Niseme tuu kuwa matokeo ya mchezo wa jana yalinihuzunisha sana. Miungu ya mpira ilishindwa kumzawadia PSG kombe pamoja na kwamba mchoni pa wengi ndio ilikuwa timu bora. Mpira ni magoli, Chelsea walifunga magoli na hivyo walistahili kushindi mchezo wa jana.
Lakini inakuwaje timu ambayo kwa takribani miezi sita imetuburudisha kwa kucheza kandanda safi, kuonekana imekamilika katika kila idara kushindwa kuleta ushindani uliotegemewa kwenye mchezo mkubwa kama jana? Wachezaji waliosifiwa kwa umahiri wao wa “gusa achia twende kwao”, ukali wa ukabaji wao na ukatili wa umaliziaji wa nafasi walizokuwa wakitengeneza , jana walishindwa kutatua changamoto ambazo wapinzani wao Chelsea waliwapa.
Nini hasa kilisababisha anguko la PSG jana (kwa yale tulioyaona uwanjani)? Ni rahisi kusema kibong bongo kuwa “mpira una dunda” au ah Chelsea wachawi. Tujaribu kuchambua wapi PSG walikosea na wapi Chelsea walipatia.
Chelsea walikuwa jasiri:
Katika mchezo wa mpira, nafasi ndio kila kitu; tengeneza, dumisha na itumie kumshambulia mpinzani (create maintain and exploit). Jambo la pili ni kwamba, jaribio lolote lile la mpinzani katika kujaribu kupokonya mpira, litaacha nafasi katika sehemu zingine za uwanja. (any pressing attempt by the opposition will create space somewhere on the field). Hivyo basi wewe uliyekuwa na mpira ni kujua nafasi ipi inachwa wazi na ni kwa namna gani nitaweza kuitumia hiyo nafasi kumshambilia mpinzani wangu.
Moja ya ubora wa PSG ni Ule uwezo wa kwenda kuanza kutaka kumpokonya mpira mpinzania akiwa kwenye nusu yake. Dembele alisifiwa sana katika kuongoza wenzie kwenye hili jambo. Hivyo basi, Chelsea walilitarajia hili na baadala ya kuogopa, wao wakalitumia kama fursa ya kumshambilia PSG. Nafasi kuu mbili ambazo pressing ya PSG iliacha wazi ni:
Goli la tatu Palmer alipokea mpira kwenye kwenye nafasi katikati ya mtari wa mabeki na viungo na kuweza kusafiri nao na kutoa pasi ya goli.
Kabla ya magoli haya kufungwa, tayari kulikwa na viashiria na majaribia kadhaa kushambilia hizo nafasi ambazo Chelsea hawakuzitumia vizuri ila PSG walishindwa kuzifanyia kazi.
Goli la pili ni la transition, PSG walipoteza mpira Chelsea walifanikiwa kumpa mpira Palmer ambaye alikuwa amekimbilia kwenye nafasi ambayo Mendez aliacha wazi wakati wakiwa wanapanga mashambulizi yao kabla ya kupoteza mpira. Takwimu za FIFA za kiufundi zinaonesya kwa timu zimeboresha ufanisi wa mashambulizi ya kustukiza ukilinganisha na kombe la dunia liliofanyika Qatar. Ukipoteza mpira kizembe utadhibiwa.
Kwa ufupi, Celsea walijua ni nafasi zipi mpizania wao anaacha wazi akiwa anafanya pressing lakini pia nafasi zipi anaziacha wazi akiwa anajenga mashambulizi yake. Lakini kujua tuu haitoshi, inabidi utelekeze mashambilizi kwa ufanisi wa hali ya juu kitu ambacho Chelsea walifanikiwa.
PSG mdebwedo…..
Kwa upande wa PSG, mambo kadhaa yawaliwaangusha.
Pongezi ziende kwa Chelsea kwa kuwa jasiri na kujua namna gani ya kukabiliana na mpizani, hususani, kubadilisha ubora wa mpizani kuwa udhaifu. Kushindwa kwake Luis Enrique kungamua mbinu za wapinzani wake wakati game inaendelea au kushindwa kutafuta suluhisho kumemgharimu. Haimaanishi kuwa yeye ni kocha mbaya, lah hasha, bali inadhihirisha kuwa wote sisi ni binadamu na katika kusaka ukamilifu basi kunamatukio yanatukumbusha kuwa hilo ni jambo lisilowezekana.
Chelsea wameonyesha ni namna gani ya kumfuga PSG, je timu zingine zitafuata mbinu alizotumia Enzo Maresca na vipi kuhusu Enrique? Atakuja na mbinu mpya ya kuficha madhaifu yaliojitokeza jana. Tusubiri ligi zitakapo anza.

- Nafasi kati ya mstari wa mabeki na Donnaruma. Mstari wa mabeki wa PSG ilikuwa karibu na mstari wa katikati ya uwanja.
- Nafasi kati ya mstari wa mabeki na mstari wa viungo. Ilikuifanya hii nafasi iwe kubwa yakutosha, James na Caicedo walishuku chini kuelekea golini kwao ili kumvuta Luiz na Neves.
Goli la tatu Palmer alipokea mpira kwenye kwenye nafasi katikati ya mtari wa mabeki na viungo na kuweza kusafiri nao na kutoa pasi ya goli.
Kabla ya magoli haya kufungwa, tayari kulikwa na viashiria na majaribia kadhaa kushambilia hizo nafasi ambazo Chelsea hawakuzitumia vizuri ila PSG walishindwa kuzifanyia kazi.
Goli la pili ni la transition, PSG walipoteza mpira Chelsea walifanikiwa kumpa mpira Palmer ambaye alikuwa amekimbilia kwenye nafasi ambayo Mendez aliacha wazi wakati wakiwa wanapanga mashambulizi yao kabla ya kupoteza mpira. Takwimu za FIFA za kiufundi zinaonesya kwa timu zimeboresha ufanisi wa mashambulizi ya kustukiza ukilinganisha na kombe la dunia liliofanyika Qatar. Ukipoteza mpira kizembe utadhibiwa.
Kwa ufupi, Celsea walijua ni nafasi zipi mpizania wao anaacha wazi akiwa anafanya pressing lakini pia nafasi zipi anaziacha wazi akiwa anajenga mashambulizi yake. Lakini kujua tuu haitoshi, inabidi utelekeze mashambilizi kwa ufanisi wa hali ya juu kitu ambacho Chelsea walifanikiwa.
PSG mdebwedo…..
Kwa upande wa PSG, mambo kadhaa yawaliwaangusha.
- Walionekana kukosa nguvu au kuchoka, ile pressing yao ambayo imewasaidi kwa muda mrefu haikuwa na ukali uliozoeleka. Goli la kwanza Luiz anaonekana yupo sambamba na Palmer lakini wakati palmer anajituma kwa nguvu kuwenda kumalizia shambulizi, yeye anaonekana akiwa na jog taratibu. Pia mwanzo wa mchez katika dakika 10 za mwanzo, mipira mnne yote ya kugombania walishwa kuipata na ikishia miguuni ya wachezaji wa Chelsea.
- Uzembe kwenye utoaji pasina kuchagua pasi ngumu kuliko rahisi. Goli la pili PSG walikuwa na umiliki wa mpira ila walitaka kutafuta pasi ngumu ambayo haikuwa sahihi. Wakapoteza mpira na kuja kuuokota kunyavu. Hilo mfano mmoja tuu lakini kunamengine ambayo ni makosa pasipo kuwa na shinikizo lolote toka kwa mpizani (unforced errors).