Chanzo cha uovu wote

Chanzo cha uovu wote

Afadhali hujasema KE ndo chanzo! :wacko:
 
Mwanamke kiumbe dhaifu chanzo cha yote.

Sidhani hapo ni kumuonea tu mwanamke hata kama Hawa aldaganywa kwanini Adamu alikubali na wakati alikua wa kwanza kuubwa na alionywa na Mungu all in all hakuna asiye mdhaifu
 
Mkuu Eiyer sidhani kama kujua ni chanzo cha uovu, kwasababu uovu haujaanza na mwanadamu, kwa maana nyingine uovu ninaweza nikasema ni dhambi, Kutokana na shughuli za shetani katika bustani ya Edeni inaonekana dhambi ilikuwepo ulimwenguni kabla Adamu na Hawa hawajatenda dhambi...

Tukirudi katika Biblia haielezi dhambi ilivyoanza katika asili yake, inaelezewa jinsi ilivyoingia kwa wanadamu, Mungu alipowapa wanadamu ulimwengu ulioumbwa aliweka mpaka, kwasababu uhuru kamili usingelingana na hali ya mwanadamu ya kuwa mfano wa Mungu

Mwanzo 2:15-17

15 Bwana Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza.
16 Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula,
17 walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.

Lakini mwanadamu alivuka mpaka Mungu aliomuwekea hivyo aliangukia katika dhambi, Alitaka kutawala maisha yake mbali na Mungu na kuwa mwamuzi wa mwisho kuhusu mambo yaliyo mema na Mabaya Mwanzo 3:1-6

Kiburi kilikuwa kiini cha dhambi ya mwanadamu, Warumi 1:21-23

21 kwa sababu, walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza.
22 Wakijinena kuwa wenye hekima walipumbazika;
23 wakaubadili utukufu wa Mungu asiye na uharibifu kwa mfano wa sura ya binadamu aliye na uharibifu, na ya ndege, na ya wanyama, na ya vitambaavyo.

1 Yohana 2:16 Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.

Isaya 10:15 Je! Shoka lijisifu juu yake alitumiaye? Je! Msumeno ujitukuze juu yake auvutaye? Ingekuwa kana kwamba bakora ingewatikisa waiinuao, au fimbo ingemwinua yeye ambaye si mti.

Obadia 1:3 Kiburi cha moyo wako kimekudanganya, Wewe ukaaye katika pango za majabali, Mwenye makao yako juu sana; Asemaye moyoni, Ni nani atakayenishusha mimi?

Dhambi ya mwanadamu ilianza moyoni mwake mwenyewe, tendo la kutotii lilikuwa matokeo yake

Mithali 4:23 Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.

Yeremia 17:9 Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; nani awezaye kuujua?

Marko 7:21-23

21 Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati,
22 wivi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu.
23 Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi.

Kwa hiyo kwa muktadha huo tunaweza tukasema chanzo cha uovu tunaweza tukasema ni kiburi, ni chombo ambacho shetani alikitumia na kufaulu alipomjaribu mwanadamu ili amwasi mwumbaji wake Mwanzo 3:1-6

Mithali 16:18 Kiburi hutangulia uangamivu; Na roho yenye kutakabari hutangulia maanguko.

Danieli 5:20 Lakini moyo wake ulipoinuliwa, na roho yake ilipokuwa ngumu akatenda kwa kiburi, aliuzuliwa katika kiti chake cha enzi, nao wakamwondolea utukufu wake.

Kiini cha kiburi ni ubinafsi, furaha ya mwenye kiburi siyo kuwa na kitu fulani tu, bali kupata zaidi kuliko watu wengine, kuwa bora zaidi kuliko watu wengine, Kiburi pia ni dhambi aichukiayo Mungu

Mithali 8:13 Kumcha Bwana ni kuchukia uovu; Kiburi na majivuno, na njia mbovu, Na kinywa cha ukaidi pia nakichukia.

Mithali 16:5 Kila mwenye moyo wa kiburi ni chukizo kwa Bwana; Hakika, hatakosa adhabu.

kwa hiyo ukijaribu kuangalia kwa undani zaidi chanzo cha uovu hakitokani na mwanadamu, lakini mwanadamu ameukuta uovu tayari upo, kwa hiyo kujua sidhani kama ni chanzo cha uovu, chanzo cha uovu kwa maana nyingine kinatokana na shetani, hata kule Edeni shetani ndio muhusika pia...
 
Last edited by a moderator:
Mkuu wangu Eiyer, asante kwa mwaliko wako. Na nianze kwa kusema, binafsi napingana na mtazamo wako ulioutoa katika post namba 1, chanzo cha dhambi si KUJUA, maana kama ni ufahamu mwanadamu alikuwa nao kabla hata ya kutenda dhambi. Maana, hata kabla ya kula tunda, Adamu alipoletewa mke, alimtambua kwa kusema kuwa alikuwa nyama katika nyama zake, pia alijua kuhusu nini Mungu alimhitaji kufanya. Kumbe kilichosababisha uovu ni hiki.
1. Kutokutii agizo la Mungu.
2. UDADISI na hii ndiyo ilizaa utovu wa agizo la Mungu, kivipi hii?. Hebu fikilia, Hawa kilichompitisha karibu na mti wa ujuzi wa mema na mabaya ni kipi kama sio kutka kuchunguza siri iliyopo katika mti huo. Ingawa pia, hoja yako yaweza kuwa na mashiko kiasi chake, maana kupitia UDADISI, unapata kujua kitu. kwa hiyo KUJUA hakuji pasipo kuwepo utafiti au udadisi wa suala husika. Mfano, kama kuna ugonjwa wa mlipuko katika eneo flani, ugonjwa hauwezi kufahamika kama hakuna utafiti wa kisayansi, kwa hiyo UTAFITI/UDADISI hutangulia KUJUA.
 
Last edited by a moderator:
Sidhani hapo ni kumuonea tu mwanamke hata kama Hawa aldaganywa kwanini Adamu alikubali na wakati alikua wa kwanza kuubwa na alionywa na Mungu all in all hakuna asiye mdhaifu
Mtu mmoja alimwambia mchungaji wakiwa kanisani(lakini si katika siku ya ibada) kuwa HAWA alikuwa mjinga, na laiti angekuwa yey, asingemkubalia nyoka katika ushawishi wake. Mchungaji alipomaliza kumsikiliza, akatoa agizo kwa kuacha karatasi aliyoikunja vizuri na kuiweka juu ya meza, na yule mjamaa akaambiwa asiifungue karatasi. Mchungaji aliondoka, akaenda ofisini kwake, na yule jamaa akatamani sana kujua ni kwa nini mchungaji amemwambia asifungue karatasi ile, ndipo baadaye aliifungua. mchungaji aliporudi alikuta kanisa limesafishwa vizuri sana, ndipo alipouliza ni nani kafanya ule usafi, jamaa akasema ni yeye. kumbe karatasi hiyo ilikuwa na maagizo ya kusafisha kanisa, na ndipo mchungaji akamwambia kuwa, kwa kuwa hajatii kile amemwambia, kumbe hata angekuwa yeye pale bustanini(Eden) angekula, maana tayari amekiuka agizo la mchungaji kwa kutaka KUDADISI ni nini hasa ameandika katika karatasi ile. Leo hii fikiria hili, vitu vyote ambavyo Mungu kasema visiguswe ndivyo vinavyopendwa sana, mfano uzinzi, nguruwe, pombe na mengine mengi, lakini naamani watu hawakuanza kupenda hivi hivi tu pasipo mmoja wapo kutaka kudadisi kutaka kujua kilicho ndani ya katazo. Hata wewe unayesoma, fikiria ni nini kilikupelekea kwa mfano ukaanza ngono kabla ya ndoa(kama ulifanya hivyo). Kwa hiyo kila binadamu wa leo na walioishi zamani, tunashawishika kutenda dhambi, kupitia yafuatayo.
1. Udadisi wa kutaka kujua kilicho ndani ya katazo.
2. Ushauri uliojaa ubembelezi mwingi katika kufanikisha udadisi huo(rejea Hawa alivyoshauriwa na nyoka)
3. Nyingine utamalizia mwenyewe ewe ndugu msomaji.
 
Back
Top Bottom