Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Katibu Mkuu wa Chama Cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Salum Mwalimu ametoa wito kwa watumishi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), kutenda haki katika kusimamia uchaguzi Mkuu wa Oktoba baadaye mwaka huu.
Ametoa wito huo leo Juni 7, 2025, baada ya kuungana na waumini wengine wa dini ya Kiislamu kwenye swala ya Eid al-Adha katika msikiti wa Bakwata Mkoa wa Simiyu – Masjid Noor, uliopo Bariadi.
Akizungumza baada ya kumaliza kuongoza harambee ya kuchangisha fedha za ujenzi wa msikiti huo, Mwalimu amesema wanaposherekea sikukuu hiyo viongozi wasihubiri amani bila haki, hasa kwa kuwataka wasimamizi wa uchaguzi wakatende haki.
"Tunapohimiza amani tuhubiri na haki, vyote viende sambamba na hata watendaji watakaoenda kusimamia uchaguzi mkuu wakatende haki ili tukimaliza wote tuwe wamoja," amesema. Mwalimu
Pia amewataka waumini hao na Watanzania kwa ujumla kujitokeza kushiriki haki hiyo ya msingi ya kuchagua, kuchaguliwa na kupiga kura kama Katiba ya Tanzania inavyoeleza.
"Mkashiriki uchaguzi. Msirudi nyuma, nendeni mkagombee udiwani, ubunge na urais, tukapeane mawazo kuhakikisha tunashinda na kupata viongozi watakaokuja kuondoa matatizo yanayowakabili Watanzania," amesema Mwalimu