GadoTz
JF-Expert Member
- Nov 20, 2014
- 350
- 569
Wote tunaikumbuka nguvu ya Lowassa ndani ya CCM ilianza kama masihara matokeo yake Lowassa akakuwa mpaka akafikia hatua akawa kama untouchable licha ya kuwa na kashfa za ufisadi lakini nguvu yake ilikuwa kubwa kiasi cha kukitikisa chama.
Naiona hiyo nguvu pia anaanza kuwa nayo Mtemi Chenge akiwa mwenyekiti wa bunge amekuwa na sauti kuliko ata spika na naibu wake kiasi cha kufukuza mpaka mbunge kikaoni.
Wasiwasi wangu ni kuwa CCM haswa wabunge wake wanatutengenezea Lowassa mpya maana ni wazi Chenge kapata uenyekiti wa bunge baada ya kuchaguliwa na wabunge haswa wa CCM. Sielewi haswa mapenzi ya wabunge wa ccm kwa Chenge yalitoka wapi au labda ni nguvu ya vijisenti ila kwa kweli katika vitu vinavysikitisha ni hili la Chenge kuwa mwenyekiti wa bunge na kuwa anafanya maamuzi haswa yanayousiaana na rushwa ikiwa yeye alikamatwa 'ready handed' na SFO kwenye ishu ya rada.
Nashauri Magufuli awe makini sana na huyu mtu anakuwa taratibu na anapata moral authority ya kushughulikia wanaotoa tuhuma za rushwa. Najua Magufuli awezi kupingana na maamuzi ya wabunge wake ila muda sio mrefu anakabidhiwa rungu la uenyekiti wa chama awa ndio majipu ya chama.
La sivyo ufisadi utakuwa ni wimbo wa kisiasa tu kama wapinzani walivyompa mtuhumiwa wa ufisadi kugombea urais na ccm mnampa mtuhumiwa wa ufisadi kuliongoza Bunge.