chanzo cha mateso

Andrew Nyerere

JF-Expert Member
Nov 10, 2008
3,007
2,429
.ExternalClass .ecxhmmessage P{padding:0px;}.ExternalClass body.ecxhmmessage{font-size:10pt;font-family:Verdana;}

''Ni lazima tuendelee na hii mihadhara yetu '',alisema yule Mwalimu wa Kihindi halafu nitafurahi kurudi India ambako kuna maendeleo zaidi ya utamaduni.'' Akayapanga makaratasi yake mezani na akatutazama kwa wasiwasi kuona kama tunafuatilia,halafu akaendelea. '' Gautama katika safari zake alifikiria sana. Kwa miaka sita alisafiri,na kutumia karibu muda wake wote kutafuta Kweli,kuugundua ukweli,kutafuta maana nyuma ya maisha. Aliposafiri aliteseka kwa mambo mengi magumu,kukosa mahitaji ya msingi,ukata,njaa,na kati ya swali la kwanza alilouliza ni ''Kwa nini sina furaha?''

''Gautama alilifikiria hili swala sana,na jibu likamjia wakati wanyama wa porini walipokuwa wanamsaidia,konokono walipokuwa wanakipooza kichwa chake,ndege walipokuwa wanazipepea kope zake,na wengine wote wanakaa kimya ili asisumbuliwe. Aliamua kwamba zipo Kweli Nne Kubwa,ambazo aliziita Kweli Nne Tukufu,ambazo zilikuwa sheria ya kukaa kwa Binadamu hapa Duniani.
Kuzaliwa ni mateso,alisema Buddha. Mtoto anazaliwa kwa mama yake ,na kusababisha maumivu kwa mama na maumivu kwa mtoto,ni kwa maumivu tu ndio mtu anaweza kuzaliwa katika Dunia hii,na kitendo cha kuzaliwa kinasababisha maumivu na mateso kwa wengine. Kuzeeka ni mateso;na mtu anapozeeka na chembe chembe za mwili wake zinaposhindwa kujijenga upya kama mwanzo,ndipo uzee unapoanza,viungo havifanyi kazi kwa usahihi,mabadiliko yanatokea,na kuna mateso. Mtu hawezi kuzeeka bila mateso. Kuugua ni mateso;kiungo kinaposhindwa kufanya kazi kwa usahihi kunatokea maumivu,mateso,wakati hicho kiungo kinaulazimisha mwili kujirekebisha na hali hii mpya. Kifo ni mwisho wa mateso;kifo kinaleta mateso,siyo kitendo cha kufa chenyewe,lakini hali zinazoleta kifo chenyewe zinaleta mateso. Kwa hiyo,,tunakuwa hatuna furaha.
''Mateso yanasababishwa na kuwepo kwa vitu ambavyo tunavichukia. Tunakuwa katika hali ya kukosa furaha,ya kukata tamaa,tunapokuwa na wale ambao hatuwapendi;wakiwepo wale tunaowachukia. Tunakosa furaha tunapotengana na vitu ambavyo tunavipenda;tunapotengana na tunayempenda,kama,wakati mwingine, hatujui tutakuwa tena na mtu yule lini,hivyo tunateseka,tunakata tamaa,kwa hiyo tunakuwa hatuna furaha.
''Kutaka na kukosa kile tunachokitaka,hicho ndicho chanzo cha mateso,hicho ndicho chanzo cha kukosa furaha,chanzo cha huzuni. Kwa hiyo inakuwa tunakuwa na hamu na kitu lakini hatukipati,na badala yake tunateseka na tunakosa furaha. '' Kifo pekee kinaleta amani,kifo pekee kinaleta uhuru kutoka katika mateso. Kwa hiyo ni dhahiri kwamba kung'a ng'ania kuishi ndicho kinachotuletea mateso.,kung'ang'ania kuishi ndicho kinatufanya tusiwe na furaha.''

Yule Mwalimu wa Kihindi alitutazama,na kusema,''Buddha,Gautama wetu Mbarikiwa,hakuwa mtu menye kukatishwa tamaa,isipokuwa alikuwa anatazama hali ya mambo ilivyo halisi. Gautama alielewa kwamba mtu asipoielewa hali halisi hawezi kuyaondoa mateso. Mtu asipoelewa kwa nini kuna mateso hawezi kuendelea kwenye Njia ya Katikati.


Mafundisho yalisisitiza sana kuhusu mateso,nilifikiria;lakini nakumbuka njisi Kiongozi wangu mpendwa,Lama Mingyar Dondup alivyoniambia. Alisema,''Tuzingatie,Lobsang,alivyosema hasa Gautama. Hakusema kwamba kila kitu kinasababisha mateso. Hata kama imeandikwa nini katika Misahafu;hata kama Waaalimu Wakubwa wanasema nini,Gautama hakusema wakati wowote kwamba kila kitu ni mateso. Alivyosema hasa ni kwamba kila kitu kina uwezekano wa kuleta mateso,kwa hiyo ni lazima ieleweke vizuri kwamba kila tukio katika dunia linaweza kuishia katika maumivu,au kukosa raha kidogo,au kukosa muafaka. Linaweza! Haikuelezwa mahali popote kwamba ni lazima lisababishe maumivu.

Kuna kutoelewano kwingi kuhusu Watu Wakubwa walisema au hawakusema nini:Gautama alikuwa na imani kwamba mateso ,maumivu,ilikuwa siyo tu mateso ya mwili,au maumivu tu ya mwili. Alisisitiza kwamba mateso ya akili yanayosababishwa kuchanganyikiwa katika hisia [disfunction of the emotions]yalikuwa ni mateso makubwa zaidi,yenye uwezo mkubwa zaidi wa kuondoa muafaka,zaidi ya maumivu ya mwili tu au kukosa fauraha kwa mwili. Kama siishi kwa muafaka ni kwa sababu zijajifunza kuikubali dunia ilivyo,na faida zake na uwezekano wa kuteseka. Naweza tu kupata furaha kwa kuzielewa sababu za kuondoa furaha na kuzikwepa hizo sababu.
Nilikuwa nayafikiria mambo haya ,pia nafikria jinsi ile dawa ya miti shamba ilivyokuwa inaleta harufu sana,wakati yule Mwalimu wa Kihindi akaipinga tena ile meza yake ya kufundishia,na kusema,''Hii ndiyo Kweli ya kwanza ya zile Kweli Tukufu . Sasa tuijadili Kweli Tukufu ya Pili.

''Gautama alikuwa anawahubiria wafuasi wake,wale waliomuacha kwanza wakati msisimko ulipoondoka katika Mafundisho yake,lakini sasa walikuwa wafuasi wa Gautama tena. Aliwaamibia,''Nafundihsa mambo mawili tu,mateso na jinsi ya kuondokana na mateso. Sasa hii ndiyo Kweli Tukufu kuhusu chanzo cha mateso. Ni ile kiu inayosababisha kurudia kuishi;ni kiu inayoambatana na starehe za hisia na inatafuta kushibishwa mara hapa,mara pale. Inachukua umbo la hamu ya kutaka kuzishibisha hisia[the senses],au hamu ya kupata maendeleoa na vitu vya kidunia.''

'''' Kama tulivyofundishwa, mateso yanafuatia kitu ambacho tumekitenda vibaya,yanasababishwa na mtazamo ambao siyo sahihi kuhusu dunia. Dunia yenyewe sio mahali pabaya,lakini baadhi ya watu ndani yake wanafanya ionekane mbaya,na ni mtazamo wetu,makosa yetu,ambayo yanaifanya dunia ionekana mbaya sana. Kila mtu ana hamu,matamanio na ashiki za aina aina,ambazo zinamfanya mtu afanye mambo ambayo anapokuwa katika hali shwari zaidi na mantiki,wakati hana hizo hamu,matamanio,na ashiki za aina aina,asingefanya.
'' Mafundisho Makubwa ya Gautama ni kwamba yeyote mwenye matamanio hawezi kuwa huru,na yule ambaye hayuko huru hawezi kuwa na furaha. Kwa hiyo,kushinda tamaa ni kuchukua hatua kubwa kuelekea furaha.

''Gautama alifundisha kwamba kila mtu ni lazima ajitafutie furaha. Alisema kuna aina ya furaha ambayo haileti kutosheka,ni kitu cha kupita tu,hakidumu na ni aina ya furaha ambayo mtu anapata wakati anapotaka mabadiliko wakati wote,kila wakati anataka kwenda huko na huko kutazama sehemu mpya na kukutana na watu wapya. Hii ni furaha ambayo haidumu. Furaha ya kweli ni ile ambayo inaweza kumletea mtu kutosheka kwa kweli,ambayo inatoa pia roho uhuru kutokana na kutoridhika. Gautama alisema,''Wakati nilipokuwa nafuatilia furaha..nimegundua kwamba tabia mbaya zinatokea,na tabia nzuri zinapungua,basi aina hiyo ya furaha ni lazima ikwepwe. Wakati nafuatilia fuaraha na nikagundua kwamba tabia mbaya zinapungua na tabia nzuri zinatokea,aina hiyo ya furaha iendelezwe.''

''Sisi,kwa hiyo,ni lazima tuache kufukuzia vitu visivyo na maana vya mwili,vitu ambavyo havidumu mpaka katika dunia ijayo,tuache kujaribu kuzishibisha hamu ambazo zinakua kila tunavyozidi kuzililisha,na,badale yake,tufikrie tunatafuta nini hasa,na tunaweza kukipata vipi? Tufikirie kuhusu asili ya hamu zetu,chanzo cha hamu zetu,halafu tunaweza kutafuta kukiondoa hicho chanzo.''

Mwalimu wetu alikuwa analichangamkia somo lake. Alikuwa anasumbuliwa ,pia,na ile harufu ya miti shamba kwa sababu akasema,''Tutapumzika kidogo hapa kwa sababu sitaki kuzipa fatiki kubwa sana akili zenu ambazo nadhani hazina upeo mkubwa sana kama akili za wanafunzi wangu wa Kihindi.''
Akachukua makaratasi yake,akayaweka katika mkoba wake,kwa uangalifu akufunga mkoba,na akashikilia pumzi yake alivyonipita. Kwa muda mfupi wale watoto wengine wakakaa kwa utulivu wakisubiri hatua zake zififie alivyokua anaondoka. Halafu mmoja akanigeukia na kusema,'' Lobsang,kwa kweli unatoa harufu sana! Bila shaka ni kwa sababu unachanganyikana na mashetani,unaruka kwenda mbinguni pamoja nao..'' Nikajibu,kwa mantiki,''Sikiliza,kama nilikuwa nimechanganyikana na mashetani sikupaswa kuruka kwenda mbinguni pamoja nao,ila upande mwingine,na anavyofahamu kila mtu niliruka juu'' Tulitawanyika na kila mtu akaelekea kivyake. Nilkwenda dirishani,na kutazama kwa hamu,najiuliza Kiongozi wangu alikuwa anafanaya nini katika Lamasery ya Rose Fence,nikawa nafikiria huyu Mwalimu wa Kihindi ambaye namchukia sana ataondoka lini. Nikawa nafikiria kwamba kama yeye alikuwa muumini mzuri wa Kibudha kama alivyojitaswiri kuwa,angekuwa na uelewa mkubwa zaidi na hisia kwa watoto wadogo.
 
Back
Top Bottom