Chenge Kiporo cha Lema

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
ANDREW Chenge, Mbunge wa Bariad Magharibi, hajaponyoka mikononi mwa Godbless Lema, Mbunge wa Arusha Mjini, anaandika Happiness Lidwino.

Licha ya hotuba ya Godbless Lema, Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kutosomwa bungeni jana, hotuba yake ilimgusa Chenge katika sakata la rada. Kifuatayo ni kipengele hicho.

Mheshimiwa Spika, Mh Andrew Chenge (MB) ametuhumiwa na imethibitika hapa Bungeni na katika taasisi za Uchunguzi za Kimataifa (SFO) kuwa alihusika kwa karibu na kwa ufanisi katika sakata la kashfa ya ununuzi wa rada ya Taifa.

Mheshimiwa Spika, Mwandishi Andrew Feinstein , Colonel .U.S. Army (retired) katika Kitabu chake “ THE SHADOW WORLD – Inside the Global Arms Trade, katika ukurasa wa 188-196, amefanya uchambuzi wa kina jinsi Andrew Chenge alivyofanikiwa kukwapua fedha za Wananchi kiasi cha pesa za Kimarekani dolari 1.2 milioni kupitia Kampuni yake ya Franton Investment Ltd Jersey na Kampuni hii ya Andrew Chenge ikampa aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Dr. Idrissa Rashid pesa za Kimarekani dolari $600,000 kupitia Kampuni ya Gavana huyu inayojulikana kwa jina la Langley Investment Ltd.

Mheshimiwa Spika, Lakini kwenye utawala huu wa utumbuaji majipu, Andrew Chenge ni Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na M/kiti wa Kamati ya sheria ndogo, jambo hili lina sura ya dharau na fedhea kwa Bunge lako tukufu na kwa jamii.

Mheshimiwa Spika, Wako wengi wenye sura hizi za Mh Chenge na wengine ni Mawaziri ambao wamekuwa na kashfa mbali mbali kwenye Serikali iliyopita lakini wameonekana kwenye madaraka tena katika Serikali hii ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais aneyeamini katika utumbuaji majipu , wakati kuna majipu mengine asiyoweza kuyatumbua ndani ya baraza la Mawaziri.

Mheshimiwa Spika, Taifa linapokuwa na huzuni juu ya utawala unaopuuza na kudharau Wananchi , kwa vyovyote vile hali ya amani na usalama inakuwa mashakani na kuwatia moyo watumishi wengine wa Umma katika masuala yanayohusu ufisadi, rushwa na ubadhirifu kwamba sio mambo mabaya. Ndio maana imekuwa ni vigumu kukemea rushwa katika ngazi mbalimbali za utawala wa nchi hii ikiwemo Jeshi la Polisi.

6.2 Kuingiliwa kwa Uhuru wa Bunge na Mhimili wa Dola

Mheshimiwa Spika, tishio lingine la hali ya usalama Nchini ni Serikali kuingilia Uhuru wa Bunge , ni ajabu kubwa kwamba chombo kinachopanga matumizi ya fedha za Serikali ni Bunge , lakini kwa wakati huu tumeona Serikali ikiondoa matangazo ya moja kwa moja ya Bunge kwa kisingizio cha kubana matumizi , kazi ambayo hata hivyo kama ingekuwa ni hoja basi jambo hilo lingefanywa na Bunge na sio Serikali.

Mheshimiwa Spika, Wananchi kupata habari na kujua wanachojadili wabunge wao ni hitaji la lazima la Kikatiba na sio hisani ya Serikali, malumbano yetu dhidi ya hoja mbali mbali ndani ya Bunge yalikuwa ni muhimu kwa ustawi wa usalama wa Nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, Wananchi , walipotuona kupitia vyombo vya habari mbali mbali , tukilumbana juu ya maisha na maendeleo yao , jambo hili lilikuwa linasidia kupunguza tension na uchungu kwa jamii kwani walikuwa wanashuhudia tukipigana na kulumbana juu ya ustawi wa maisha yao , walipata matumaini waliposikia majibu ya Serikali hata kama yalikuwa ni uongo.

Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni inasikitishwa na jinsi Bunge letu linavyoendelea kukosa nguvu na kuingiliwa na mihimili mingine ya dola kwa kuelekezwa ni kipi cha kufanywa na kipi si cha kufanywa. Ni wazi sasa bila chenga kuwa Bunge hili limeingiliwa na dola na sasa ni Bunge kibogoyo jambo linalohatarisha usalama na amani ya nchi, kwa kuwa Dola sasa inaweza kufanya chochote na isionekane kukemewa na Bunge ambalo kazi yake ni kuisimamia Serikali, badala yake sasa hivi Serikali ndio inalisimamia Bunge.

Mheshimiwa Spika, kisingizio cha gharama kubwa za kurusha matangazo ni uongo mkubwa ambao hata shetani anaushangaa, kwani hata vyombo vingine vya habari vilivyokuwa vinarusha matangazo ya “live” kwa gharama zao navyo vimezuiwa sio na Serikali bali na uongozi wa Bunge uliodhibitiwa na Serikali ya Dkt. Magufuli.
 
Katika jambo ambalo wamekosea Ni kuzuia risala ya Lema isisomwe mpaka sasa wananchi wanajua serikali hii iliyokuwa kila siku kuwa italalanao mbele mafisadi sasa hivi ndiyo kinara wa kukumbatia ufisadi
 
Unamjua chenge au unamsikia?,
yaani mwandishi wa marekani atunge novel ya kumtia hatiani chenge na akaweza kweli?

Mwandishi hawezi mtia hatiani Chenge! Mwandishi kaelezea jinsi Chenge alivyofanikisha mchakato!! Au hujasoma maelezo? Kilichomtia mtia hatiani ni taarifa ya SFO au we mgeni?
 
SFO ndo TAKUKURU labda.,kwamba mahakama zetu zitafuata ushahidi huko?.

By the way,wamempea lema cheti cha usajili wa hilo kampuni la me chenge kuthibisha kuwa ni la kwake?
 
Mungu siku moja atatusaidia kusafisha damu chafu hapa Tanzania maana ndio inasababisha majipu.
 
Mwandishi hawezi mtia hatiani Chenge! Mwandishi kaelezea jinsi Chenge alivyofanikisha mchakato!! Au hujasoma maelezo? Kilichomtia mtia hatiani ni taarifa ya SFO au we mgeni?
Mkuu, shida ni lugha iliyotumika hapo; Lema ameyachukua maneno kama yalivyo so labda msomaji wako ana aleji na hiyo lugha ya malkia.
 
Wakat utawala wa Magu unaanza nilijua hakuna kipindi wabunge wa ccm watakuwa na hoja nzito na nzur kama msimu huu sabab wataongea openly, kumbe vise vercer its true
 
ANDREW Chenge, Mbunge wa Bariad Magharibi, hajaponyoka mikononi mwa Godbless Lema, Mbunge wa Arusha Mjini, anaandika Happiness Lidwino.

Licha ya hotuba ya Godbless Lema, Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kutosomwa bungeni jana, hotuba yake ilimgusa Chenge katika sakata la rada. Kifuatayo ni kipengele hicho.

Mheshimiwa Spika, Mh Andrew Chenge (MB) ametuhumiwa na imethibitika hapa Bungeni na katika taasisi za Uchunguzi za Kimataifa (SFO) kuwa alihusika kwa karibu na kwa ufanisi katika sakata la kashfa ya ununuzi wa rada ya Taifa.

Mheshimiwa Spika, Mwandishi Andrew Feinstein , Colonel .U.S. Army (retired) katika Kitabu chake “ THE SHADOW WORLD – Inside the Global Arms Trade, katika ukurasa wa 188-196, amefanya uchambuzi wa kina jinsi Andrew Chenge alivyofanikiwa kukwapua fedha za Wananchi kiasi cha pesa za Kimarekani dolari 1.2 milioni kupitia Kampuni yake ya Franton Investment Ltd Jersey na Kampuni hii ya Andrew Chenge ikampa aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Dr. Idrissa Rashid pesa za Kimarekani dolari $600,000 kupitia Kampuni ya Gavana huyu inayojulikana kwa jina la Langley Investment Ltd.

Mheshimiwa Spika, Lakini kwenye utawala huu wa utumbuaji majipu, Andrew Chenge ni Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na M/kiti wa Kamati ya sheria ndogo, jambo hili lina sura ya dharau na fedhea kwa Bunge lako tukufu na kwa jamii.

Mheshimiwa Spika, Wako wengi wenye sura hizi za Mh Chenge na wengine ni Mawaziri ambao wamekuwa na kashfa mbali mbali kwenye Serikali iliyopita lakini wameonekana kwenye madaraka tena katika Serikali hii ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais aneyeamini katika utumbuaji majipu , wakati kuna majipu mengine asiyoweza kuyatumbua ndani ya baraza la Mawaziri.

Mheshimiwa Spika, Taifa linapokuwa na huzuni juu ya utawala unaopuuza na kudharau Wananchi , kwa vyovyote vile hali ya amani na usalama inakuwa mashakani na kuwatia moyo watumishi wengine wa Umma katika masuala yanayohusu ufisadi, rushwa na ubadhirifu kwamba sio mambo mabaya. Ndio maana imekuwa ni vigumu kukemea rushwa katika ngazi mbalimbali za utawala wa nchi hii ikiwemo Jeshi la Polisi.

6.2 Kuingiliwa kwa Uhuru wa Bunge na Mhimili wa Dola

Mheshimiwa Spika, tishio lingine la hali ya usalama Nchini ni Serikali kuingilia Uhuru wa Bunge , ni ajabu kubwa kwamba chombo kinachopanga matumizi ya fedha za Serikali ni Bunge , lakini kwa wakati huu tumeona Serikali ikiondoa matangazo ya moja kwa moja ya Bunge kwa kisingizio cha kubana matumizi , kazi ambayo hata hivyo kama ingekuwa ni hoja basi jambo hilo lingefanywa na Bunge na sio Serikali.

Mheshimiwa Spika, Wananchi kupata habari na kujua wanachojadili wabunge wao ni hitaji la lazima la Kikatiba na sio hisani ya Serikali, malumbano yetu dhidi ya hoja mbali mbali ndani ya Bunge yalikuwa ni muhimu kwa ustawi wa usalama wa Nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, Wananchi , walipotuona kupitia vyombo vya habari mbali mbali , tukilumbana juu ya maisha na maendeleo yao , jambo hili lilikuwa linasidia kupunguza tension na uchungu kwa jamii kwani walikuwa wanashuhudia tukipigana na kulumbana juu ya ustawi wa maisha yao , walipata matumaini waliposikia majibu ya Serikali hata kama yalikuwa ni uongo.

Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni inasikitishwa na jinsi Bunge letu linavyoendelea kukosa nguvu na kuingiliwa na mihimili mingine ya dola kwa kuelekezwa ni kipi cha kufanywa na kipi si cha kufanywa. Ni wazi sasa bila chenga kuwa Bunge hili limeingiliwa na dola na sasa ni Bunge kibogoyo jambo linalohatarisha usalama na amani ya nchi, kwa kuwa Dola sasa inaweza kufanya chochote na isionekane kukemewa na Bunge ambalo kazi yake ni kuisimamia Serikali, badala yake sasa hivi Serikali ndio inalisimamia Bunge.

Mheshimiwa Spika, kisingizio cha gharama kubwa za kurusha matangazo ni uongo mkubwa ambao hata shetani anaushangaa, kwani hata vyombo vingine vya habari vilivyokuwa vinarusha matangazo ya “live” kwa gharama zao navyo vimezuiwa sio na Serikali bali na uongozi wa Bunge uliodhibitiwa na Serikali ya Dkt. Magufuli.
Mbona imejaa kunakili taarifa za magazeti na SFO tu. Mawazo ya Lema yako wapi? Hivi hawa wajinga wanaijua bajeti kweli? Hivi watumishi wanaohudumiwa na hii wizara wanajua nini upinzani unachowawazia katika kuboresha maisha yao?
Jamani, kuweni na akili. Badilisheni hii mbinu kwani watu wamechoka unafiki wenu. Lema alimuita Lowasa kila jina la ufisadi, leo kabadilika na kumuita Lowasa ni mtukufu. Mbinu hii mmeishaitia dosari hivyo tumieni mbinu mpya.
 
Mwandishi hawezi mtia hatiani Chenge! Mwandishi kaelezea jinsi Chenge alivyofanikisha mchakato!! Au hujasoma maelezo? Kilichomtia mtia hatiani ni taarifa ya SFO au we mgeni?
Hiyo ni clue kwa vyombo vyetu vya uchunguzi hapa Tz kama vingekuw serious, lkn kwakuwa lengo ni kumlinda na kumsafisha basi,tusome hiyo novel na kuifurahia kama mazezeta!
 
Bado kuna majuha wamekaririshwa kuwa chadema sasa kinatetea mafisadi, hii imekuwa somo zuri kwa wajinga hawa kujua nani anatetea ufisadi na nani anapinga. Jicho la makengeza mtuhumiwa wa ufisadi kwenye utawala wa mtu anayejitanabaisha kuupinga ufisadi anapewa nafasi nyeti, bado mnakariri atawakamata mafisadi, mmerogwa
 
Hiyo ni clue kwa vyombo vyetu vya uchunguzi hapa Tz kama vingekuw serious, lkn kwakuwa lengo ni kumlinda na kumsafisha basi,tusome hiyo novel na kuifurahia kama mazezeta!

Nakumbuka yuko mwanasiasa mwingine alituhumiwa SFO na walikuja hapa bongo kumpeleleza. Mpinzani huyo inasemekana ana mijengo ya kutosha yuko London.
 
Nikweli wenye sura za chenge wapo wengi sana hata mgombea wa uraisi kupitia UKAWA Lowasa nae anasura hiyo hiyo ya chenge
 
Back
Top Bottom