Chenge apiga billion 1 - fedha za escrow

Kudakwashe

Member
Joined
Nov 23, 2014
Posts
53
Reaction score
25
Duru za uchunguzi zinaeleza kwamba Chenge amehojiwa na Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa ( Takukuru ) na kuthibitisha alilipwa kiasi hicho cha fedha kutoka kwenye fedha za ESCROW kiasi cha Tsh 300 bilion.

Chenge alipoulizwa kiasi hicho kilikua cha nini alipata wakati mgumu kujibu , lakini mwisho alijibu ni ada ya ushauri.

'' Imethibitika pasishaka kwamba Chenge amepewa kiasi cha Sh 1.6bilion.Ameithibitishia Takukuru alipohojiwa , " zilisema duru za habari za kuaminika kutoka ofisi ya Bunge.

Chanzo kiliongeza : "Awali alipoulizwa ni za nini hakuweza kutoa jibu la haraka sana , lakini mwisho akasema ni za ushauri ".

Uchunguzi zaidi umebaini kuwapo kwa wanufaika wengine wa fedha hizo lakini ( majina yao yamehifadhiwa baada ya kukosekana kujitetea kama maadili ya taaluma yanavyoeleza ).Hata hivyo , juhudi za kuwatafuta zinaendelea na wataanikwa.

Lakini tayari pia Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Anna Tibaijuka amekiri kupokea kiasi cha Sh 1 bilioni kutoka kwa mtuhumiwa wa wizi wa ESCROW.

MAJIBU YA CHENGE.
Alipoulizwa Chenge kuhusiana na tuhuma hizo alijibu kama ifuatavyo :

MWANDISHI : Mheshimiwa shikamoo pole kwa majukumu yote , samahani mimi mwandishi habari gazeti la MWANAHABARI kuna taarifa ambazo zikielekeza kuhusika kwako na kashfa ya Escrow , unazungumziaje.

CHENGE : Na mimi nimeona na kusikia kwenye mitandao ya kijamii yakiwemo Magazeti kunihusisha na suala hilo lakini mimi siwezi kusema chochote.

MWANDISHI : Kwanini usitoe ufafanuzi zaidi ili ukweli ujulikane kama unahusika au uhusiki kuliko kukataa kuzungumza ?

CHENGE : Mimi sitaki kabisa kuzungumzia suala hilo.

MWANDISHI : Au unakataa kuzungumza suala hili kwa sababu unaongea na mimi kwenye simu ungependa tuonane ana kwa ana. ?

CHENGE : Hapana hata ukija tukionana sitakua tayari kuzungumza chochote.

MWANDISHI : Mheshimiwa lakini kwa ujumla unalionaje suala la Escrow.

CHENGE : Sijui lolote.

MWANDISHI :Kweli hujui suala la Escrow Account ?

CHENGE : Kukata simu bila kujibu swali wala kuagana.

Chanzo: Mwanahabari :
 
Bilioni 1.6? hiyo nayo hela! hivyo ni vijisenti vya kununulia nyanya tu sokoni Tandika.
 
huyu kiongozi wa timu ya wakwapuaji wakubwa wa rasmali za umma.
 
Na huyu mwandishi naye sijui kanjanja. Mtu una habari kwamba amepokea 1.6 bn kwa nini usimtupie hilo swali kwamba inasemekana umepokea kiasi cha Shs. 1.6 za ESCROW kutokana na ushauri ili Chenge ahangaike nalo. Sasa anazunguka mbuyu wa nini hapo. Ametukosesha fursa murua.

Anataka wakutane halafu katika kumuhoji amuulize " sasa mheshimiwa tuandikeje haya mahojiano kwenye gazeti la kesho?" akitegemea aambiwe andika vyovyote huku akipewa bahasha ya kaki
 
ESCROW imekuwa ikipigiwa kelele nyingi sana, mpaka sasa majina yaliyovuja ni yale ya James Rugemalelila kwenye account ya Mkombozi bank. Ruge alipata 30% ya fedha zote na majina yaliyopo mkombozi jumla ya mgawo haufiki 6B. Je Wengine ni akina nani na Je Seth mwenye mkwanja mkubwa aligawia kina nani?

Ili kuwa analytical na fast kuliko makinda na ndugai ni veyma JF ikaweka majina yote hapa kwa yule mwenye data za ukweli kama ilivyokuwa JF ya ukweli. Tulikuwa tunakuwa wa kwanza kabla yeyote enzi za kanzi.
 
Mkuu Mkwawa hii ngoma imeanzia utosini
 
Majina ishaelezwa kwamba yapo JF yamehifadhiwa kwenye BLACK BOX ,ila kinachosubiriwa kama unavyojua tunaweza kusema hii kesi ipo katika mahakama za kibunge ,sasa huko wakilikoroga ndio uhakika unawekwa hapa ,yaani likitumbuka tu huko bungeni hapa tunakamua ili kuhakikisha jipu halioti tena ,mpaka moyo wa jipu utoke.

WaTz tunaugua na jipu hili muda mrefu sasa ila inaonekana limeshaivah.
 
Back
Top Bottom