Mimi naona sawa tu kama ni sheria inayohusu Chato, jaribu kudadisi zaidi kama madiwani wa Chato walikaa wakakubaliana sheria hiyo iwepo. Miji mingi nchini ni mchafu, ili kujenga utamaduni wa kufanya usafi na kutotupa taka hovyo, inabidi kujiwekea taratibu kama hizo. Matunda yake utakuja kuyaona muda si mrefu!!
Hata siku moja huwezi ukalazimisha suala la usafi kwa nguvu. nitapita mwakani kushuhudia usafi wa chato uefikia wapiMimi naona sawa tu kama ni sheria inayohusu Chato, jaribu kudadisi zaidi kama madiwani wa Chato walikaa wakakubaliana sheria hiyo iwepo. Miji mingi nchini ni mchafu, ili kujenga utamaduni wa kufanya usafi na kutotupa taka hovyo, inabidi kujiwekea taratibu kama hizo. Matunda yake utakuja kuyaona muda si mrefu!!
Haina maana kufanya kazi na kurundika uchafu bila kuuondoa na kuuchoma.
Ni sheria nzuri japo kwenye utekelezaji ndio kunaleta kizungumkuti
OTIS
Napenda kufahamu jambo moja muhimu, je ni amri kutoka kwa Mkuu wa wilaya au ni mapendekezo ambayo wananchi wameyapokea na kuyafanyia kazi kwa utaratibu waliojiamulia kwa vikao husika?
Kwa maoni yangu kutokana na tabia mbaya tuliyojijengea wa -TZ wengi(si wote) hatufanyi kitu kwa ridhaa zetu hasa usafi na utunzaji mazingira ndio maana miji/mikoa mingi ni michafu na maendeleo ni duni, ukiuliza kila mtu atatupa lawama sehemu/mamlaka fulani bila kujali yeye mwenyewe amewajibika vipi katika hilo.
Kuhusu muda wa kazi, kidogo hapo inatakiwa busara itumike kutokana na mazingira mahalia na shughuli zao za uzalishaji mali zikoje,ingawa nina wasiwasi kidogo kuwa sehemu nyingine utakuta mtu aneyelalamika ni mchezaji wa pool table kutwa nzima nje ya grocery fulani kama tulivyozoea kuwaona baadhi ya vijana ambao ndio nguvu kazi ya Taifa wanavyofanya sehemu nyingi ya nchi hii hivi sasa.
Otherwise Big up Mkuu wa Wilaya na jopo lako kwa maamuzi/amri sahihi kwa jamii husika.
Hizo ni taratibu walizojiwekea.. kwani wana chato wamelalamika? hata Tanga nakumbuka enzi za Kalembo kuna kipindi walikua na utaratibu kama huo sijui kama bado unaendelea