Chanzo cha wanaume kufa mapema

Chanzo cha wanaume kufa mapema

Shida ni kuwa baba zetu mnakuwa wakali kama mbogo huku utotoni so lazima mkimbiwe.

Mfano unahitaji shati la shule, madaftari, kalamu viatu na soksi, sasa ili umwambie mzee hivyo vyote ubajipanga balaaaa namna ya kufikisha pia jinsi ya kuukabili USO wake mkali.

Unamweleza hizo shida zako utaskia

"Maelezo mengi ya nini sema vinagharimu shilingi ngapi jumla?"

Mtoto unatoka hapo unajua fika baba siyo wa mastori wala Maelezo marefu hadi uzeeni.

So vingine baba zetu mnakwama sana kisa ukichwa cha nyumba.
 
Hakuna iyo research yako siyo sahihi wababa waliofiwa na wake zao ni wengi ila walishaoa wake wengine hivyo ugane umeondoka.

Kumbuka kuwafundisha wanawake waachee kumwaga sumu kwa watoto kuwa baba ni mbaya kisa ana kamchepuko kamoja utamkuta mama ana huzuni watoto tukiwa wadogo ukimuuliza mama nini shida babaako amewasahau anaangaika na wanawakee hata hiyo shulee unayosoma hukustahili ungesoma Ulaya wewe hela zotee kwa Mwajuma ndalandefuu ww unazani ukiwa mkubwa iyo sumu itatoka kwa dawa gani.

N:B-WANAUME USIEKEZE NGUVU ZAKO ZOTE KWA WATOTO KUMBUKA KUJIWEKEZEA KWA FAIDA YAKO YA UZEENI SBB HAKUNA MKATABA KUWA UTAKUJA KULIPWA NA KUTUNZWA ILA UKIWA NA UWEZO HESHIMA UTAENDELEA KUPEWA TU HATA YA KINAFIKI SBB WANAJUA WAKILETA UJINGA HAO NA MAMA YAO UNAOA MWINGINE ATAKAEKUHESHIMU KAMA NA MTAKULA MTATIBIWA BILA KUWASUMBUA KUMALIZIA HELA KWA WATOTO SIYO UWEKEZAJI
 
Hajui alicho maanisha
Ungemwelesha kuwa

Mgane-mwanamme aliyefiwa na mke

Mjane-Mwanammke aliyefiwa na mume.

Kujigamba kuwa hajuichochote inahalalisha na wewe hujui kitu, maana mwenye kujua maana husema maana. Na asiyesema maana hajui maana kwa kuwa hana maana yoyote Bali majigambo ya nyani ktk shamba ila mahindi.
 
Nikiwa mdogo niliona wababa wengi wanakufa mapema nikauliza wakubwa why? Nikaambiwa jibu lipo kwa Bible in proverbs chapter 5.
 
Mmh!! JF ni zaidi ya chuo asee,, madini yaliyopo huku ni nondo za kupata u-professor wa tz
 
Baba anapokuwa bado ana nguvu, yuko kazini huwa anakua na nguvu na ushawishi mkubwa sana kwenye familia yake, familia humsikiliza, huzingatia uwepo wake!

Tatizo huanza pale baba anapozeeka, nguvu za uzalishaji mali zimekwisha, amestaafu! Na pale watoto wanapokua wamekua watu wazima wameanza maisha yao! Hapo ndipo mambo kwa baba humgeuka!

Mkewe huanza kumchukulia poa! Ile heshima aliyokuwa akipewa huanza kupungua taratiib.. baba hasikilizwi tena Kama zamani, isitoshe anakua hahusishwi sana tena kwenye mambo ya mkewe sababu hata akiambiwa atasaidia nini na pesa hana? Badala yake mkewe huanza kuwafanya watoto kuwa washirika wake zaidi na kumuweka kando mumewe. Baba anaachwa pembeni!

Mama huanza safari kwenda kwa watoto, huko hukaa sana, baba kaachwa nyumbani peke yake! Watoto wanagombea mama aende kwao, lkn baba hakuna anayemtaka!

Wakiwa nyumbani na mkewe, simu toka kwa watoto 80% anapigiwa mama, baada ya maongez mareefu, ndo baba anapewa simu anasalimiwa dk 2 imeisha hiyo! Baba simu anayo, ila haoni simu za watoto wakimpigia, na wakimpigia ni kwa sababu maalumu tena maongez huwa mafupi! Hawana muda nae!

Baba anajikuta anakuwa mpweke sana, anakua mgeni kwa familia yake mwenyewe! Wale ambao alizimalizia nguvu zake za ujana kuwatafutia hawana muda nae!

Pale baba anapokuwa anaihitaji sana faraja ya familia yake sababu ameshazeeka... Familia humpa kisogo! Upweke unamsonga! Sababu ya upweke mawazo humsonga, hili hupelekea kinga ya mwili kushuka na kufanya iwe rahisi kushambuliwa na magonjwa na haichukui muda anafariki!

Familia wataliaa, watachapisha matisheti, watatoa mapesa kumnunulia sanduku la gharama na kumjengea kaburi la gharama, mitandaoni watampost sana! Lakini alipokuwa hai. No one cares!

Tuwajali baba zetu, walijitoa na kujinyima sana kufanya tufike tuliko! Ni dhambi mbele za Mungu tena ni laana mbaya kuwapuuza baba zetu!

Wakati unaendelea kumsifia mama yako kuwa ni bora,msifie hata baba kwa kukuchagulia mama aliye bora.Mwanaume unamtumia mama laki moja baba anatumiwa elfu tano hivyo unapoka madaraka ya baba nyumbani maana mwenye pesa ndiye mwenye mamlaka. Baba anaambiwa usipotii hutakula umesahau nawe ni mwanaume yatakukuta kama hayo.

Copied & Posted
FB_IMG_1617162463931.jpg
 
 
Baba anapokuwa bado ana nguvu, yuko kazini huwa anakua na nguvu na ushawishi mkubwa sana kwenye familia yake, familia humsikiliza, huzingatia uwepo wake!...
Women are Human Beings. They are valued for who they are.

Men are Human Doings. They are valued for what they do.

Many men realize it too late in their lives. It was not them men who were valued. It was what they brought to the table that was valued.

The second them men stopped bringing something that was valued, that very second them men were made aware they were disposable. To many men that is heartbreaking.

What them men do with the heartbreak, differ from one man to another. Some of them men go through some psychosis, and eventually die. Some other men, lose the meaning of life, and they wish they were dead, and welcome death with open hands.

That my friend, is one of the main reasons why men die early.
 
Back
Top Bottom