Chenge: Jeuri yake ni kaburi la CCM

Chenge: Jeuri yake ni kaburi la CCM

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
25,946
Reaction score
38,658
ANDREW CHENGE.jpg
Hatimaye nyoka mwenye makengeza ameweza kupuruchuka kuwekwa kikaangoni kwa kukiuka maadili ya Uongozi wa Umma.

Malalamiko dhidi yake yalikuwa yasikilizwe tangu juzi tarehe 24/2/2015 ambapo aliibuka barazani akiwa na court injuction kulizuia Baraza la Maadili kumhoji kwa kuwa kesi yake ipo mahakamani hivyo asihojiwe katika Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma hadi kesi yake itakapotolewa uamuzi na mahakama inayosikiliza kesi ya awali kuhusu ESCROW. Kama haitoshi huku akijua Baraza linaweza kuja na maamuzi ya kutupilia mbali ZUIO lake ameamua kukata rufaa Mahakama Kuu kuhusu ufafanuzi wa yeye kuhojiwa na Baraza la Maadili kuhusu ESCROW.

Fafanuzi nyingi zilizotolewa na weledi wa Sheria ni kwamba, kimsingi Baraza lilanolisikiza malalamiko dhidi ya Chenge na wenzake haliingilii kesi za msingi ama zinazoendelea kwenye mahakama. Kwani hakuna kesi inayohusu kukiukwa maadili ya Uongozi ambayo imewahi kufunguliwa mahakamani kuhusiana na sakata la ujambazi wa pesa kutoka ESCROW Account. Hivyo pia Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi haina penal code zaidi sana inaishia kutoa ushauri kwa mamlaka husika kuhusu uthibitisho wa malalamiko dhidi ya mlalamikiwaji ili hatua stahiki zichukuliwe ambazo inawezekana mtu akaondolewa ktk nafasi yake ya uongozi, kushtakiwa mahakamani, kufilisiwa ama hatua zingine zozote za kinidhamu.

Chenge, ametia aibu kubwa taaluma ya Wanasheria nchini, siyo tu kutajwa bali kwa ushahidi ameshiriki matukio mengi kama siyo yote makubwa ya kijambazi dhidi ya pesa za umma, mikataba yenye utata na hata kufikia uhalifu wa kuficha pesa nje ya nchi ambazo yeye anaziita vijisenti. Inawezekana anayafanya haya akijua ukweli wa ndani kabisa kuwa hakuna wa kumchukulia hatua kwani aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu na anajua wapi abane na wapi ajifiche kupitia sheria ambazo amewahi kuwa msimamizi wake mkuu. Mchezo uliochezwa mbele ya Baraza la Sekretarieti ya Maadili hauvumiliki na haupendezi hata kidogo.

Narejea maneno ya Baba wa Taifa aliposema "Bila CCM IMARA nchi itayumba" hii kauli ni fupi lakini nzito na ina mantiki kubwa sana. Tukiamua leo kuandika historia ya uimara wa CCM itakuja kugundulika kwamba ilishakwenda na Nyerere.

Kuvumilia uozo imekuwa hulka yetu sisi Watanzania wa leo. Ukiwaacha viongozi ambao kwao uozo ni godoro la sufi la kulalia, sisi wananchi tumefikia mahala kuwaenzi wahuni wanaowajibishwa kwa kukiuka miiko ya uongozi na tunawapokea majimboni kama washindi na wafalme, ndiyo maana mtu kama Chenge amepewa hadhi ya Uchifu huko kwao, Siyo kwa sababu ya uongozi wake bali kwa sababu ya wingi wa pesa alizoiba na ubabe wa kipuuzi dhidi ya dola na watu hivyo ameonekana ni shujaa.

Leo tunaendelea kuwaita waheshimiwa wale wote wanaotukejeli na kutupuuza na tunaendelea kuwapa kura kwa kishindo eti Chama kisianguke. Tunashindwa kuwawajibisha majizi na hatimaye tunawapa another round for the road wakati tunajua ni madereva wanaopaswa kutuendesha bila ulevi wa madaraka....

Jeuri ya Chenge kusema kwamba yeye ni NYOKA mwenye makengeza anayeangalia mahala pesa ilipo si ya kuichekea hata kidogo. Hivi tangu lini uongozi ukawa ni mtaji wa biashara? Je sanduku la kura ndilo linaloamua nani awe tajiri na nani awe maskini? Inawezekana hii kasumba imeanza kutulevya Watanzania na tukafikia kuona kwamba hayo ndiyo majaliwa yetu. Tukatae kabisa upuuzi, wizi na uozo kwenye maongozi ya nchi. Hii jeuri anayoendelea kuionyesha Chenge ni dalili mbaya sana kwa CCM.

Ikumbukwe kwamba Chenge ndiye mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Chama kitaifa, yeye ameonyesha mfano mbaya kimaadili na bado hakuna mtu ndani ya chama anayestuka na biashara inaendelea kama kawaida. Ina maana bila Chenge nchi itayumba? Uimara wa CCM umepukutika na nchi inayumba sana. Muda bado ungalipo ili chama kijisafishe kiingie ktk ngwe ya uchaguzi kikiwa kimetakata. Watanzania wanazidi kufunguka fahamu zao na sasa wanaelekea kuchoshwa na mwenendo wa kulindana na kuoneana haya katika masuala ya msingi ya kitaifa.

Katika msahafu wa Wakristo imetajwa kwamba Mungu ni baba yetu, na pia shetani ni baba wa waovu. Sisi watanzania tulimchagua mioyoni mwetu kuwa Nyerere awe Baba wa Taifa, hivyo napendekeza sasa Chenge aitwe baba wa UFISADI nchini.
Mada yako umeiweka vizuri sana na nimeipenda na ninawaonea huruma sana watanzania kwa kuwa viongozi waliowachagua wanawadhihaki , wanawatukana , wanawabeza, wanawakashifu na wananchi hawajui kuwa wakiamua kutowachagua tu hawa watu jeuri zao zitaisha na watapotea kabisa na kusahaulika na kubaki historia.

Ninatamani kumuona Rais wa awamu ya tano toka upinzani kwa kuwa kura za serikali za mitaa zimeonesha wazi wimbi na upepo wa mabadiliko , na sasa tutashangaa kuona kama wapiga kura watahamia upande wa majoka yenye makengeza, Betina na MAMVI!! Kwa nchi ilipofikia sasa ya watemi majoka yenye makengeza na Betina pesa ya mboga kutukana raia hadharani sasa tunahitaji Rais mpya mkali toka upinzani mwenye ubavu wa kuwatupa jela majoka yote yenye makengeza kina Chenge , Betina nk, Rais atakaeziba mianya yote ya ufisadi serikali kuu na serikali za mitaa , rais mcha Mungu anaechukia ufisadi, Rais ataezuia ujangili na kuuzwa wanyama hai ili watalii waje nchini, rais ataezuia safari za mawaziri na bongo movie kula bata nje ya nchi, rais atakeleta elimu na afya bure kama enzi za Nyerere manake mabilioni yetu yapo uswisi na escrow , Rais atakaefufua reli zote na viwanda, Rais atakewezesha kupatika maji safi na salama na umeme wa bei nafuu, Rais atakaesaidia kushuka bei ya petrol, Rais atakajali walimu na madaktari na wafanyakazi wengineo, Rais atakaejenga uwanja mpya wa kiwango wa ndege kama Kenya, Rais atakaejenga barabara za juu kama Kenya na Uganda wasiojua zipo bongo no nginjera tu miaka hamsini sana ya umaskini hakuna kitu! viongozi kazi kuiba mali ya umma tu na kusomesha watoto wao nje ya nchi ndo wanachojua!

Kuna mda nimesoma thread flani ya gamba ilikuwa na list ya majina ya wagombea toka magamba club ila bahati mbaya sana yalikuwa majina yenye ukakasi aliyoweka na a nikashangaa eti sikuona jina hata moja la mgombea mwenye sifa ya kuwa Rais wa nchi tajiri inayofilisiwa na magamba, nchi ya kusadikika ya Danganyika! Rais gani anaweza kutoka magamba club?

Rais atakeendeleza uongozi wa nchi ambayo raia wake walio wengi wamenyimwa elimu sahihi ya uraia kwa maana hawajui kuwa kulala na njaa au kuugua na kukosa matibabu ni kosa la serikali , hawajui kuwa kura ni mkataba na serikali wa kupata hali bora ya maisha kwa watu na kama serikali haiwezi kuleta hali bora inatakiwa iwapishe wengine au mwananchi kuchagua serikali toka chama kingine , hivi ndivyo ulaya na marekani wameendelea , serikali ikishindwa kuwapa wananchi hali bora inapigwa chini kwenye uchaguzi mkuu! hii inaitwa SOCIAL CONTRACT THEORY, pale Mlimani wanafundisha vizuri sana.

Hata raia unapokosa kazi si kwa uzembe unatakiwa kulipwa unemployment benefit na Tanzania imesaini mkataba huo wa kuondoa njaa na magonjwa na tatizo la ajira kwa raia wake na kukubali jukumu la kuwasaidia raia wake wote wenye shida na njaa na magonjwa, mwaka 2002 huko Geneva, hiyo inaitwa SOCIAL PROTECTION FLOORS na wananchi hawana habari hiyo, hawajaambiwa na serikali yao hadi leo kuhusu huo mkataba uliosainiwa na serikali yao kuwapa hali bora na kuwanasua na umaskini wa kutupa!

System ya uendeshaji wa nchi ya Tanzania sasa imeoza, nchi inanuka kwa ufisadi , kuonea raia, rushwa na umaskini uliokithiri, umaskini unaowatesa watu wake millioni 47 wanaokufa kwa njaa na magonjwa , raia wasio na elimu wala ajira huku majoka machache yenye makengeza kina
Chenge , Anna Tibaijuka , Werema ( na wengineo wote wanajijua na Mungu anawangoja wafe awachome moto mkali) , wakijilimbikizia mabilioni ya mali ya umma kwenye akaunti zao na kuleta shida kubwa sana kwa raia wa kawaida ya kupata pesa manake haya majoka yenye makengeza na sumu kali yamezitoa pesa kwenye mzunguko wake!

Pesa ambazo zingepita mahospitalini, kwa mama ntilie, deiwaka, mashuleni, madukani, serikali za mitaa, wizarani nk na kila raia angeambulia japo kidogo ila mashetani na watemi kina Chenge wamezikwapua zote bila huruma!jamani mtu ana familia ya watoto watatu wazee kama yeye na mke wake mzee anakwapua millioni elfu nne na mia sita (1.6B) zote anapeleka wapi kama si ulafi na ushetani tu? haya majambazi ni ya kupiga risasi hadharani tu kama China! majitu yanakwapua mabilioni yasiyoyahitaji katika maisha yao ya kila siku, na cha ajabu sana mabilioni yasiyoyatumia!

Ikumbukwe kuwa umaskini wa Tanzania ni wa kujitakia na unasababishwa na mashetani wachache wenye maumbo ya binadamu, mashetani wenye nyadhifa mbali mbali serikali kuu na serikali za mitaa!. ni ajabu sana wadanganyika wana macho na hawaoni jinsi nchi yao inavyoliwa na mafisadi , waziri anakuja kwenye mkutano wa kampeni na TOYOTA LANDCRUISER GX six cylinder iliyotokana na kodi ambazo ni majasho ya walalahoi manake matajiri wanasamehewa kodi bongo, gari inakunywa mafuta kwa siku moja ni bajeti ya mlalahoi kwa mwaka na wanawatimulia vumbi raia waliokaa juani eti kuwasikiliza huku wakisikia njaa kali na kiu kwa kukosa chakula na maji safi na nguo waliovaa zina viraka na chini wamevaa tairi za gari na wengine wana sugu kwa kuhangaika na jembe la mkono miaka nenda miaka rudi hadi alama za dole gumba zinazowatambulisha nazo zimefutika ila bado masikini hawa wanachagua hawa matajiri kuwaongoza, kwa kutumia akili ndogo tu, hivi watu wasiojua njaa inavyouma watakusaidiaje wewe kapuku pangu pakavu?

Hivi raia wengi hawajui kuwa umaskini wa bongo ni wa kutengenezwa ili watu wawe bize kuhangaikia maisha wenzao wabaki masaki kula bata hata foleni ya Dar ni ya kutengeneza ili raia wasi discuss mambo ya maendeleo manake muda wote watu wa Dar wako bize wana discuss foleni na kuwaza foleni na kuota wako kwenye foleni!, eti mtu anaamka saa kumi kukwepa foleni isimkute eti atachelewa kibaruani na hawa miungu watu viongozi wetu wakiwa na safari zao mjini hawana tabu, piki piki ya usalama inapita na ving'ora kuyaamuru magari yakae pembeni wenye nchi yao , miungu watu wapite , si watumie helikopters manake pesa ya nchi iko mikononi mwao badala ya kuwaletea adha wananchi walio kwenye madala dala wamebanana joto na majasho yakiwatiririka kusubiri msafara upite! hivi unadhani hao wanaopita na misafara yao wasiojua adha ya foleni wataondoaje foleni?! jamani amkeni miaka hamsini ya umaskini haitoshi tu!

Wakati huo huo Tanzania ni nchi iliyojaa udikteta uliojificha katika kichaka cha demokrasia iliyoishia kwenye makaratasi manake walalahoi wanaojaribu ku exercise demokrasia wanatekwa na kuteswa, na huku vyombo vyenye jukumu la kulinda usalama navyo vinawapiga watu ovyo, vinaua na kuleta vilema kwa raia wasio na hatia , watu wanaoandamana kudai haki zao za kikatiba! bongo ni nchi ya ajabu sana! viongozi na matajiri wako juu ya sheria , akili zangu zinaniambia wafungwa wengi Tanzania wanafungwa kwa kuonewa tu , kwa kuwa kina Chenge wameiba pesa zote za umma na wananchi wanakosa elimu na huduma za afya na matokeo yake hawana ajira wanaishia kukaba na kuiba na kukamatwa na kufungwa manake wanasikia njaa na hawana namna ya kupata chakula na nguo kihalali kama Panya Road, ikumbukwe sitetei uhalifu kamwe!

Magereza zimejaa masikini tu! nawapa pole sana,
hata sisi tunaopiga cargo na deiwaka ughaibuni nawaambia ukweli wangu ni effects za kina Chenge pia , manake tumesota sana bongo miaka nenda rudi, tukaanza kuzeekea kwenye umaskini, tumelala na njaa na kukosa matibabu na nguo, tulipopata upenyo bila kuwaza mara mbili mbili tukakimbilia nje!!na wengi wetu hatupendi kabisa kurudi bongo kuona tena nyuso mbaya kabisa za kina Chenge!

Jamani Chenge ni mfano mbaya sana kuwahi kutokea katika historia ya jamii ya Tanzania, ni mfano mbaya sana kwa watoto wa Tanzania. Huyu nyoka mwenye makengeza na sumu kali anafaa kufundishwa shuleni kama mfano wa raia wahujumu uchumi na vyanzo vya umaskini na uhalifu Tanzania. Chenge ni nyoka mwenye makengeza na sumu kali inayoua raia wa Tanzania , nyoka mbabe alie mstari wa mbele kupeperusha bendera ya ufisadi huku wenzake wakimfuata kwa shangwe nyuma yake. Ndio, yeye na wenzake wote katika chama wanapigana vikumbo kufilisi mali ya wavuja jasho, walalahoi wanaokamuliwa kodi huku matajiri wakipewa misamaha ya kodi.

Chenge na genge lake la majoka yenye makengeza na sumu kali yalio madarakani na yale yaliostaafu tangu uhuru yanaishi kifahari masaki kwa kutumia mali ya umma ambayo ni majasho ya walalahoi wa Tanzania, nani anabisha? Chenge ameonesha wazi stage tuliyofika katika nchi ambapo sasa watawala wetu wako juu ya sheria! mtu ni mwizi wa dhahiri na anagoma kuhojiwa na hafanywi kitu , japo tukumbuke most of viongozi wa Tanzania ni mafisadi na kama huamini taja jina moja lolote na waambie TAKUKURU NA CAG wamkague na utayopata iwe siri yako!

Maskini nchi tajiri ya Tanzania iliyojaa rasilimali lukuki imepata bahati mbaya sana kuwa na viongozi mashetani, wezi, walafi, wabinafsi , wasiomjua mungu na madhalimu wakubwa wasiojali mateso wanayopata raia wake. Wananchi shime shime tupigie kura upinzani kwenye uchaguzi mkuu kuyaondoa madarakani majoka haya yenye makengeza na sumu kali inayotuua! gamba mmoja tu akisoma hii comment , i will be extremely happy! . Tanzania bila magamba inawezekana , tumeanza kuona uchaguzi serikali za mitaa!
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ninakuomba tuondolee mafisadi katika uongozi wa nchi ya Tanzania, Amen
 
Duh!Chenge ndie mwenyekiti wa kamati ya maadili ya maccm?
 
CCM ni sawa na ukoo wa panya: baba mwizi, 'mama mwizi, babu mwizi, bibi mwizi, motto mwizi, kaka mwizi, dada mwizi, mjomba mwizi, shangazi mwizi, mkwe mwizi' BY Mh. Nassari
 
Kwa tabia aliyoonyesha nyoka mwenye makengeza ni DHARAU kubwa kwa CHAMA chake na wapiga KURA wake. Kweli pesa ndiyo kila kitu Tanzania. Ile dharau watu wengi waliona kupitia vituo vya luninga na watu wanajiuliza hivi ndiyo wakubwa wa nchi hii wanavyodharau vyombo vya kisheria.
 
kijapo kiburi ndipo lijapo anguko,kiburi cha ccm na viongozi wake hata wakashindwa kuwasikiliza wananchi ndio anguko lao
 
Hakuna mwenye uwezo wa kumwajibisha chenge serikalini wala kwenye chama kamwe! Katiba pendekezwa imetungwa na kuandikwa na fisadi chenge, ndiyo katiba ambayo jk anasema ni katiba bora afrika. Ndani ya ccm wote wameoza, kilichobaki ni kugawana vyeo kama njugu tu. Period!
 
hua najiulza kiburi hiki chenge anakitoa wapi? na huko ccm akuna mtu wa kumkanya? yaan jamaa anafanya anachojickia na hakuna wa kumhoji " kwel ccm ina wenyewe
 
Tufanye utafiti.
Kwa nini anaogopwa na mamlaka za nchi yetu?
Tatizo mnasukumwa na hisia kuliko ukweli na sheria. Je umeshajiuliza ikiwa kweli ni mchafu kiasi hicho mbona hajafukuzwa katika Chama na pia hajafikishwa mahakamani?
 
Tatizo mnasukumwa na hisia kuliko ukweli na sheria. Je umeshajiuliza ikiwa kweli ni mchafu kiasi hicho mbona hajafukuzwa katika Chama na pia hajafikishwa mahakamani?
Hebu tuanze na sakata la rada (BAE) ambapo vyombo vya uchunguzi vya Uingereza vimemhusisha na rushwa aliyopokea na kuificha kwenye offshore account....
Naomba unitoe tongotongo kuhusu usafi wake hapo ili tusonge mbele na tuhuma zingine
 
A powerful gang is backing him up cuz if he goes down,the whole gang goes down.Y'all know who am talking about.
 
Hebu tuanze na sakata la rada (BAE) ambapo vyombo vya uchunguzi vya Uingereza vimemhusisha na rushwa aliyopokea na kuificha kwenye offshore account....
Naomba unitoe tongotongo kuhusu usafi wake hapo ili tusonge mbele na tuhuma zingine
Yote yaliandikwa, lakini kiukweli ni kuwa yalibaki hisia tu. Kungekuwa na uthibitisho wa kumhusisha yeye na sakata hilo kijinai angepelekwa mahakamani. Kuwa na Account nje na pesa hizo siyo kosa kwa mujibu wa sheria zetu mpaka sasa ikiwa tu unaweza kuelezea zimepatikanaje. Nina hakika Mh alieleza kwa ufasaha alizipataje na zikaonekana ni za halali ndiyo maana hakupelekwa kwa Pilato.
 
Aisee, inaelekea jamaa anaona mbali sana na is an advanced and professional corrupt!
Umeshahau
Na ni chenge aliyetunga katiba iliyoondoa maadili kama tunu ya taifa
Katiba hiyo inaitwa "Katiba bora" na MaCCM
Sasa hebu fikiri zaidi hapo
Katika msahafu wa Wakristo imetajwa kwamba Mungu ni baba yetu, na pia shetani ni baba wa waovu. Sisi watanzania tulimchagua mioyoni mwetu kuwa Nyerere awe Baba wa Taifa, hivyo napendekeza sasa Chenge aitwe baba wa UFISADI nchini.
 
Chenge hana jeuri yoyote bali anacheza na mfumo wa serikali dhaifu. Bila shaka anajua kwa uhakika waliiba ama kupokea fedha hizo na nani serikalini. Hata hivyo upo msemo kwamba wezi huwa mara nyingi ni jasiri.
 
Duh!Chenge ndie mwenyekiti wa kamati ya maadili ya maccm?

What? Basi kama hivyo ndivyo maadili yalishazikwa siku nyingi. Ona jinsi walivyochakachua katiba kwa kuwa tu alikuwa katibunwa hotuba.
 
Yote yaliandikwa, lakini kiukweli ni kuwa yalibaki hisia tu. Kungekuwa na uthibitisho wa kumhusisha yeye na sakata hilo kijinai angepelekwa mahakamani. Kuwa na Account nje na pesa hizo siyo kosa kwa mujibu wa sheria zetu mpaka sasa ikiwa tu unaweza kuelezea zimepatikanaje. Nina hakika Mh alieleza kwa ufasaha alizipataje na zikaonekana ni za halali ndiyo maana hakupelekwa kwa Pilato.

Bila shaka wewe ni mtoto wake au ni mtu ambaye unafaidi ufisadi wake.
 
Tanzania six not pour country but due to the miss use of power lead to the people live in pour situation
 
Back
Top Bottom