Chenge amruka shahidi aliyemkaanga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chenge amruka shahidi aliyemkaanga

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Zak Malang, Oct 6, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Oct 6, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Chenge amruka shahidi aliyemkaanga

  Na Ummy Muya

  MWANASHERIA mkuu wa zamani, Andrew Chenge jana katika utetezi wake alimkana shahidi wa tatu wa upande wa mashitaka, Fortunatus Musilimu akidai kuwa hamfahamu na kwamba huenda ana una ugomvi naye.

  Musilimu, ambaye pia ni Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (ASP), alidai wakati akitoa ushahidi Juni 7 mwaka huu kuwa Chenge aliwasilisha hati batili ya bima na kwamba gari lake aina ya Toyota Hilux lenye namba za usajili T512ACE lilikutwa na mabaki ya ubongo wa watu waliofariki katika ajali iliyosababishwa na waziri huyo wa zamani wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

  Musilimu alidai siku hiyo kuwa alimhoji Chenge kuhusu tukio hilo na kwamba mbunge huyo wa Bariadi, alikiri kuendesha gari hilo.
  Musilimu alidai kuwa Chenge aliwasilisha hati mbalimbali za gari zikiwemo za bima na kwamba baada ya kufuatilia zilionekana kuwa batili, kwani muda wake wa matumizi ulikuwa umekwisha.

  Lakini, katika siku ya kwanza ya utetezi wake kwenye kesi hiyo ya makosa mawili ya kusababisha vifo na la tatu la kuendesha gari lisilo na bima, Chenge alidai kuwa hamfahamu shahidi huyo na kwamba huenda ana ugomvi naye.

  “Nilimuona hapa hapa akinifanyia vituko; huenda ana 'beef' na mimi... nasisitiza sikuendesha kwa uzembe na sikusababisha vifo,” alisema Chenge na kusababisha watu walipuke kicheko.

  Shahidi wa tatu katika shauri hilo ni mkuu wa Kitengo cha Usalama Barabarani wa Kinondoni, Fortonatus Musilimu ambaye aliandika maelezo ya Chenge baada ya tukio hilo lililosababisha vifo vya wasichana wawili Victoria George na Beatrice Costantine.

  Akiongozwa na Wakili Simon Mponda, ambaye anamtetea, Chenge alidai kuwa hamfahamu shahidi wa tatu katika shauri hilo na kwamba alimuona mahakamani hapo akimfanya vituko.

  Chenge alitoa kauli hiyo dhidi ya kamanda Musilimu ilikuja baada ya kudai kwamba hakuwa katika mwendo kasi bali alikuwa katika mwendo wa kawaida huku katika maelezo yake aliyoyatoa kituo cha polisi cha Oysterbay na kuandikwa na Musilimu yalionyesha kwamba mshtakiwa alikuwa katika mwendo wa kati ya kilomita 70 hadi 100 badala ya 30 hadi 50 kutokana na eneo hilo kuwa na makazi ya watu.

  “Mimi ni mkazi wa Oysterbay kwa zaidi ya miaka 20, lakini sijawahi kuona kibao kinachopima mwendokasi na wala hakuna mataa katika barabara ya Haille Salaise isipokuwa kuna alama ambazo wanafunzi huzitumia wakati wa kuvuka barabara hiyo,” alisema Chenge.

  Alipoulizwa kuhusu kuendesha gari lisilokuwa na bima, Chenge alikanusha kuendesha gari ambalo bima yake ilianzia Januari 8 mwaka jana na kuishia Januari 7 mwaka huu.

  Akitoa maelezo kuhusu mkanganyiko wa namba ya gari hilo yaani T512 ACE na T512 AEC, Chenge alidai kuwa huenda tatizo hilo lilitokana na uandishi gari yake ina namba T512 ACE na sio T512 AEC.

  Wakili wa upande wa mashtaka hakupata nafasi ya kumhoji Chenge baada ya hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Kwey Rusema kupata udhuru na hivyo kuliahirisha hadi Oktoba 20.


  Chanzo: Mwananchi
   
 2. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #2
  Oct 6, 2010
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Sidhani kama utetezi huo utamsaidia sana Chenge kwani nina imani alitia sahihi yake kwenye maelezo yaliyochukuliwa na huyo Afande, sasa atasemaje hamjui na wala hajawahi kumuona!! Kichekesho

  Tiba
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Oct 6, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kama mimi ni hakimu ningelisweka jizi hili jela miezi 6 tu kwa kosa la kughushi hati -- bila faini. Akale dona huku akihangaika na rufaa yake. mafisadi wengi sana wataogopa kwani hakimu huyu atakuwa shujaa in just a short time na kurekebisha mwenendo wa nchi. Please...hakimu... Tanzanians are looking at you.
   
 4. SILENT WHISPER

  SILENT WHISPER JF-Expert Member

  #4
  Oct 6, 2010
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 2,231
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  chenge hawezi kufungwa...! magereza ya nchi hii ni kwa ajiri yetu sisi walalahoi..! FISADI kama chenge hawezi kwenda jela..!

  kuna siku nilisema kama tuwaua vibaka wa simu na kuku......! why not these pipo like chenge and other FISADIZ.....?

  WE THE PIPO AGAINST ALL THE FISADIZ.....! trust me we will win..!


  kama unategemea kikwete kuwa funga hawa jamaa ...U CAN JUST FORGET IT...READY MY LIPS..!
   
 5. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #5
  Oct 6, 2010
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Chenge asilete usanii hapa wakala wa bima wameika na stika yake.
   
Loading...