makoye2009
JF-Expert Member
- Jun 12, 2009
- 2,638
- 1,218
Watanzania tufikie mahali tuambizane ukweli ili tupone.
Hakuna aliyetegemea kuwa kuna siku Watanzania wenzetu wanaoishi huko Msumbizi wangelifurushwa bila huduma kwa kisingizio cha kuingia kinyume cha sherianchini! Kuna Watanzania wamefukuzwa na wameishi huko tangu Msumbiji ipate Uhuru mnamo mwaka 1975 tarehe 25 June chini ya Uongozi wa Mwanamapinduzi Camarada Samora Moises Machel.
Ijulikane kwamba Uhuru wa Msumbiji usingewezekana bila ya Tanzania kuingilia kati chini ya Uongozi thabiti wa Baba wa Taifa Marehemu Baba wa Taifa, Mwl. J.K. Nyerere. Baada ya Uhuru urafiki wa Tanzania na Msumbiji uliitwa ni Urafiki na Udugu wa DAMU. Baba wa Taifa kwenye hotuba ya Uhuru wa Msumbiji aliweka wazi kuwa kuna Watanzania askari na raia walikufa kwa kuipigania Msumbiji. Watanzania maelfu kwa mamilioni walikuwa wanajitolea mpaka Damu ili ipelekwe kwenye Mapambano dhidi ya Majeshi ya Wareno wakisaidiwa na Jeshi la Makaburu wa Afrika Kusini.
Unaweza kusema leo Wana Msumbiji wamesahau wema na fadhila zilizofanywa na Watanzania chini ya Uongozi wa Baba wa Taifa. Swali linakuja kwani sasa? Tumekuwa na awamu 4 zote zilizopita hatukuwahi kusikia upuuzi huu wa Wanamsumbiji isipokuwa Awamu hii ya Tano ya Mhe. sana John Pombe Magufuli. Kwanini Awamu ya 5 na siiwe awamu zilizopita??Hapa iko shida!!!
Shida yenyewe ni Mkuu wa Kaya. Tangu ameingia Ikulu mkuu wa kaya hahagaiki na Maswala ya nchi za kigeni kwa maana ya majirani zaidi ya Kenya, Uganda, Rwanda na Ethipia. Lakini pia Mkulu bado hajawahi kukanyaga nchi hata moja iwe ya Ulaya, Asia wala Marekani. Hili Kidiplomasia ya Kimataifa ni tatizo kubwa na linaweza kusababisha madhara makubwa kiuchumi, Kisiasa na Kijamii. Sina hakika kama hapo Msumbiji wana fahamu Rais wa Nchi iliyowasaidia kujikomboa anaitwa nani.
Mkuu wetu JPM yuko bize na Wapinzani tu. Kila siku ni kuagiza Mapolisi wawakamate wapinzani na kuwatia ndani pasipo na dhamana. Hata hii longolongo ya Makonda ya kudai kupambana na Madawa ya kulevya ni kchaka tu cha kujificha lakini walengwa wakubwa ni WAPINZANI. Nchi paka sasa hivi Uchumi umetetereka, Nchi haina chakula, Miradi ya maendeleo imesimama kwa vile Bajeti ya 2016/7 ya 21.9 Trilioni haitekelezeki. Bunge jlililoshia jniuzi wamesema ni asilimia kama 20(20%) imeweza kutekelezeka na mwaka unaishia Mei. Mkulu anaendelea na wimbo wake wa Hapa Kazi Tu huku akilazimisha Kuinyoosha nchi bila ya kufuata Katiba na Sheria!!!
Ni wakati sasa kwa JPM kutafakari na kubadilisha mwelekeo wa kisiasa kuanzia ndani nchi na nje ya Nchi ili kuondoa matatizo yanayoendelea kulikumba Taifa letu. Bila ya kufanya hivo Tanzania itaendelea kushuhudia Janga mojabaada ya Jingine. Biblia Takatifu imesema Mithali:''
"USIONDOE ALAMA YA MIPAKA YA ZAMANI ILIYOWEKWA NA WAZEE WAKO''
Mithali 22:28.
Rais Magufuli ameamua kungoa alama za mipaka yote ya zamani iliyoachwa na Wazee wetu kina Nyerere, Karume, Mwinyi, Mkapa na Kikwete. Tunaelekea wapi?