Chato tunaomba tujengewe Chuo Kikuu

Honestly Bukoba nzima hakuna chuo kinachoeleweka halafu Chato mjengewe chuo hapo kuna nini cha maana? Kuna watu wabinafsi sana ila nyie Chato line ninwa tofauti inabidi tutafute history yenu mmetokea wapi nyie?????? Niliwahi kufuatilia nadhani sababu Mwanza kuna vyuo vya kutosha basi hata shinyanga ndio wangejengewa chuo huo ni mkoa mkongwe lakini unazidiwa hadi na wilaya kama kahama . Labda kikijengwa chuo itaongeza mzunguko wa watu na pesa. Au huko bukoba Ila sio Chato NO
 
Mbona una wivu na Chato ndugu?
 
Ni kweli kabisa Kamanda. Chuo Kikuu kijengwe walau kimoja kuhudumia mikoa 6 jirani (Geita, Simiyu, Katavi, Tabora, Shinyanga, Kigoma, watu 20 milioni) sasa wana Chuo Kikuu kimoja (Kipalapala Seminary). Linganisha na Watanzania wengine Kilimanjaro, Manyara na Arusha (mikoa 3, watu milioni 8) wana vyuo vikuu 7 (Arusha Tech, Makumira, IAA, Chuo cha Polisi, Kilema, KCMC, ESAMI). Ni nchi moja, of course, wote tunasoma kokote.
 
kabla ya Chato lazma kile cha Butiama kianze! Ikumbukwe Mkulu alisimamisha ujenzi wa Chuo cha Kumbukumbu Butiama! Na kiukweli Geita mjini itafaa zaidi ujenzi wa chuo zaidi ya Chato kuondoa dhamira ya Chato kujitenga na mkoa wa Geita!
 
Kisipojengwa awamu hii tusahau kupata chuo kikuu cha serikali kanda hii walivyopania kutukomoa sisi wa huku.
Ninachojua hela hakuna,inaweza chukua miaka 2 kuweka mambo sawa,miradi mingi iliyoanzishwa haijakamilika.A country is not a company .
 
kabla ya Chato lazma kile cha Butiama kianze! Ikumbukwe Mkulu alisimamisha ujenzi wa Chuo cha Kumbukumbu Butiama! Na kiukweli Geita mjini itafaa zaidi ujenzi wa chuo zaidi ya Chato kuondoa dhamira ya Chato kujitenga na mkoa wa Geita!
Cha butiama kitasubiri nina matumaini kwa soon kutakua mkoa mambo yataiva!
 
Kama ni kutekeleza ilani ya uchaguzi. Nasi wa Ukerewe tujengewe. Au kwa sababu JPM alitokea kwenu ndio maana waomba? Nyie mwaomba chuo sie hata barabarabna umeme hatuna na ilani ahadi zilitolewa











V
 
Ngoja tuksmilishe hospitali kwanza. Mnakumbuka Geita mjini hakuna hata taa za Barabarani eee!...
 
hiko chuo cha polis ondoa hapo. kile si chuo cha kiraia.
 
Ni roho ya ubinafsi iliyowajaa watu wa Bara.

Vyuo vilivyopo Tanzania ni vingi na havijajaa na vingine vimefungwa kwa kupungukiwa vigezo.
Ni vema vikaimarishwa vilivyopo ili viwe na hadhi y kimatafa sio kujenga vyuo vya kata visivyokidhi vigezo na hadhi za kimataifa.
 
Kinajengwa chato kama mkoa au.
Mbona mnaikosea heshima Geita kama mkoa.
 
Chuo kikuu hicho Kwio
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…