chemsha akili kidogo...!! then unipe jibu. nguo inauzwa 10000/= huna pesa ukaenda kukopa kwa dada 5000/= na kaka 5000/= jumla 10000/= ukaenda dukani ukaomba upunguziwe ukauziwa 9700/= ukabakiwa na 300 ukapunguza deni kaka yako ukampa 100 dada ukampa 100 ukabaki na 100 jumla kaka akawa anakudai 4900 na dada 4900 ukijumlisha unapata 9800/= ukiongeza na 100 yako uliyobakinayo unapata 9900/=je? 100 iko wapi? nisaidie jibu,
ukipatia nakutumia vocha yako.
Kama aliuziwa simu kwa shilingi 9,700. Ina mana angehitaji kukopa shilingi 4850 kutoka kwa grol na 4850 kutoka kwa amos i.e (9,700/2 = 4850). Na kama yeye aliwapa shilingi mia kila mmoja ina maana so far ametumia 4,850 x2 +100x2=9,900. ukijumlisha na mia alobakiwa nayo yeye jibu ni buku kumi kamili.
Kwa mbaali nimekuelewa
Ishu ni kuangalia contribution ya glor na amos kwenye actual cost aliyonunulia simu ambayo ni 4,850.
Bila shaka mmeamka salama wana jukwaa.
Nimeona si mbaya nikileta swali hili tukachemsha akili kidogo.
Juma alienda dukani kununua simu akaambiwa bei ni sh. 10,000. Bahati mbaya hakuwa nayo hiyo 10,000 ikabidi atoke nje akaazime 5,000 kutoka kwa Grol na 5,000 nyingine kutoka kwa Amos.
Baada ya kupata hiyo 10,000 Juma alirudi dukani kununua ile simu lakini akawa amepunguziwa sh. 300. Hivyo aliinunua kwa sh. 9700.
Sasa kwenye ile 300 ikabidi atoe 100 apunguze deni kwa grol na 100 nyingine kwa Amos. Hivyo alibaki na sh. 100 mkononi huku akiwa na jumla ya deni la sh. 9800.
Lakin sasa Juma akichukua ile 100 aliyobaki nayo akajumlisha kwenye lile deni lililobaki ambalo ni 9800 anapata jumla ya 9900.
Sasa naomba mniambie ile 100 ilipotelea wapi, maana nimeambiwa nikipata jibu napewa 25,000 asubuhi hii.
huwez kujumlisha pesa uliyobaki nayo katka jumla ya maden yako.hiyo mia moja uliyobak nayo ijumlishe katika kias ulichotumia wewe kununua simu ambapo utapata amount unayodaiwa.hakuna pesa imepotea.