Chelewa, Uzikwe

Kudo kama ipo sokoni tangaza tununue,tusijesubiri kumjua anaemlenga Mara miguu ya kuku akaja na misheni nyingine(kuna wanaosubiri mpaka leo kujua yaliyojiri Congo)
 
Kudo weka riwaya,au tangaza inauzwa tununue,najua unatumia muda pengine na pesa kuandaa riwaya zako,kwa kweli hatupaswi kuzipata bure labda uamue mwenyewe,lakini pia hupaswi kututesa kama tuna uwezo wa kununua,funguka kama inauzwa tuje inbox!
 
Muda ulinikimbia boss! Majukumu yananibana mbavu boss.. Lakini nitaendelea kuweka hapa leo.... Na nitaweka vipande viwili kwa siku ya Leo....
Bado haijakamilika, hivyo haiuzwi kwa sasa
 
RIWAYA; CHELEWA, UZIKWE.

NA; BAHATI K MWAMBA.

SIMU; 0758573660/0624155629.

SEHEMU YA NNE.

****

Alikuwa haamini kama kweli nyumba yake ilikuwa inateketea kwa moto, nyumba ambayo aliipenda kuliko kitu chochote kile.

Ukiachilia mbali nyumba, pia kulikuwa na magari na pikipiki kadhaa ambazo alizinunua kwa sababu ya kazi yake ya umamluki.

Hakika lile lilikuwa ni pigo kubwa kwake.

Wakati akiwa bado amepiga magoti, alisikia sauti za hamaniko kutoka kwa watu waliokuwa wakisogea pale. Aligeuka na kutazama sauti zilipokuwa zinatokea.

Aliona makundi ya watu yakiwa yanasogea pale, alitambua walikuwa ni majirani zake ambao walikuwa wanakuja kutoa msaada.

Haraka alisimama na kuificha vizuri bastola yake na kuanza kuelekea karibu na nyumba yake iliyokuwa ikiungua.

Alipiga hatua chache na kusimama, kisha aligeuka na kutizama kwenye kiuchochoro fulani.

Hisia zake zilimwambia aliona mtu wakati alipokuwa akigeuka kuwatizama watu, waliokuwa wanazogoa kuja kushangaa nyumba yake.

Haraka alipiga hatua na kuelekea kwenye ule uchochoro, lakini hakuna alichoambulia zaidi ya ukimya mkubwa.

Aliinama chini na kugusa ardhi taratibu sana.

“Kulikuwa na kiumbe maeneo haya!” Alijisema taratibu huku akiinuka na kuutazama uchochoro ule kwa mashaka makubwa.

“Kama ameshindwa kuniua leo, hatoweza kuniua siku yoyote katika maisha yake.” Alijisemea huku akiondoka eneo lile na kuwafuata majirani zake, ambao walikuwa wanapiga kelele za hamaniko na woga.

Alijiunga nao na baadhi walianza kumpa pole kwa kuunguliwa na nyumba yake. Wengine waliwasiliana na jeshi la uokozi.

Saa moja baadae, jeshi la uokoaji lilikuwa linafanya kazi yake, huku polisi wa kawaida na wao wakiwa wamefika eneo lile na kuanza kumhoji chanzo cha moto ule.

Ilimlazimu kudanganya, alisema yeye ndiye chanzo cha kuungua kwa nyumba yake, kwa kuwa alifungua gesi na kujisahau, kiasi ilisambaa nyumba nzima na alipojaribu kuwasha jiko, moto mkubwa ulizuka na yeye alifanikiwa kutoka salama.

Uongo wake ulimuokoa, kwani hakukuwa na maswali mengi juu yake.

Aliongopa kwa kuwa alijua namna polisi wetu wanavyokuwaga wavivu kufuatilia mambo magumu. Polisi wetu huwa ni watu wa kurahisisha mambo bila kuwa na maswali ya kwanini.

Aliokoka kirahisi kwenye kesi ngumu na badala yake, alisaidiwa na kupewa pole, kisha aliachwa ajihangaikie kupata makazi.

Majira ya saa nne ahsubuhi yalimkuta akiwa anaingia kwenye nyumba yake maeneo ya Magomeni.

Aliingia ndani huku akili yake ikiwa mbali kwa kile kilichokuwa kimetokea usiku.

Alipitiliza hadi kwenye chumba kilichokuwa kinatumika kwa matibabu. Aligonga mara mbili na kutulia, kisha aligonga kwa mara nyingine tena.

Sekunde chache baadae, mlango ulifunguliwa na alikutana na bastola ya Dokta Masu.

“Easy Boy! Am back!” Miguu ya kuku alimwambia huku aliingia ndani.

“Umemaliza kumpa tiba huyo Mzee?” Alimuuliza Dokta Masu.

“Yes, nimemaliza na hapa tulikuwa tunakusubiri na ungechelewa dakika kumi zaidi, ningeanza kukufuatilia” Dokta alisema huku akiweka bastola yake kwenye meza.

“Kimetokea nini huko?” Alfa aliuliza huku akijiinua kitandani.

“Nyumba imeungua na sijaokoa kitu chochote!” Miguu ya kuku alijibu huku akivua koti alilokuwa amevaa.

“Eeh!”

“Yes, imeungua na imeinguzwa na mtu..” Alisema huku akimtupia kipande cha karatasi alichokitoa kwenye mfuko wa koti lake.

“Remember the name!..” Alfa alikisoma kwa sauti, kisha akauliza.

“Ni nini hiki!?”

“Ni karatasi niliyoikokota kando ya ukuta wa nyumba yangu, sijui na sielewi inamuhusu nani!”

“Remember the name!” Alfa alirudia kusoma kwa sauti.

Chumba kilipitiwa na ukimya wa sekunde kadhaa, huku kila mmoja akiwaza lake.

“Huyo mtu anajaribu kukumbusha kitu, bila shaka mnafahamiana” Dokta Masu aliamua kuuvunja ukimya.

“Mwanzo nilihisi tunafahamiana, lakini baadae nimegundua hili tukio la kuchomewa nyumba, linahusiana na hili la Alfa kuvamiwa nyumbani kwake!” Miguu ya kuku alisema analowaza.

“Bila shaka linahusiana kwa karibu sana na ninahisi linahusiana na kile ulichoenda kukifanya Goma, Congo. Jambo hili linaanzia huko.!” Alfa alisema.

“Hebu ngoja,” Miguu ya kuku alisema huku akimgeukia Dokta.

“Umefanikiwa kutoa risasi iliyokuwa mwilini mwa Alfa?”

“ Ndiyo!”

“Umeona ni aina gani hiyo?”

“Kwa haraka nimeona inatoka kwenye ganda lenye kipenyo cha milimita 8•5”

“Hii ni risasi inayotoka kwenye kitengo cha siri nchini Congo na anaewauzia silaha hizo ni Bob Rando, kwa sababu sharia za kimataifa hazijarihusu aina hiyo ya risasi kutumika vitani..” Miguu ya kuku alisema huku akikuna kichwa chake na kuchukua simu yake, kisha alifungua sehemu ya ujumbe wa barua pepe na kutuma ujumbe kwa mtu fulani. Alipohakikisha ujumbe umepokelewa, alimgeukia Dokta Masu.

“Ni vema uende, hili jambo nitalishugulikia na endapo nikihitaji msaada, nitakutafuta.”

“Hamna shaka, lakini kuwa makini, hawa jamaa naona wamejipanga sana!”

“Usitie shaka, kikubwa hakikisha simu yako iko hewani muda wote. Msaada wako utahitajika wakati wowote”

“Tuko pamoja!” Dokta alijibu huku akibeba begi lake na kuondoka.

Ndani ya chumba cha matibabu, walibaki Alfa na Miguu ya kuku. Walihutaji kujadili jambo wakiwa wawili.

Lakini kichwa cha Miguu ya kuku bado kilikuwa na mashaka na watu watatu, ambao wangeliweza kuhusika na tukio la kumtafuta usiku na kumchomea nyumba yake, hakuwa akitaka kukubali kirahisi ya kwamba, waliomtenda ndiyo hao hao waliomtenda Alfa.

Hesabu ziligoma. Mchezo ulichezwa na vichwa tofauti.

Kwa nini?

Kwa sababu mwandiko uliokuwa kwenye karatasi, haukuwa mwandiko wa mwanaume.

Kengele zikalia kichwani mwake. Kuna namna alihisi kuhusu huyo mtu aliyemchomea nyumba yake.

Miguu ya kuku alikaa kwenye kiti na kumtazama Alfa kwa jicho kali.
.
.
.
.
.
.ENDELEA KUWA NAMI
 
Good
 
Toeni pesa mtumiwe whatsup,mimi nishaimaliza nasubiri misheni nyingine ya miguu ya kuku!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom