Pengine haikuwa lazima, lakini kwa kuwarahisishia ufahamu nimejaribu kufanya tafsiri ya chapuchapu, haiko sahihi sana:
Bibie alifungua mlango wa danguro huko Winnipeg na kumwona bwana mmoja mtu na heshima zake, mtanshati na aliyevalia vizuri
Nikusaidie nini bwana? aliuliza yule bibie.
Bwana akajibu, Napenda kumwona Valerie
Bwana, Valerie ni mmjoa kati ya wasichana wetu Ghali sana. Pengine ungehitaji mwanamke mwengine
Hapana, mimi ninmtaka Valerie
Wakati wanazungumza yale, Valerie akachomoza mlangoni na kumwambia yule bwana kuwa anatoza $5000 kwa mara moja. Yule bwana bila kusita akatoa pochi na kuchomoa $5000 na kumpa Valerie., wakapanda gorofani.
Baada ya saa moja, yule bwana akaondoka taratibu.
Usiku wa pili, yule bwana akarejea tena. Valerie mwenyewe akashangaa kwani hakuna aliyekuja mara moja na kurejea kutokana na ughali wa huduma zake, na akamwonya Yule mteja wake kuwa bei ni ile ile, hakuna punguzo. Kwa mara nyengine tena, akatoa pesa na wakapanda juu.
Usiku ulofuata bwana alifika tena pale na kila mtu akaduwaa kuona amekuja siku tatu mfululizo, na vado akalipa na mambo yakawa kama siku zilizotangulia. Baada ya shughuli, Valerie akamwambia mteja wake,
Hakuna mtu amefika hapa siku tatu mfululizo. Unatokea wapi?
New Brunswick , Yule bwana akajibu.
Kweli?. Mimi nina jamaa huko New Brunswick
Naelewa. Dada yako amefariki na mimi ni wakili wake. Aliwacha urithi wa $15000 alizousia nikukabidhi, alijibu yule bwana.
Mafunzo ya hadithi hii ni mambo matatu ya uhakika (na machungu) ni:
Kifo. 2. Kodi 3. Kukazwa na wakili