Chanzo cha mvutano kati ya USA na North Korea

Rasi ya Korea ilikuwa koloni la Japan kuanzia 1910 hadi mwaka 1945. 1945 kwenye mwisho wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia jeshi la Urusi liliwafuata Wajapani kaskazini mwa rasi na Wamarekani waliingia kusini. Korea ikagawiwa.

Mwanzoni kulikuwa na majadiliano ya kuunganisha Korea tena lakini Vita Baridi ilileta uadui kati ya pande hizo mbili. Kila moja ilianzisha serikali ya pekee katika kanda la utawala wake kufuatana na itikadi yake. Warusi walitaifisha tasnia na ardhi wakaacha serikali ya kikomunisti katika kaskazini na Wamarekani waliacha uchumi wa kibepari na serikali iliyochaguliwa katika kusini. Kila upande ulikandamiza vikali wafuasi wa itikadi ya kinyume.

Hapo mwanzo wa Korea Kaskazini (mwanzoni chini ya Warusi) na Korea Kusini (mwanzoni chini ya Marekani) waliokuwa maadui tangu mwanzo.

Mwaka 1950 dikteta wa kaskazini aliamua kuunganisha Korea kwa njia ya vita. Mwezi wa Mei 1950 jeshi la kaskazini lilivamia Korea ya Kusini likateka mji mkuu wa Seoul na kusukuma watetezi hadi kusini ya rasi ya Korea.

30 Julai 1950 Baraza la Usalama la UM iliamua kuingilia kijeshi dhidi ya uvamizi kutoka Korea Kaskazini. Azimio hii lilipita kwa sababu Umoja wa Kisovyeti (=Warusi) hukuhudhuria kikao hivyo ulishindwa kupiga veto yake. Jeshi lililoingia kwa niaba ya Umoja wa Mataifa liliunganisha vikosi kutoka nchi 22, jumla askari 500,000 na wengi wao kutoka Marekani.

Vita iliendelea hadi 1953. Korea ya Kaskazini iliweza kudumu kwa sababu ya msaada wa kijeshi wa China iliyoleta askari milioni moja Korea. Katika vita hii watu wengi waliuawa na hasa kaskazini iliharibika sana . Si rahisi kutaja idada ya wahanga wote, lakini makadirio yanataja karibu milioni 4 watu raia na wanajeshi hadi milioni 1 pande zote mbili.

Soma hapa: Vita ya Korea - Wikipedia, kamusi elezo huru
 
Back
Top Bottom