Cheka Unenepe!!

Cheka Unenepe!!

Song'ito

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2011
Posts
348
Reaction score
150
*************************************************************************************************************

Dada mwenye mtoto mchanga aliingia ndani ya basi kupitia mlango ulio karibu na dereva, dereva alipomwona mtoto wake akamwambia

" Hakya nani tena dada sijawahi kuona mtoto mwenye sura mbaya kama huyu wa kwako… sipati picha baba ake atakuwaje"

Mdada akiwa amekasirika akaenda nyuma kabisa ya basi akakaa karibu na baba mmoja mtu wa makamo. Dada akamwambia yule baba "dereva wa gari amenidhalilisha sana leo kwa kweli"

Huyo baba wa karibu yake akamwambia "usikubali hata, nenda mbele kamwambie ukweli, na wakati unaenda unaweza kuniachia huyo nyani wako nikuangalizie"

Dada akazimia



*************************************************************************************************************
Watu watatu waliokuwa wanasafiri kupitia jangwani walikwama katikati ya jangwa baada ya gari yao kuharibika…wakahangaika sana bila mafanikio ili wajiokoe lakini hawakufanikiwa…wakiwa wamekata tamaa wakatokewa na malaika na kuwaambia kila mmoja aseme kitu chochote anachotaka na atatimiziwa.

Wa kwanza akasema anataka awe nyumbani, mara akawa nyumbani kwake mda ule ule..

Wa pili vile vile akataka awe nyumbani ikawa hivyo....

Wa tatu yeye baada ya kufikiria akasema, " nipo mpweke sana, natamani ningekuwa na rafiki zangu" mara ghafla bin vuu wakawa wote watatu jangwani tena.

************************************************************************************************************
 
ah haaa haaa haaa...................masikiiini dada wa watu
 
nimetosheka ngoja niende mjini sasa!
 
hahahahahahah...
............... nyani wako nikuangalizie!
 
dah! Huyu jamaa wa kumuomba nakumbuka kisa cha nabii fulani hahahahaha,noma tupu. Nalog off
 
Ka mi ningesema "haya huyapa nyani mwezako" nadhani angekufa.
 
Back
Top Bottom