopokea pesa za wizi ni wa kutia rumande ili waunganishwe na kesi ya wezi singa Rugemarila bila kumsahau yule mnikulu Shaban Gurumo na mke wa kizito Ikulu aliyedaiwa kupokea kati ya bilioni 2 mpaka 5 za pesa za wezi.
Soon utawaona kizimbani
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom