Chatanda: Tundu Lissu lazima ang'oke!

Chatanda: Tundu Lissu lazima ang'oke!

Wana singida mashariki wajiandae kula mamilioni ya mafisadi katika mkakati wao wa kutaka kumng'oa lissu kwenye ubunge! Yatatengwa mamilioni ya fedha kwa ajili hiyo!
 
By the way nguvu na kiburi cha huyu mama ilikua ni Lowassa kule Arusha. Lowassa hayuko Singida. Pia ikumbukwe wabunge wengi wa Chadema ni wabunge wa taifa zaidi kuliko majimbo. Watu wako tayari kusafiri kwenda Singida kulinda kura za lissu tu.

Hujui unacho kisema. Huyu mama hakuwa na Lowassa bali alikuwa adui namba moja wa Lowassa. Lakini walimchosha akachoka. Singida ndiyo ataipata fresh kwa mpingo Lisu.
 
Akuna wa kumzuia Lissu! ata Jk mwenyewe awezi awezi.
 
Wewe mama umekimbia mabwana za watu kule arusha sasa umekuja huku singida sisi tutakushikisha adabu kama uliopata arusha karibu mashababi tupo kwa ajili yako arusha walikupika singida tutakupakua kotekote karibu
 
Atuambie kwa nini mapato ya ccm kwenye jengo imepaa baada ya yeye kuondoka?, suala lla Lissu isiwe sehemu ya kutafuta mwamvuli!, kwa lissu anaota,labda akirejesha fedha hizo alizokwiba!
 
Lisu siyo wa nguvu nyingi kumuondoa mwepesi sana wakati ukifika mtayaona.

Hivi huwa mnaona sana sifa kuitwa mwanaccm. Nimewaona wanachama wa kwanza wakipewa kadi mwaka 77, wakishindwa na kutamka jina la CCM, Mapinduzi, Mapundusi, gidumu, wote nao wakumbuka wametangulia mbele za haki na umaskini wao. Tulicheza ngoma sana siku hiyo, ngonjera tulitamba sana, Chama Kipya kimeingia nchini! Alama Jembe Nyundo. Tuliimba. Nilicheza ngoma nikapata senti hamsini? ilikuwa hela kubwa sana. Nilikuwa gumzo tarafani. Kiwanja tulichocheza nilipita juzi kimekufa? umaskini tele kuliko hata 77. NI mwenye utindio wa bongo ndiye anayeweza kujisifu kwa kumwondoa Lissu. Ni fisadi, mnafiki, asiyeipenda nchi yetu, atakayependa watu kama Lissu wasiongee. Nilishajikomboa
 
Lazima ang'oke kwa sababu Zipi? Katiba ya JMT Inasema Kwamba mbunge ni mwakilishi wa watanzania, sio wa jimbo lake tu. Je mama Huyu anajua ni mangapi lissu amewafanyia watanzania bila ya kujalisha itikadi zao? Ni Kwamba tu akili Zetu zinaendeshwa na matumbo badala ya ubongo, hivyo kushindwa kuona mambo rationally and objectively. Pia ni Kwamba we are taking things for granted kwasababu tunaishi ndani ya mabadiliko, Vinginevyo lissu ameshaingia Katika vitabu vya historia na Hakika jina lake litatajwa sana miaka mingi ijayo nchi hii itakapokuja kombolewa kutoka kwa mafisadi na manyang'au wasio heshima Sheria na Haki za wananchi. Hata Kama itakuja kuwa mwaka 2090, lissu atajadiliwa kama mashujaa wa harakati hizo.

Sent from my iPhone using JamiiForums

.....salute GT !!!
 
Baada ya kufikiria kuleta maendeleo, anazungumza utumbo.!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Hatimae aliekuwa katibu wa CCM mkoa wa Arusha na kuhamishiwa Singida, Mary Chatanda, ametua mkoani humo na kutangaza kuongoza vita kali ya kuhakikisha Mbunge wa Iramba (M) - CDM Mhe, Tundu Lisu anang'olewa katika uchaguzi Ujao.

Itakumbukwa Mama huyu ndio yule aliyeshindwa vibaya sana katika vita ya aina hii hii dhidi ya Mbunge wa Arusha Mhe, Lema wakati akiwa mkoani humo.

Haya sasa vita inahamishiwa Singida.
Wewe hujuwi unachokiandika Kwani Tundu Lissu ni mbunge wa Iramba Magharibi? Lissu ni mbunge wa Singida Mashariki kwani Iramba Magharibi kwa sasa Iramba ni Mh Nchemba! Na Singida Magharibi jirani na Lissu ni Mh Misanga!

Next time kabla hujaandika ni bora kujiridhisha kwani usiwe na haraka Kama mkojo wa asubuhi au vijana wa Bavicha!
 
Muda wote maccm wanafikiria namna ya kunyang'anya wapinzani majimbo kwa gharama yoyote ile iwe kwa kuhonga, kuiba kura na hata kuua na kujeruhi. Ccm imepoteza utu kabisa katika taifa hili!
 
Hatimae aliekuwa katibu wa CCM mkoa wa Arusha na kuhamishiwa Singida, Mary Chatanda, ametua mkoani humo na kutangaza kuongoza vita kali ya kuhakikisha Mbunge wa Iramba (M) - CDM Mhe, Tundu Lisu anang'olewa katika uchaguzi Ujao.

Itakumbukwa Mama huyu ndio yule aliyeshindwa vibaya sana katika vita ya aina hii hii dhidi ya Mbunge wa Arusha Mhe, Lema wakati akiwa mkoani humo.

Haya sasa vita inahamishiwa Singida.

Mkuu rekebisha kidogo kwenye jimbo la Lissu.Huyu kamanda ni nbunge wa jimbo la Singida Mashariki,waweza muita mbunge wa Ikungi ukitaka.Iramba bado hawajajitambua lakini ndio tunapeleka dozi na soon before election watakuwa tayari.Huyu mama Chatanda atakufa kwa presha we subiri tu.Singida ya sasa si ya Ccm tena.
 
hatimae aliekuwa katibu wa ccm mkoa wa arusha na kuhamishiwa singida, mary chatanda, ametua mkoani humo na kutangaza kuongoza vita kali ya kuhakikisha mbunge wa iramba (m) - cdm mhe, tundu lisu anang'olewa katika uchaguzi ujao.

Itakumbukwa mama huyu ndio yule aliyeshindwa vibaya sana katika vita ya aina hii hii dhidi ya mbunge wa arusha mhe, lema wakati akiwa mkoani humo.

Haya sasa vita inahamishiwa singida.

tundu alishapoteza jimbo zamani sana
 
tundu lissu amekuwa mbunge miongoni mwa wabunge wa mfano wanaosimamia jambo lisilo la mkumbo na kuhakikisha kuwa wananchi wanapata haki yao
 
TUNDU LISSU ni Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki sio Iramba.

Huyo Mary Chatanda hana Hekima kabisa ni mwanamke wa Vurugu na machafuko tu.

Aache kuweweseka na kutoa mapovu bure hilo jimbo bado ni la CHADEMA mpaka 2020.
 
Back
Top Bottom