Twende taratibu kidogo pia mkuu tukiwa na lengo la kuelimishana.
1. Mungu alimwambia Ibrah uzao wako ndio utakuwa urithi wako. Agano Mungu alifunga na Ibrahim lakini agano lile lilihusu mtoto atakayetoka kwenye mauno ya Ibrahim, walifahamu hivyo.
2. Ishmael anazaliwa, Ishmael ni mtoto wa Ibrahim kupita mjakazi wake, na sio mkewe halali Sara ambaye Mungu ndie alimtambua kama mke wa Ibrahim.
Baadae Mungu anamwambia Ibrahim, mtoto atakayetoka kwenye tumbo la Sara ndie atakayekurithi. Kumbuka Mungu alikuwa anatengeneza kizazi cha Utumishi(kiroho) kwahiyo ilipaswa kuwa ni lazima mtoto asiwe kwenye hatia ya aina yoyote ile.
3. Baada ya mafarakano baina ya Sara na yule mjakazi alozaa na Ibrahim, Hajir anafukuzwa na mwanae Ibrahim, kwa kuwa Ishmael ndio uzao wa kwanza wa Ibrahim, na uzao wowote wa kwanza unakuwa ni lango na ulimwengu wa roho wa nuru na giza unautambua vizuri mzaliwa wa kwanza, Mungu anambariki kwa Baraka za mwilini Ishmael. Lile kusudi la Mungu, Spiritual matters, Mungu alikusudia zipite kwa mtoto ambaye atazaliwa baina ya Ibrahim na Sara.
4. Hajiri akafukuzwa na mwanae, akapewa mali nyingi sana kutoka kwa Ibrahim, akaenda zake.
Moja ya vitu ambavyo vinamkanganyiko baina ya watu hawa ni hivi, kwanini Ishmael apewe Urithi mapema ikiwa bado baba yupo hai? Urithi una nguvu endapo mtu akawa amefariki. Kumpa Urithi kwa wakat ule, maana yake ni kwamba mimi na wewe ndo basi tena. Hakuna ushirika, agano au muunganiko wowote baina yetu.
Ishmael na kizazi chake ndiko kwenye misingi ya dini ya Kiislamu, na kwa Isaka mtoto wa Ibrahim na Sarah ndipo msingi wa Ukristo ulipoanzia.
Sasa sikiliza, wakati Ibrahim akiwa Mlima Moriah kama sikosei, Mungu alimwambia Ibrahim, uzao wako utamiliki malango ya adui zako. Kwa tafsir ya kawaida, uzao wa Ibrahim hautashindwa na maadui zake kamwe. Ile vita iliyoinuka ya Ishmael na uzao wake dhidi ya Isaka na uzao wake, uzao wa Ishmael hautakuja kushindwa kamwe. Hili ni agano ambalo Mungu alifunga na Ibrahim.
Uzao wa Ibrahim kwa Sara una baraka, uzao wa Ibrahim na Hajiri una mafanikio. Unaweza ukawa na mafanikio na usiwe na Baraka ila ukiwa na Baraka, mafanikio utakuwa nayo.
MUNGU ANAMWAMBIA IBRAHIM ATAKAYEMLITHI ATATOKA KATIKA VIUNO VYAKE
Mwanzo 15:3
Abramu akasema, Tazama, hukunipa uzao, na mtu aliyezaliwa nyumbani mwangu ndiye mrithi wangu.
Mwanzo 15:4
Nalo neno la Bwana likamjia likinena, Huyu hatakurithi, bali atakayetoka katika viuno vyako ndiye atakayekurithi.
ISHMAEL NDIO MTOTO WA VIUNO WA IBRAHIM
Mwanzo 16:3
Sarai mkewe Abramu akamtwaa Hajiri Mmisri mjakazi wake, baada ya kukaa Abramu katika nchi ya Kanaani miaka kumi, akampa Abramu mumewe, awe mkewe.
Mwanzo 16:4
Basi akamwingilia Hajiri, naye akapata mimba. Naye alipoona ya kwamba amepata mimba, bibi yake alikuwa duni machoni pake.
MUNGU ANAAHIDI BARAKA KWA ISHMAEL
Mwanzo 16:11
Malaika wa Bwana akamwambia, Tazama! Wewe una mimba, utazaa mwana wa kiume, nawe utamwita jina lake Ishmaeli, maana Bwana amesikia kilio cha mateso yako.
Mwanzo 16:12
Naye atakuwa kama punda-mwitu kati ya watu, mkono wake utakuwa juu ya watu wote na mkono wa watu wote utakuwa juu yake, naye atakaa mbele yao ndugu zake wote.
UZAO WA ISHMAEL
Mwanzo 25:12
Hivi ndivyo vizazi vya Ishmaeli, mwana wa Ibrahimu, ambaye Hajiri, Mmisri, mjakazi wa Sara, alimzalia Ibrahimu.
Mwanzo 25:13
Na haya ndiyo majina ya wana wa Ishmaeli, kwa majina yao, na kwa vizazi vyao. Mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli, ni Nebayothi, na Kedari, na Abdeeli, na Mibsamu,
Mwanzo 25:14
na Mishma, na Duma, na Masa,
Mwanzo 25:15
na Hadadi, na Tema, na Yeturi, na Nafishi, na Kedema.
Mwanzo 25:16
Hao ndio wana wa Ishmaeli, na hayo ni majina yao, katika miji yao, na katika vituo vyao, maseyidi kumi na wawili kwa kufuata jamaa zao.
ARABUNI
Isaya 21:13
Ufunuo juu ya Arabuni. Ndani ya msitu wa Arabuni mtalala, Enyi misafara ya Wadedani.
Isaya 21:14
Waleteeni wenye kiu maji, Enyi wenyeji wa nchi ya Tema; Nendeni kuwalaki wakimbiao na chakula chao.
Isaya 21:16
Kwa sababu Bwana ameniambia hivi, Katika muda wa mwaka, kama miaka ya mtu mwenye kuajiriwa, utaangamia utukufu wote wa Kedari.