Cheka amkimbia Dulla Mbabe, ashindwa kutokea ulingoni

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
52,090
114,627
Katika hali ya kushangaza mashabiki wa ndondi tumepigwa na butwaa baada ya Cheka kugoma kutokea ulingoni jana bkwa sababu zisizo na kichwa wala miguu

Akiongea na mashabiki mdhamini wa pambano hilo alisema kuwa atamshitaki Cheka kwa uhuni alioufanya kwa kuwa amemletea hasara licha ya kuwa alishachukua malipo ya awali.

Dulla Mbabe aliunguruma na kuwaeleza mashabiki kuwa ngumi sio maneno,amemtaka Cheka aache kidomodomo
 
Zama za cheka zshaisha,dulla naye akipata viongoz wazur atafka mbal
 
Upuuzi Kama huu Michezoni halafu wanaitisha kikao cha kujadili kwa nini Mchezo w ngumi hauna wadhamini.
Nilimsikia Cheka akisema walitaka apande Ulingoni bila ya kumpa Advance
 
Huyu jamani si kupigwa na ponjoro juzi juzi huko India? Hata muda wa kupumzika na ku recuperate kweli kaupata? Management yake wanataka auwawe? Good for him kwa kulikacha pambano
 
Katika hali ya kushangaza mashabiki wa ndondi tumepigwa na butwaa baada ya Cheka kugoma kutokea ulingoni jana bkwa sababu zisizo na kichwa wala miguu

Akiongea na mashabiki mdhamini wa pambano hilo alisema kuwa atamshitaki Cheka kwa uhuni alioufanya kwa kuwa amemletea hasara licha ya kuwa alishachukua malipo ya awali.

Dulla Mbabe aliunguruma na kuwaeleza mashabiki kuwa ngumi sio maneno,amemtaka Cheka aache kidomodomo
nenda kule facebook ukaone majibishano yao....baada ya api ndo utajua mchezo wa ngumi bado ni mchezo uliotawaliwa na wahuni ndo maana tabia na matendo ya kihuni huni bado yanaendelea kujitokeza
 
Ubabaishaji umezidi kwenye huu mchezo,aliwahi kugoma kupanda ulingoni siku ya pambano akitaka kulipwa chake kwanza.
 
nenda kule facebook ukaone majibishano yao....baada ya api ndo utajua mchezo wa ngumi bado ni mchezo uliotawaliwa na wahuni ndo maana tabia na matendo ya kihuni huni bado yanaendelea kujitokeza
Mchezo wa ndondi ni ya wahuni.

Watoto wa manzese,keko na magomeni kagera hupenda huu mchezo lkn wote wahuni

Na wacheza ndondi wengi hutokea maeneo haya na kumbi za mapigano yapo maeneo hayo

Mfano mzuri marehemu mashali alikuwa mhuni vibaya pamoja na crew yake nzima hapo manzese na mwisho wake tumeuona

Wacheza ndondi wengi 97% wahuni ,hayo majibizano subiri nikayatizame
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom