Chanzo ni leseni feki pekee??. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chanzo ni leseni feki pekee??.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by ngoshwe, Oct 7, 2010.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  Oct 7, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  [​IMG]
  THE NEW DRIVING LICENSE SYSTEM
  1.0 INTRODUCTION

  The government introduced a new computerized driving license system which has replaced the old system. The objective of this new system is to monitor and control issuance of driving licenses with a view to address the problem of fake licenses which are the causative for many road accidents
  The system meets international standards and has introduced important changes in the process of issuing licenses for driving motor vehicles in the country.
  So far nine driving license registration sites have been established in nine regions including Ilala, Temeke and Kinondoni tax Regions. Others are Kilimanjaro, Tanga, Arusha, Mwanza, Mbeya and Dodoma.

  Thereafter the system will be rolled out to the rest of the regions by December 2010.

  2.0 DRIVING LICENSE UNDER THE NEW SYSTEM
  The aim of introducing the new system is to replace the old system which did not differentiate between the types of licenses for driving passenger vehicles of different capacities.
  Under the new system specific class of driving license is designed to a certain class of motor vehicle only. Holders of driving license of certain class will be obliged to drive only such a class upon which he was tested for and not otherwise.
  In order to obtain the new driving license, all must undergo training to the recognized driving school (institutions) before they are issued with a new license.
  The system is categorized under different groups depending on the capacity of the vehicle namely:
  A - License to drive motor cycles with or without a sidecar and whose capacity exceeds 125cc or 230kg.
  A1 - Licenses to drive motor cycles without sidecar and whose capacity is less than 125cc or 230kg.
  A2 – License to drive motor powered tricycles and quadricycles.
  A3 – Licenses to drive moped whose capacity does not exceed 50cc.
  B – License to drive all types of motor vehicles except motor cycles, commercial, heavy duty and public service vehicles.
  C – License to drive public service vehicles with seating capacity of 30 and more passengers in addition to the driver, Vehicles in this category may be combined with a trailer having a maximum authorized mass of not more than 750kg. Applicants must have held Class CI or E license for a period of not less than three years.
  C1 - License to drive public service vehicles with a seating capacity of 15 but less than 30.
  Passengers in addition to the driver. Vehicles in this category may be combined with a trailer having maximum authorized mass of not more than 750kg. Applicants must have held Class D license for a period of not less than three years.
  C2 – Licenses to drive public service vehicles with seating of four but less than fifteen Passengers. Vehicles in this category may be combined with a trailer having maximum authorized mass of not more than 750kg. Applicants must have held Class D license for a period of not less than three years.
  C3 – Licenses to drive public services vehicles with a seating capacity of four or less passengers inclusive the driver. Vehicles in this category may be combined with a trailer having a maximum authorized mass of not more than 750kg. Applicants must have held a Class D license for not less than three years.
  D – License to drive all types of vehicles except motor cycles, heavy duty and public service vehicles.
  E - License to drive all types of vehicles except motor cycles and public serves vehicles. Applicants must have held Class D License for not less than three years.
  F – License to drive truck laying vehicles steered by their trucks.
  G – License to drive farm or mine vehicles.
  H – Provisional license for learner drivers.
  Under this system all information regarding drivers will be collected through a computer system for data capture before the new license are issued. The aim is to ensure that a correct license is issued to a proper holder depending on the motor vehicle and designed.

  3.0 VALIDITY OF LICENSE
  The driving license will be valid for three years and the driver will be required to renew it after this period. This requirement is based on the road Traffic Act No. 30 of 1973 as amended under ( CAP 168 RE 2002) together with the road traffic rules of 2004 and 2010.

  4.0 DRIVERS TEST
  Before issuing a driving license to an individual, he/she must first attend a driving training and qualify. Thereafter such a person will be tested and awarded license for the grade which he/she has applied for and passed.
  If a driver wants to drive various types of vehicles, he/she will be required to undergo training for all driving license categories and on passing the test he/she will be awarded a license that will show all the license categories which he/she has passed.

  5.0 FEATURES OF THE LICENSE
  The license will be in a form of a smart card with the national flag and emblem on it. It will also have personal information about the owner such as name, date of birth, license number, date and place of issue and expiry date.
  Together with this information which will be captured in the license, other details relating to the driver such as his/her TIN, gender, address, fingerprints and his/her signature will be in the license.
  6.0 OFFENCES
  All offences that will be committed by a driver will be captured by this new licensing system and this information will determine the fate of the license if the offence recurs.
  The license can be suspended or withdrawn depending on the gravity of the offences.

  7.0 CONCLUSION
  The objective of introducing this new computerized driving license system by the government is to capture the correct data about the driver that will help in monitoring them and ensure that the government gets its due revenue.
  It is the expectations of the government that this new system of issuing licenses will reduce road accidents which are mostly caused by drivers who do not have the necessary driving qualifications.
  Those who have old licenses should start to prepare the necessary documents like certificate of competence and for those who intend to apply for a new license to go for training.
  In this regard, members of the public are urged to start preparing themselves to get these new licenses.

  For more information please contact us

  MTAZAMO:

  Sina hakika sana iwapo kuna utafiti uliofanyika wa kuhusianisha ajali zinazoendelea kupoteza maisha yetu na ubovu wa mfumo wa kutoa leseni hapa nchini.

  Hakuna pia uhakika iwapo ni kwa kiasi gani lesini mpya zitadhibiti ajali iwapo mfumo wa usimamizi wa matumizi ya leseni hizo unaofanywa na askari wa usalama barabarani na mamlaka nyingine utaendelea kuwa ule ule wa kirushwa rushwa.

  Kwa nchi za wenzetu, mfumo uliopo ni pamoja na kukagua magari na kuyapasisha kwa kila mwaka kupitia mamlaka maalumu (kwa UK inafanywa na Inajukikana kama MOT - test kifupisho cha " The Ministry of Transport Test"). Hii inahakikisha kuwa magari mazima tu ndio yanayotembea barabarani na kama gari halijapasi viwango vya kiusalama na kimazingira (annual roadworthyness test) halipewi cheti na hivyo kutoruhusiwa kutembea barabarani. Mfumo wa usimamizi utalifuatilia vilivyo (monitoring). Jambo hili ni muhimu sana kwani hata dereva akiwa na lesini safi/halali, ikiwa chombo anachotumia ni kibovu, ajali hazitakwisha.

  Kwa upande mwingine, mifumo ya sheria iliyopo kwa nchi za wenzetu inawafanya raia kuhesmu sheria sio kwa hofu ya kufungwa au kutozwa faini bali kwa maana ya kulinda wengina na mali zao pia (compliance). Hii inafanya hata mtu akigundua unaedesha gari wakati amekuona ukibwia kileo sehemu, atawajulisha polisi haraka sana ili wakukamate haraka barabarani kabla hujasabaisha ajali.

  Aidha, ikiwa dereva wa chombo cha abiria kasababisha ajali , utaratibu uliopo ni kumbana kisheria huyo dereva na pia mwajiri wake (employer) hata ikiwa kampuni itafunguliwa mashtaka kisheria na kutozwa faini kubwa sana (kwa UK kwa kosa la ajali inayoababisha kifo kwa mujibu wa Sheria ya Mauaji ya bila Kukusudia kwa Makampuni " The Corporate Manslaughter and Corporate Homicide Act, 2007", faini yake haina ukomo "UNLIMITED FINE"), kufungiwa biashara au kampuni kuamriwa na mahakama kujitangaza kosa lake kwenye vyombo vya habari na kwingineko (publicity order).

  Hatua kama hizi kwa kampuni zinalenga katika kuhakikisha wamiliki wa Kampuni waajiri wanachukua tahadhali mapema kabla ajali haijatokea ikiwemo kuajiri madereva wanao faa, kuhakikisha wanaweka barabarni vyombo vyenye kuzingatia sheria za usalama na pia kutoa taarifa kwa wateja kuhusu tahadhari ya afya na usalama wao (health & Safety). Sheria hizi za usalama wa watu zinabana watoa huduma na wafanyabisahra wote katika sekta zote za kibishara sio usafiri pekee, ni katika maofisi, majumbani, kwenye huduma za starehe nk.

  Kwetu, ajali ikitokea, mwajiri anasukuma kesi kwa dereva na hata kama chombo kilikuwa kibovu, chombo kinatengenezwa haraka ili kiendeelee na biashara na thanamini ya maisha ya walioathirika na ajali inakuwa imepotea.
   
 2. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #2
  Oct 7, 2010
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  Kwa nchi za wenzetu, mfumo uliopo ni pamoja na kukagua magari na kuyapasisha kwa kila mwaka kupitia mamlaka maalumu
  Jana gari yangu haikupasishwa kwakuwa ilikuwa imuchubuka rangi kwenye bumper ya nyuma.........
   
 3. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #3
  Oct 7, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Mfumo huu ni mzuri na unaweza kupunguza ajali kama tu yafuatayo yatafanyika

  1. Kila leseni itakayotolewa inatakiwa kukatiwa bima itakayoambatana na gari lipi mwenye leseni atakuwa akilitumia (Hapa nina maana ya Reg # ya gari kuwekwa wazi) Ili mtu akisoma namba tu ni straight inajulikana possible drivers ni nani. Hili litaondoa mchezo wa day waka kwa wenye daladala na watu kuazimana magari ambayo wanakuwa hawana taarifa muhimu kuhusu condition ya gari.

  2. Leseni zote ziwe centralized, hivi vituo viwe ni kwa majaribio ya practical tu baada ya mtu kupass test ambayo ni computer based na anfanyia katika computer iliyo kuwa connected na central llicensing. Baada ya mtu kufaulu mtihani wa theory ambao maswali yake yanakuwa yanajulikana let say kama 1000 ambayo yanaulizwa machache kutoka katika hayo. Hii itapunguza influence za vituoni na mtu akifeli harudishiwi ada ya mtihani ila anaweza rudia mpaka aseme sasa basi.

  3. Traffic police waondolewe katika kuwafanyia watu testing, kiundwe kikosi maalum cha training Police wao kazi yao iwe ni enforcement tu, kazi ya kutoa leseni waiachie kitengo kitakachokuwa kinajulikana kama " Tanzania Drivers and car registration Agency" Chini ya wizara ya mambo ya ndani kikiwa linked na TRA kwa ajili ya kukusanya malipo yote ya ada na kodi za magari kama TRL.

  4. Kila leseni ikitoka iwe imeambatana na number ya officer aliyemfanyia practical test driver huyo na kumpatia leseni, ili iwe kama monitoring control ya madereva na mtahini ili kama tutaona madereva wa mtahini fulani rate yao ni kubwa ya kufanya makosa barabarani basi sisi tunammulika huyo mtahini.

  5. Mtu yeyote atakaye kamatwa anaendesha gari ambalo hakuwekewa bima kuliendesha basi adhabu ya fine inaenda kwa mwenye gari na dereva muhusika anakatwa points automatic pale tu king'amuzi kikigundua Driver and car are not compatible. Hii itawondolea traffic police lawama kwani si wao ni system.


  Kama tutaweza kufanya haya ninaamini discipline barabarani itaongezeka na huenda ajali za kizembe zikapungua. Otherwise itakuwa ni sawa na kubadili shuka tu wakati kitanda ni kilekile na kunguni wake kibao.
   
 4. PingPong

  PingPong JF-Expert Member

  #4
  Oct 7, 2010
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 933
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 45
  Usishangae ukiambiwa hata hizo kompyuta bado hazijanunuliwa...:roll:
   
 5. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #5
  Oct 8, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Mkuu Hosstede umegusa hoja za msingi sana kuhusu uthibiti wa ajali za barabarani.

  Sina hakika iwapo TRA na Jeshi la poilsi wanafanya kazi kwa msingi unaofananana.

  Inasemekana kwa Askari wa Usalama barabarani, wakikamata gari bovu au limezidisha mzigo, kwao suluhisho ni kupewa kitu kidogo tu watairuhusu gari iendelee. Kwao masharti ya "road licence" au "road toll" ni ulaji mzuri.
   
 6. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #6
  Oct 8, 2010
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,344
  Trophy Points: 280
  Mkuu umesema kila kitu.
  Ninachoongezea hapa ni kuwa utoaji wa leseni ni sehemu tu ya suluhisho si suluhisho kamili. Kama walivyosema wenzangu, wenzetu wa nchi nyingine wamebana kila mahali [loophole] kuzuia rushwa, kuwawajibisha wahusika[ mkaguzi.mtoa leseni, na bima].
  Mfano, Leseni ya udereva ipo katika smart card, na mtu aki swipe anapata historia ya mwendeshaji. Mwajiri hawezi kumuajiri mtu mwenye leseni chafu kwasababu bima ya gari inaongezeka hata mara mbili au tatu. kwahiyo ukitaka kupata kazi ni lazima upeleke police abstract ambayo inapatikana katika kila kompyuta hata za vijijini. Pili dereva mwenye leseni chafu bima yake ni kubwa kuliko ya dereva safi,hakuna flat rate kama Tanzania. Tatu, bima ya dereva inategemea umri [young 18-25 ni kubwa sana], middle age 30-60 ni nzuri, seniors 65 above ni kubwa. Ukiwa na Familia inasadia bima kwavile upo responsible. Ukiwa professional unapata punguzo.
  Tatu,mtu akipata ajali mara ya kwanza anapata warning, mara ya pili leseni inafungiwa miezi 3, mara ya tatu leseni inafungiwa miaka miwili na akimaliza muda huo lazima aende driving school.
  Nne, faini kwa makosa ya barabarani hailipwi kwa cash, dereva anakwenda kulipia polisi au analetewa bill, kama asipolipa kwa muda fulani polisi wote wanataarifa zake kupitia leseni, akikamatwa adhabu yake ni afadhali asingekuwa na leseni.
  Tano, magari ya abiria kama mabasi, dereva anatakiwa awe na umri wa miaka 35+ na leseni yenye historia safi ya miaka 10.
  Sita, dereva aliyesababisha ajali na kuua huyo tena asahau kazi maana hata kama kosa si lake hakuna mwajiri atakayeweza kulipia bima ya gari atakalomkabidhi huyo mtu.
  Haya yote na yale waliyosema wenzangu, ndiyo yanaleta nidhamu, kiasi cha mtu kusimama kwenye taa saa 8 usiku akiwa peke yake. Camera zikikunasa unakatiza hovyo, mwezi unaofuata bima yako ni mara mbili, polisi watakutumia warning na kukupa probation period.
  Kwahiyo leseni zi- facilitate process ya usalama lakini zenyewe si jibu bila ya kuwa na machanganyiko wa mambo muhimu [other factors]
   
Loading...