Chenge apiga billion 1 - fedha za escrow

Mbowe yumo na kamdhibiti mnyika ambaye ni waziri kivuli nishati na madini kanyamaza kimyaaaaaa
 
Muulize david Kafulila anajua wezi.....na uzushi wake....
 
Kwenye hiyo orodha Mbowe yumo.

Hivi Mbowe ni waziri wa nini vile? Na maamuzi yake kiutawala yana wezaje kuyumbisha serikali pengine dawa mahospitalini au vitabu mashuleni vikakosekana kwa sababu ya maamuzi yake baada ya kupewa mgawo? Tusaidieni tuelewe.
huenda mbowe amenyamazishwa ili asirapu pale bungeni. huwezi kumtenganisha mchaga na hela ndo maana wezi.
watu makini kama akina Zitto, Kafulila (sisimizi-slaa/tumbili-werema) peter serukamba wamelishikia bango kwa masilahi mapana ya umma.
 
huenda mbowe amenyamazishwa ili asirapu pale bungeni. huwezi kumtenganisha mchaga na hela ndo maana wezi.
watu makini kama akina Zitto, Kafulila (sisimizi-slaa/tumbili-werema) peter serukamba wamelishikia bango kwa masilahi mapana ya umma.

Kumbe mpango mzima hapa ni "HUENDA AMENYAMAZISHWA"? Basi mie sina neno zaidi.
 
Haya tena mwanahabari saidi Kubenea...Mtungaji uongo mkuu sasa anamchokonoa Mzee Chenge....baada ya kuona hakuna mahali anapoweza kumsingizia ameona amzushie kuwa kahojiwa na kadai fedha za ushauri....Mbona mna haraka jinsi hiyo????? subirini keshokutwa sio mbali tutawajua woooote waliopokea mgawo na walioomba wakanyimwa....
 
Hii issue imewashika pabaya CCM. I hope watu wa vijijini wanaweza kuelewa kinachoendelea Dodoma.
 

Hii ndio ishara namba moja kuwa 'KATIBA PENDEKEZWA' iliyoandikwa na huyu mwizi ni 100% disqualified, pamoja na vigezo vingine lukuki...kwa kuwa mwizi hawezi kujenga jela ya kujifunga mwenyewe! Wametengeneza 'kitabu cha CCM' wanachokiita Katiba Pendekezwa ili kujificha na kumaliza uhai wa umma kwa wizi wao mkuu...manyang'au wa-head!

Kunatakiwa kuwe na kipengele cha kuvuliwa nguo hadharani kwa wezi kama Chenge na wezi wengine, wachapwe viboko matakoni 'hamso' na mwisho wapitie mkondo wa 'kamba shingoni' ili kukomesha wizi huu wa udhalilishaji wa uhai wa umma...kwa sababu hakuna utawala Tanzania, bali genge tu la walafi!!
 
Huyo ndo mwenyekiti wa kamati ya aadili ya chama. hahaaaaasa
 
Tangu akiwa mwanasheria mkuu wa serikali amekumbwa na kashfa nyingi na wizi wa fedha za umma. Amehusishwa na fedha za EPA, Meremeta, Rada, Ndege ya Rais ametajwa na sasa ESCROW nayo katajwa kupata mgawo.
Ajabu ni kuwa ndani ya CCM anaaminika sana kiasi cha kupewa cheo " kikubwa" cha Mwenyekiti wa kamati ya maadili. Pia Bungeni ilipoanzishwa Kamati ya Budget ambayo ni muhimu sana ikafanywa juu chini akapewa uenyekiti yeye. Hapo hatujasahau latika BMK alivyopewa Uenyekiti wa Kamati ya uandishi. Sasa pamoja na kufahamika kwa sifa mbaya aliyonayo ( ukiacha ile ya kumwaga unga unga usiku Bungeni aka ulozi) inakuwaje kila itokeapo nafasi mpya CCM lazima wampe? Tena wanampa huku wakimtukuza kumwita Mtemi?
Au hivyo vyeo anavitaka yeye na hivyo anatumia mafedha aliyokwapua kupata uungwaji mkono?
 
Chenge ni ishara ya upumbavu wa sisi watanzania... tusisahau kwamba mzee chenge pia "anahusishwa" na kifo cha yule binti aliyekua anafanya kazi mwanza hotel, alimgonga oysterbay

Kwa maovu aliyohusishwa nayo, endapo Chenge angekua chama cha upinzani, angekua anaishi jela au hata wameshamnyonga
 
Wahuni hawa hawajali chochote kile, wanajua watakwiba watakavyo na hakuna kibaya kitawachowatokea kuhusiana na adhabu kali dhidi ya wizi wao. Huyu Chenge alikuwa afukuzwe pamoja na akina Lowassa, Rostam na wengineo kama wachafuzi wa chama katika kile kilichoitwa "kulivua gamba" lakini baada ya kumtisha DHAIFU Janga Kubwa kwamba kama watafukuzwa chamani basi "Ikulu hakutalalika" basi DHAIFU akagwaya na hakuna aliyefukuzwa. Matokeo yake wizi wa mabilioni unaendelea mwaka hadi mwaka.
 

ngoja nikwambie kwanini hawawezi kumtenga chenge
chenge aliwahi kuwa mwanasheria mkuu wa serikali kwa miaka 10 wakati wa utawala wa mkapa, mkataba hauwezi kusainiwa bila ofisi yake kuipitia na kuikubali. kwahiyo kama unakumbuka vizuri mikataba mingi michafu ilipita mikononi mwake na wausika walikuwa wanapitishiwa mikataba yao michafu kupitia kwake wakiwemo mawaziri wote akiwemo mkulu aliyepo ikulu hivi sasa kwahiyo siri zote zinazousiana na uchafu wa mikataba yote anaifahamu na wezi waliousika nayo ndio maana kipindi kile amekamatwa na acount kule London akatoa ile kauli ya vijisenti akilinganisha na wezi wengine wanaoitafuna nchi hii. siku ya ukombozi wa pili wa nchi ukitokea tukiungana na ndugu zetu wa Burkina Faso waliotuonyesha njia mtu prime muhimu kuliko wote ni chenge ndio anaweza kutupatia siri zote chafu kuhusu mikataba badala ya kumfunga miaka 30 jela angalau mkampunguzia mpk 10 endapo atatapika kila kitu.
 
Mkuu usishangae ccm sifa ya kwanza kupewa cheo Ni lazima uwe mwizi mzoefu. Huyu chenge amewazidi wenzake kwa uwizi kwa hiyo Ana sifa ndio maana wanampa vyeo. Nisaidieni kushangaa nchi hii jamani.
 

Dah!Umenifungua macho mkuu!!Huo ndio ukweli.Je ndani ya Ccm hakuna wazalendo wakalimulika ili na kulisemea kwa manufaa ya nchi?
 
CCm ni ukoo wa panya; baba mwizi, mama mwizi, mtoto mwizi, kaka mwizi, dada mwizi, mjomba mwizi,shangazi mwizi, babu mwizi, bibi mwizi.By Mh.Nassari.
 
Uchawi wa Chenge umewapumbaza wana ccm wote kiasi kwamba hata kuwaweka ndani kinyumba anaweza
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…