Chenge: Jeuri yake ni kaburi la CCM

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
26,362
Reaction score
39,842

Hatimaye nyoka mwenye makengeza ameweza kupuruchuka kuwekwa kikaangoni kwa kukiuka maadili ya Uongozi wa Umma.

Malalamiko dhidi yake yalikuwa yasikilizwe tangu juzi tarehe 24/2/2015 ambapo aliibuka barazani akiwa na court injuction kulizuia Baraza la Maadili kumhoji kwa kuwa kesi yake ipo mahakamani hivyo asihojiwe katika Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma hadi kesi yake itakapotolewa uamuzi na mahakama inayosikiliza kesi ya awali kuhusu ESCROW. Kama haitoshi huku akijua Baraza linaweza kuja na maamuzi ya kutupilia mbali ZUIO lake ameamua kukata rufaa Mahakama Kuu kuhusu ufafanuzi wa yeye kuhojiwa na Baraza la Maadili kuhusu ESCROW.

Fafanuzi nyingi zilizotolewa na weledi wa Sheria ni kwamba, kimsingi Baraza lilanolisikiza malalamiko dhidi ya Chenge na wenzake haliingilii kesi za msingi ama zinazoendelea kwenye mahakama. Kwani hakuna kesi inayohusu kukiukwa maadili ya Uongozi ambayo imewahi kufunguliwa mahakamani kuhusiana na sakata la ujambazi wa pesa kutoka ESCROW Account. Hivyo pia Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi haina penal code zaidi sana inaishia kutoa ushauri kwa mamlaka husika kuhusu uthibitisho wa malalamiko dhidi ya mlalamikiwaji ili hatua stahiki zichukuliwe ambazo inawezekana mtu akaondolewa ktk nafasi yake ya uongozi, kushtakiwa mahakamani, kufilisiwa ama hatua zingine zozote za kinidhamu.

Chenge, ametia aibu kubwa taaluma ya Wanasheria nchini, siyo tu kutajwa bali kwa ushahidi ameshiriki matukio mengi kama siyo yote makubwa ya kijambazi dhidi ya pesa za umma, mikataba yenye utata na hata kufikia uhalifu wa kuficha pesa nje ya nchi ambazo yeye anaziita vijisenti. Inawezekana anayafanya haya akijua ukweli wa ndani kabisa kuwa hakuna wa kumchukulia hatua kwani aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu na anajua wapi abane na wapi ajifiche kupitia sheria ambazo amewahi kuwa msimamizi wake mkuu. Mchezo uliochezwa mbele ya Baraza la Sekretarieti ya Maadili hauvumiliki na haupendezi hata kidogo.

Narejea maneno ya Baba wa Taifa aliposema "Bila CCM IMARA nchi itayumba" hii kauli ni fupi lakini nzito na ina mantiki kubwa sana. Tukiamua leo kuandika historia ya uimara wa CCM itakuja kugundulika kwamba ilishakwenda na Nyerere.

Kuvumilia uozo imekuwa hulka yetu sisi Watanzania wa leo. Ukiwaacha viongozi ambao kwao uozo ni godoro la sufi la kulalia, sisi wananchi tumefikia mahala kuwaenzi wahuni wanaowajibishwa kwa kukiuka miiko ya uongozi na tunawapokea majimboni kama washindi na wafalme, ndiyo maana mtu kama Chenge amepewa hadhi ya Uchifu huko kwao, Siyo kwa sababu ya uongozi wake bali kwa sababu ya wingi wa pesa alizoiba na ubabe wa kipuuzi dhidi ya dola na watu hivyo ameonekana ni shujaa.

Leo tunaendelea kuwaita waheshimiwa wale wote wanaotukejeli na kutupuuza na tunaendelea kuwapa kura kwa kishindo eti Chama kisianguke. Tunashindwa kuwawajibisha majizi na hatimaye tunawapa another round for the road wakati tunajua ni madereva wanaopaswa kutuendesha bila ulevi wa madaraka....

Jeuri ya Chenge kusema kwamba yeye ni NYOKA mwenye makengeza anayeangalia mahala pesa ilipo si ya kuichekea hata kidogo. Hivi tangu lini uongozi ukawa ni mtaji wa biashara? Je sanduku la kura ndilo linaloamua nani awe tajiri na nani awe maskini? Inawezekana hii kasumba imeanza kutulevya Watanzania na tukafikia kuona kwamba hayo ndiyo majaliwa yetu. Tukatae kabisa upuuzi, wizi na uozo kwenye maongozi ya nchi. Hii jeuri anayoendelea kuionyesha Chenge ni dalili mbaya sana kwa CCM.

Ikumbukwe kwamba Chenge ndiye mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Chama kitaifa, yeye ameonyesha mfano mbaya kimaadili na bado hakuna mtu ndani ya chama anayestuka na biashara inaendelea kama kawaida. Ina maana bila Chenge nchi itayumba? Uimara wa CCM umepukutika na nchi inayumba sana. Muda bado ungalipo ili chama kijisafishe kiingie ktk ngwe ya uchaguzi kikiwa kimetakata. Watanzania wanazidi kufunguka fahamu zao na sasa wanaelekea kuchoshwa na mwenendo wa kulindana na kuoneana haya katika masuala ya msingi ya kitaifa.

Katika msahafu wa Wakristo imetajwa kwamba Mungu ni baba yetu, na pia shetani ni baba wa waovu. Sisi watanzania tulimchagua mioyoni mwetu kuwa Nyerere awe Baba wa Taifa, hivyo napendekeza sasa Chenge aitwe baba wa UFISADI nchini.
 
Duh!Chenge ndie mwenyekiti wa kamati ya maadili ya maccm?
 
CCM ni sawa na ukoo wa panya: baba mwizi, 'mama mwizi, babu mwizi, bibi mwizi, motto mwizi, kaka mwizi, dada mwizi, mjomba mwizi, shangazi mwizi, mkwe mwizi' BY Mh. Nassari
 
Kwa tabia aliyoonyesha nyoka mwenye makengeza ni DHARAU kubwa kwa CHAMA chake na wapiga KURA wake. Kweli pesa ndiyo kila kitu Tanzania. Ile dharau watu wengi waliona kupitia vituo vya luninga na watu wanajiuliza hivi ndiyo wakubwa wa nchi hii wanavyodharau vyombo vya kisheria.
 
kijapo kiburi ndipo lijapo anguko,kiburi cha ccm na viongozi wake hata wakashindwa kuwasikiliza wananchi ndio anguko lao
 
Hakuna mwenye uwezo wa kumwajibisha chenge serikalini wala kwenye chama kamwe! Katiba pendekezwa imetungwa na kuandikwa na fisadi chenge, ndiyo katiba ambayo jk anasema ni katiba bora afrika. Ndani ya ccm wote wameoza, kilichobaki ni kugawana vyeo kama njugu tu. Period!
 
hua najiulza kiburi hiki chenge anakitoa wapi? na huko ccm akuna mtu wa kumkanya? yaan jamaa anafanya anachojickia na hakuna wa kumhoji " kwel ccm ina wenyewe
 
Tufanye utafiti.
Kwa nini anaogopwa na mamlaka za nchi yetu?
Tatizo mnasukumwa na hisia kuliko ukweli na sheria. Je umeshajiuliza ikiwa kweli ni mchafu kiasi hicho mbona hajafukuzwa katika Chama na pia hajafikishwa mahakamani?
 
Tatizo mnasukumwa na hisia kuliko ukweli na sheria. Je umeshajiuliza ikiwa kweli ni mchafu kiasi hicho mbona hajafukuzwa katika Chama na pia hajafikishwa mahakamani?
Hebu tuanze na sakata la rada (BAE) ambapo vyombo vya uchunguzi vya Uingereza vimemhusisha na rushwa aliyopokea na kuificha kwenye offshore account....
Naomba unitoe tongotongo kuhusu usafi wake hapo ili tusonge mbele na tuhuma zingine
 
A powerful gang is backing him up cuz if he goes down,the whole gang goes down.Y'all know who am talking about.
 
Hebu tuanze na sakata la rada (BAE) ambapo vyombo vya uchunguzi vya Uingereza vimemhusisha na rushwa aliyopokea na kuificha kwenye offshore account....
Naomba unitoe tongotongo kuhusu usafi wake hapo ili tusonge mbele na tuhuma zingine
Yote yaliandikwa, lakini kiukweli ni kuwa yalibaki hisia tu. Kungekuwa na uthibitisho wa kumhusisha yeye na sakata hilo kijinai angepelekwa mahakamani. Kuwa na Account nje na pesa hizo siyo kosa kwa mujibu wa sheria zetu mpaka sasa ikiwa tu unaweza kuelezea zimepatikanaje. Nina hakika Mh alieleza kwa ufasaha alizipataje na zikaonekana ni za halali ndiyo maana hakupelekwa kwa Pilato.
 
Aisee, inaelekea jamaa anaona mbali sana na is an advanced and professional corrupt!
Umeshahau
Na ni chenge aliyetunga katiba iliyoondoa maadili kama tunu ya taifa
Katiba hiyo inaitwa "Katiba bora" na MaCCM
Sasa hebu fikiri zaidi hapo
Katika msahafu wa Wakristo imetajwa kwamba Mungu ni baba yetu, na pia shetani ni baba wa waovu. Sisi watanzania tulimchagua mioyoni mwetu kuwa Nyerere awe Baba wa Taifa, hivyo napendekeza sasa Chenge aitwe baba wa UFISADI nchini.
 
Chenge hana jeuri yoyote bali anacheza na mfumo wa serikali dhaifu. Bila shaka anajua kwa uhakika waliiba ama kupokea fedha hizo na nani serikalini. Hata hivyo upo msemo kwamba wezi huwa mara nyingi ni jasiri.
 
Duh!Chenge ndie mwenyekiti wa kamati ya maadili ya maccm?

What? Basi kama hivyo ndivyo maadili yalishazikwa siku nyingi. Ona jinsi walivyochakachua katiba kwa kuwa tu alikuwa katibunwa hotuba.
 

Bila shaka wewe ni mtoto wake au ni mtu ambaye unafaidi ufisadi wake.
 
Tanzania six not pour country but due to the miss use of power lead to the people live in pour situation
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…