Charles Hillary: Nimestaafu kwa Hiari

Charles Hillary: Nimestaafu kwa Hiari

idoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2013
Posts
3,051
Reaction score
1,423
Akizungumza kwenye kipindi chake cha mwisho, Dira ya Dunia, mtangazaji mahiri wa radio na televisheni, Charles Hillary, ametangaza kustaafu rasmi kazi hiyo. Amefanya kazi na BBC-Swahili tangu mwaka 2006 mpaka Aprili, 2015 akitokea DW-Swahili alipoanza mwaka 2003 baada ya kuondoka Radio One alipofanya kuanzia mwaka 1994. Kabla ya hapo aliwahi pia kufanya kazi na RTD. Amesema ametimiza umri (wa zaidi ya miaka 55) wa kustaafu kwa mujibu wa sheria.
 
Last edited by a moderator:
Daah.. Mbona bado anahitajika sana kwenye tasnia hii ya utangazaji na haswa wa mpira wa miguu..
 
akija bongo watampatia ligi kuu aichangamshe!

Nadhani Azam Media watafanya la maana wakimchukua huyu jamaa.. Ana kipaji cha pekee katika utangazi wa kandanda.. Hata kama mpira ni mbovu na hauvutii Charles anaweza akakufanya uusikilize..
 
Zamani angerudi TBC ila sahivi wanaelekea Azam kuifanya iwe BBC ya Afrika,karibu utusaidie kutangaza Mpira make wanaotangaza sahivi hawachangamshi vilivyo
 
Huyu jamaa ni mtumwa,

Hataki kuitwa chalesi, ni lazima eti umuite kizungu chaaz.

Ni mtumwa tu.
 
quote_icon.png
By jogi
Huyu jamaa ni mtumwa,

Hataki kuitwa chalesi, ni lazima eti umuite kizungu chaaz.


Ni mtumwa tu.
Chalesi ndio nini?
hahaha!! jamaa analeta uchagga hapa. hajui hata hiyo 'chalesi' anayosema inatokana na 'chaz'!! teh teh teh!!
 
Nadhani Azam Media watafanya la maana wakimchukua huyu jamaa.. Ana kipaji cha pekee katika utangazi wa kandanda.. Hata kama mpira ni mbovu na hauvutii Charles anaweza akakufanya uusikilize..

Mpaka leo mnasikiliza mpira tu???
 
Back
Top Bottom