Chatu wa mila asababisha hofu kijijini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chatu wa mila asababisha hofu kijijini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mkwele, Jan 4, 2011.

 1. M

  Mkwele JF-Expert Member

  #1
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Source: Mwananchi

  Chatu wa mila asababisha hofu kijijini
  Monday, 03 January 2011 19:58


  Joseph Lyimo, Kiteto
  WAKAZI wa Kitongoji cha Kazaroho, Kijiji cha Matui, wilayani Kiteto, mkoani Manyara wanaishi maisha ya hofu na kushindwa kufanya shughuli za maendeleo kwa kuogopa nyoka aina ya chatu anayetishia maisha yao kwa zaidi ya miezi mitatu sasa.

  Kufuatia hofu hiyo, wameomba serikali kupitia idara ya wanyamapori, kumsaka nyoka huyo na kumuondoa kwenye makazi yao.

  Wakazi hao walidai kuwa, nyoka huyo anayekadiriwa kuwa na uzito wa kilo 80, amekuwa akifanyiwa tambiko na wenyeji wa Kabila la Warangi na Wagogo kwa kumpa unga na maziwa, ili asilete madhara ndani ya kijiji hicho.
  Mmoja wa wakazi hao, alisema nyoka huyo ana zaidi ya miezi mitatu kijijini hapo na wazee maarufu walipomuona, walitaka wananchi wasimdhuru kwani kuna masuala ya mila walitakiwa kufanya.

  "Kwa kipindi chote hicho, makabila ya Warangi na Wagogo wamekuwa wakishughulika naye, lakini baada ya kuanza shughuli za kilimo watu wamepata hofu kubwa huenda akaleta madhara kwa jamii," alisema.
  Akithibitisha kuwepo kwa nyoka huyo, Diwani wa kata hiyo, Kidawa Othmani (Obama), alisema tayari amewasiliana na maofisa wa maliasili ili wamuondoe.

  Othman alisema kutokana na malalamiko ya wananchi kuwa, hawawezi kuamini usalama wao wamemtaka kutoa taarifa ili nyoka huyo aondolewe kijijini hapo sio kuuawa.

  "Kwa kweli hali sio shwari hasa kipindi hiki cha kilimo, kila mtua anataka kwenda kufanya kazi zake maporini, sasa wanapokutana na nyoka huyo mara kwa mara inawatisha," alisema.

  Alisema hadi jana, maofisa hao walikuwa hawajafika na ametaka serikali inapojulishwa kuhusu hatari ndani ya jamii kufanya haraka kabla ya madhara.

  "Nimeongea nao mwenyewe asubuhi (maofisa wa maliasili), wakaniahidi wanakuja lakini hadi hii jioni (jana) hawajafika, hali hii inaweza kubadilisha matokeo," alisema.


  Kwa nini watu bado tuna imani ya watu wa karne ya 19?
   
 2. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #2
  Jan 4, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mila nyingine nazo za hatari sana mpaka mtu afe ndo wanashtuka! Na akifa pia wanaweza kusema ni mambo ya mila ' labda babu kamuita au alimkosema bibi nk'' Mtafuteni huyo nyoka wadau kabla hajadhuru watu
   
 3. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #3
  Jan 4, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Kwani huyo chatu kaja lini hapo kijijini na nani kamleta? na hiyo mila ni mpya?

  Kama haikuwepo zamani wamuue hana cha mila wala nini imani potofu tu!
   
Loading...