Cheka adundwa na Mashali

MRSH

Senior Member
Dec 27, 2012
104
21
Bondia maarufu nchini Thomas Mashali amefanikiwa kumpiga kwa pointi bondia mgumu nchini Francis Cheka kwenye pambano la raundi 10 lililopigwa usiku wa Christmas (December 25, 2015) kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Pambano hilo la uzito wa Kg 77 ambalo lilikuwa si la ubingwa liliwakutanisha wawili hao ili kukata mdomo wa nani mkali kati yao na hatimayeThomas Mashali akafanikiwa kumkalisha Cheka akiwa kwenye uwanja wake wa nyumbani.

Kwa muda mrefu Cheka amekuwa mgumu kupigwa akiwa Morogoro lakini Mashali amevunja mwiko huo kwa kumchakaza Cheka kwa pointi.

Majaji wamempa Mashari pointi 94, 96 na 97 wakati mwenyeji Cheka amepata pointi 96, 93 na 93.
 
Ila Mashali naye ni mbishi.Alitembezewa kisago last time hadi network ilipotea.Mwanzo nzuri sana.
 
Kodi imekusanywa kiasi gani ndo interesting point to hear. Haya mapigano yasiyokuwa hata na chanzo cha ugomvi yawanufaishe mpaka wazee wetu kijijini msoga na kwingineko
 
Sina uhakika kama Serikali inafuatilia kodi katika mchezo huu.Ni kama wanauona sio mchezo rasmi.
 
Kodi imekusanywa kiasi gani ndo interesting point to hear. Haya mapigano yasiyokuwa hata na chanzo cha ugomvi yawanufaishe mpaka wazee wetu kijijini msoga na kwingineko

Msoga wameshanufaika na macontainer yaliyotoroshwa bandarini.
 
Hahahaaaa.RItz ameshakanusha tuhuma zote anasema hana Lori wala basi.Watu wamepanga kumchafua.
 
.ni starehe kama vigodoro au. kuvuta kamba hii ni Xmas na Maulid bado mwaka mpya
yasiyowahusu tukakae kwenye stuli ndefu kushangilia ManU
Cheka si alifungwa? Kwa kumpiga Meneja wake hapo ndipo mtajua tupo mbali na hii mieleka
 
Au jamaa hakuwa fiti baada ya kutoka jela ndo msela kapata chance.😁
 
Cheka kaisha...na ngumi zitadorora

Cheka alikuwa na nidhamu sana

hao kina Mashali bangi sana
unaweza andaa pambano asitokee
 
...Cheka bado yupo,na ataendelea kuwepo, that'z a one off that'z all,mtu ashindwe kwa point iwe sababu ya kuisha, no never.Maandalizi kabla ya pambano ndio hayakua mazuri,na yale yaliyomkuta nje ya ring miezi michache iliyopita ndio sababu ya kupigwa kwake, but i do still believe, that lion will be back, to prove all of you wrong!
 
Back
Top Bottom