Chanzo cha Watanzania kufukuzwa Msumbiji ni utawala wa Awamu ya 5?

Wee mpuuzi kweli........Sasa heading yako mbna haiendani na ulichoandika.......Wakati mwingne ebu tafuteni kazi za kufanya......Hii kila siku MAGUFULI midomoni mwenu itawaathiri sana maisha yenu.....na ndio kwanza ni mwaka mmoja......

Wapuuzi ni waliozaa Kibstec! Kuna shida gani kumjibu bila kumuita mpuuzi? Huyu Rais ni baba yako, ni kuwa hujitambui tu
 
Watanzania tufikie mahali tuambizane ukweli ili tupone.
Hakuna aliyetegemea kuwa kuna siku Watanzania wenzetu wanaoishi huko Msumbizi wangelifurushwa bila huduma kwa kisingizio cha kuingia kinyume cha sherianchini! Kuna Watanzania wamefukuzwa na wameishi huko tangu Msumbiji ipate Uhuru mnamo mwaka 1975 tarehe 25 June chini ya Uongozi wa Mwanamapinduzi Camarada Samora Moises Machel.

Ijulikane kwamba Uhuru wa Msumbiji usingewezekana bila ya Tanzania kuingilia kati chini ya Uongozi thabiti wa Baba wa Taifa Marehemu Baba wa Taifa, Mwl. J.K. Nyerere. Baada ya Uhuru urafiki wa Tanzania na Msumbiji uliitwa ni Urafiki na Udugu wa DAMU. Baba wa Taifa kwenye hotuba ya Uhuru wa Msumbiji aliweka wazi kuwa kuna Watanzania askari na raia walikufa kwa kuipigania Msumbiji. Watanzania maelfu kwa mamilioni walikuwa wanajitolea mpaka Damu ili ipelekwe kwenye Mapambano dhidi ya Majeshi ya Wareno wakisaidiwa na Jeshi la Makaburu wa Afrika Kusini.

Unaweza kusema leo Wana Msumbiji wamesahau wema na fadhila zilizofanywa na Watanzania chini ya Uongozi wa Baba wa Taifa. Swali linakuja kwani sasa? Tumekuwa na awamu 4 zote zilizopita hatukuwahi kusikia upuuzi huu wa Wanamsumbiji isipokuwa Awamu hii ya Tano ya Mhe. sana John Pombe Magufuli. Kwanini Awamu ya 5 na siiwe awamu zilizopita??Hapa iko shida!!!

Shida yenyewe ni Mkuu wa Kaya. Tangu ameingia Ikulu mkuu wa kaya hahagaiki na Maswala ya nchi za kigeni kwa maana ya majirani zaidi ya Kenya, Uganda, Rwanda na Ethipia. Lakini pia Mkulu bado hajawahi kukanyaga nchi hata moja iwe ya Ulaya, Asia wala Marekani. Hili Kidiplomasia ya Kimataifa ni tatizo kubwa na linaweza kusababisha madhara makubwa kiuchumi, Kisiasa na Kijamii. Sina hakika kama hapo Msumbiji wana fahamu Rais wa Nchi iliyowasaidia kujikomboa anaitwa nani.

Mkuu wetu JPM yuko bize na Wapinzani tu. Kila siku ni kuagiza Mapolisi wawakamate wapinzani na kuwatia ndani pasipo na dhamana. Hata hii longolongo ya Makonda ya kudai kupambana na Madawa ya kulevya ni kchaka tu cha kujificha lakini walengwa wakubwa ni WAPINZANI. Nchi paka sasa hivi Uchumi umetetereka, Nchi haina chakula, Miradi ya maendeleo imesimama kwa vile Bajeti ya 2016/7 ya 21.9 Trilioni haitekelezeki. Bunge jlililoshia jniuzi wamesema ni asilimia kama 20(20%) imeweza kutekelezeka na mwaka unaishia Mei. Mkulu anaendelea na wimbo wake wa Hapa Kazi Tu huku akilazimisha Kuinyoosha nchi bila ya kufuata Katiba na Sheria!!!

Ni wakati sasa kwa JPM kutafakari na kubadilisha mwelekeo wa kisiasa kuanzia ndani nchi na nje ya Nchi ili kuondoa matatizo yanayoendelea kulikumba Taifa letu. Bila ya kufanya hivo Tanzania itaendelea kushuhudia Janga mojabaada ya Jingine. Biblia Takatifu imesema Mithali:''
"USIONDOE ALAMA YA MIPAKA YA ZAMANI ILIYOWEKWA NA WAZEE WAKO''
Mithali 22:28.

Rais Magufuli ameamua kungoa alama za mipaka yote ya zamani iliyoachwa na Wazee wetu kina Nyerere, Karume, Mwinyi, Mkapa na Kikwete. Tunaelekea wapi?
Sitoshangaa siku utakapo shindwa kumuweka mimba mkeo halafu utakuja kusema sababu ni Magufuli.
Nani alikwambia ni watanzania pekee yao ndio wameondolewa?
 
Nyie wadau sie Tz mbona tuliwafukuza wahamiaji haramu wa Nyarwanda/warundi ambao walisha zaliana mpaka wajukuu mkuki kwa ngurue kwa binadamu mchungu wacha wawafukuze
 
Wee mpuuzi kweli........Sasa heading yako mbna haiendani na ulichoandika.......Wakati mwingne ebu tafuteni kazi za kufanya......Hii kila siku MAGUFULI midomoni mwenu itawaathiri sana maisha yenu.....na ndio kwanza ni mwaka mmoja......
Tatizo lako umezibwa sehemu zako zote za ufahamu na tambala la kijani, tulioelewa tumeelewa.
 
Nionavyo ni lazima kutakuwa na tatizo kubwa sana ambalo mimi na wewe hatufahamu. Tujiulize ina maana kwa miaka yote waliokaa huko Msumbiji je ni leo wameona hawana vibali au wamekiuka sheria za uhamiaji? Je Rais Mpya wa msumbiji kwani kachaguliwa juzi kama trump? Sasa tusubiri na Malawi na wale wa Trump!!! Ila ya Msimbiji ni kitu cha kukaa chini na kufikiria mno kwa kuwa hatuna uhasama nao kama say ilivyo malawi kuhusu ziwa nyasa. Kazi ipo ila ni fundisho kuwa jenga kwako ni maana zaidi kuliko sisi Watanzania tulivyosaidia ukombozi wa bara la Afrika hasa Msumbiji na Afrika ya Kusini lakini hakuna faida kabisa.
 
Kuna cku mtu atagombana na mkewe na sababu pia atatupiwa magufuli, hivi kweli kutoka moyoni unaaminishwa kabisa lowasa ndo atakua muarobaini wako? Ama wa tz aloturoga kafa.
hivi mtu unapateje ujasiri mkubwa wa kuandika vitu laini na visivyo na mashiko kabisa
Hujasomeka hata kidogo
Huu ni upuuzi. Awamu ya t inahusikaje hapo... Acha hizo pingu inakunyemelea
Anaza pipo bwana. Sasa ndiyo nini hiki ulichoki post!!!
Kuwa kipofu siyo lazima uwe umepofuka macho tu, AKILI nayo inaweza ikawa na upofu.

Kwa kifupi 'mtukufu' kwenye suala la DIPLOMASIA ni ZERO.
 
Kwani ilikuaje kwa wale RAIA wa Rwanda walioondolewa mkoani kagera na ngo'mbe zao tukachukua licha ya vilio vyao
 
Kama ungelikuwa mwanafunzi wa kidato cha nne na mimi niwe mwalimu wako lazima ningekurudisha darasa la tano .Capacity thinking yako iko chini sana kuliko ya siafu.
Watanzania tufikie mahali tuambizane ukweli ili tupone.
Hakuna aliyetegemea kuwa kuna siku Watanzania wenzetu wanaoishi huko Msumbizi wangelifurushwa bila huduma kwa kisingizio cha kuingia kinyume cha sherianchini! Kuna Watanzania wamefukuzwa na wameishi huko tangu Msumbiji ipate Uhuru mnamo mwaka 1975 tarehe 25 June chini ya Uongozi wa Mwanamapinduzi Camarada Samora Moises Machel.

Ijulikane kwamba Uhuru wa Msumbiji usingewezekana bila ya Tanzania kuingilia kati chini ya Uongozi thabiti wa Baba wa Taifa Marehemu Baba wa Taifa, Mwl. J.K. Nyerere. Baada ya Uhuru urafiki wa Tanzania na Msumbiji uliitwa ni Urafiki na Udugu wa DAMU. Baba wa Taifa kwenye hotuba ya Uhuru wa Msumbiji aliweka wazi kuwa kuna Watanzania askari na raia walikufa kwa kuipigania Msumbiji. Watanzania maelfu kwa mamilioni walikuwa wanajitolea mpaka Damu ili ipelekwe kwenye Mapambano dhidi ya Majeshi ya Wareno wakisaidiwa na Jeshi la Makaburu wa Afrika Kusini.

Unaweza kusema leo Wana Msumbiji wamesahau wema na fadhila zilizofanywa na Watanzania chini ya Uongozi wa Baba wa Taifa. Swali linakuja kwani sasa? Tumekuwa na awamu 4 zote zilizopita hatukuwahi kusikia upuuzi huu wa Wanamsumbiji isipokuwa Awamu hii ya Tano ya Mhe. sana John Pombe Magufuli. Kwanini Awamu ya 5 na siiwe awamu zilizopita??Hapa iko shida!!!

Shida yenyewe ni Mkuu wa Kaya. Tangu ameingia Ikulu mkuu wa kaya hahagaiki na Maswala ya nchi za kigeni kwa maana ya majirani zaidi ya Kenya, Uganda, Rwanda na Ethipia. Lakini pia Mkulu bado hajawahi kukanyaga nchi hata moja iwe ya Ulaya, Asia wala Marekani. Hili Kidiplomasia ya Kimataifa ni tatizo kubwa na linaweza kusababisha madhara makubwa kiuchumi, Kisiasa na Kijamii. Sina hakika kama hapo Msumbiji wana fahamu Rais wa Nchi iliyowasaidia kujikomboa anaitwa nani.

Mkuu wetu JPM yuko bize na Wapinzani tu. Kila siku ni kuagiza Mapolisi wawakamate wapinzani na kuwatia ndani pasipo na dhamana. Hata hii longolongo ya Makonda ya kudai kupambana na Madawa ya kulevya ni kchaka tu cha kujificha lakini walengwa wakubwa ni WAPINZANI. Nchi paka sasa hivi Uchumi umetetereka, Nchi haina chakula, Miradi ya maendeleo imesimama kwa vile Bajeti ya 2016/7 ya 21.9 Trilioni haitekelezeki. Bunge jlililoshia jniuzi wamesema ni asilimia kama 20(20%) imeweza kutekelezeka na mwaka unaishia Mei. Mkulu anaendelea na wimbo wake wa Hapa Kazi Tu huku akilazimisha Kuinyoosha nchi bila ya kufuata Katiba na Sheria!!!

Ni wakati sasa kwa JPM kutafakari na kubadilisha mwelekeo wa kisiasa kuanzia ndani nchi na nje ya Nchi ili kuondoa matatizo yanayoendelea kulikumba Taifa letu. Bila ya kufanya hivo Tanzania itaendelea kushuhudia Janga mojabaada ya Jingine. Biblia Takatifu imesema Mithali:''
"USIONDOE ALAMA YA MIPAKA YA ZAMANI ILIYOWEKWA NA WAZEE WAKO''
Mithali 22:28.

Rais Magufuli ameamua kungoa alama za mipaka yote ya zamani iliyoachwa na Wazee wetu kina Nyerere, Karume, Mwinyi, Mkapa na Kikwete. Tunaelekea wapi?
 
Ni roho mbaya tu ya wanamsumbiji ndiyo iliyowafanya wakawafukuza watanzania wala serekali ya awamu 5 haihusiki,serekali ya awamu ya 5 ingekuwa na matatizo na watu wa msumbiji wasingewafanyia watanzania unyama kama huu,wangekumbuka fadhila walizofanyiwa na watanzania wangeweza kuwasamehe ukizingatia kuwa wananchi hawakuwa na makosa yoyote kama kulikuwa na makosa,makosa yalikuwa ni ya serekali ya awamu ya 5,makosa ambayo hayakupaswa kukubeshwa mwananchi wa kawaida.
 
Back
Top Bottom