sammosses
JF-Expert Member
- Jan 24, 2011
- 1,745
- 1,171
Ni vizuri uwanja wa media ukawa sawa hususani kipindi hiki ambacho tunaelekea kufanya uchaguzi wa viongozi wakuu wa nchi hii. Unapofanya mjadala kwa kuibua hoja na kuruhusu kutoa mwanya kwa watu fulani kuwashambulia wengine na kuwazuia wengine ni kuupotosha umma. Media zinatakiwa kuwa balanced katika kipindi hiki bila kujali mmiliki wa chombo hicho ni kada wa chama gani.
Kuna suala la maadili ya utangazaji ambayo yanakiukwa kwa Watangazaji kulinda ugali wao wa siku kwa kuogopa au kukiukwa matakwa ya waajiri wao na kuamua kuidhalilisha taaluma yao ambayo ni muhimu sana kwa umma. Ikiwa kwenye utawala huu wa sheria ambao unabagua na kuwafungia wale wote wanaoisema na kusemea mapungufu ya serikali na kuwaacha wale ambao wanatumia media zao kuwashambulia wengine bila kuwaonya na kuwafungia kwa kuwa tu wanatumwa na makada ambao wameishika nchi hali kama hii ni hatari kwa usalama wetu na uchaguzi kwa ujumla wake.
Mtangazaji Arap Chang aliingia kwenye mkumbo wa machafuko yaliyotokea kipindi cha uchaguzi huko Kenya kwa kuendeleza ushabiki ambao leo hii Star Tv na mwenzake wa Channel Ten wamekuwa wakiushiriki. Ni hatari sana tukinyamaza bila kulikemea hili kwani hata vitabu vitakatifu vimesema tukatazane mabaya na tuamrishane mema.
Sina mashaka kabisa na chama fulani kuelezewa mabaya yake,mashaka yangu kwa vyombo hivi ni kutokufanya check and balance kuhakikisha wanaita pande zote zinazopingana ili kuweza kutolea ufafanuzi wa mambo ambayo yanaonekana si salama kwa taifa ili upande unaotuhumiwa uweze kutoa ufafanuzi pale pale kuliko kinachofanyika hivi sasa. Niwasifu sana watangazaji wa kipindi cha malumbano ya hoja kwa umahiri wao wa kuzuia hoja zilizo nje ya mada na kukataa kutoa nafasi ya mashambulizi kwa mtu ambaye hayupo ndani ya mjadala huo.
Nachelea kusema hivi kutokana na aina ya ukiukwaji wa maadili ya utangazaji kwa media zetu kujikita kwenye ushabiki ambao unaonekana ni mkakati fulani ulioandaliwa kwa madhumuni fulani ili kumdhoofisha mtu fulani kwa malengo fulani. Mikakati kama hii mwisho wake huibua hisia na mihemuko ya wapenzi wa wale ambao wamenyimwa fursa ya kutolea ufafanuzi kwa mambo wanayotuhumiwa nayo kwa kuwa tu uwalikaji wa waibua hoja umelenga kunufaisha upande fulani.
Mwisho,Tanzania ni nchi yetu sote tuwe makini kwa kila jambo kwa tafakuri za kina ili kuondoa viashiria vya uvunjifu wa amani ambavyo vinaweza kuvunja uvumilivu tulionao Watanzania wengi ambao uvumilivu huu umetumika kama mianya ya kuwanyonya na kuwapuuza wananchi wanyonge walio wengi,nawakilisha