Chanzo cha maovu katika ndoa na mahusiano

Chanzo cha maovu katika ndoa na mahusiano

PCGAMES

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2013
Posts
802
Reaction score
1,192
Wanandoa na watarajia kuingia kwenye ndoa wameshindwa kutii miongozo ya imani zao ambazo zinatokana na Mungu, badala yake wanamsikiliza binadamu ambaye uwezo wake wa maono unaukomo.

Wauaji na wavurugaji wa kwanza wa ndoa na mahusiano ni wale wanaohamasisha kuishi kwa kujitenga wakati tayari ninyi ni mwili mmoja, kuna kauli ambazo zimekuwa zikifuatwa na kuwa kama miongozo halali na yenye busara kumbe inatengeneza sumu katika ndoa.

Kauli zenyewe ni kama vile wanandoa kutoshirikiana katika 'kushikiana simu', ni jambo ambalo linaonekana kuwa dogo kwa mtizamo wa kawaida lakini linamadhara makubwa. Unapoidhinisha jambo kama hili kwa wawili walioapa kushirikiana katika shida na raha ina maana kuwa unaenda kinyume na matakwa ya imani na matokeo yake yatakuwa mabaya kwa sababu umedharau maagizo ya Mungu.

Pia kuna mambo mengine kama kuhalalisha usawa wa kila jambo ndani ya ndoa ni kwenda kinyume na maagizo ya Mungu. "Mwanaume ampende mke wake na mwanamke amtii mme wake" haya ndio magizo la Mungu na si vinginevyo. Ukiingiza busara ya kibinadamu kama mambo ya haki sawa na kadhalika lazima kushindwa kutokee na ndipo matukio ya mauaji yanapozaliwa.

Binadamu turejee katika miongozo ya Mungu ambaye ndiye Muumba wetu maana Yeye ndiye aliyetupatia viwango maalum vya namna nzuri na bora ya kuishi, tusitegemee miongozo ya binadamu kwa maana mara nyingi ina akisi moja kwa moja kutoka kwa shetani.

Hivi kwa akili ya kawaida hatuwezi kujiuliza aliyesema wanandoa wasishirikishane simu alikuwa ana maanisha nini? Na baadhi wa wanandoa wanatii jambo baya kama hili ambalo lina akisi Uzinzi na Uasi ndani ya ndoa. Ndicho tulichoagizwa hadi tukaapa madhabahuni/ mbele za Mungu?. Tumepewa akili na Mungu ili tuweze kuchuja mema na mabaya, naomba Mungu atusaidie [emoji120]
 
Wenye akili ndogo hawataelewa hapa watakuja wamewakaa kwa fujo maana yapo kama ma agent ya uzinzi kwenye ndoa zao na ndoa za wengine kutwa kuanzisha miuzi ya uzinzi na wanaona ni kawaida

Kitu kingine unakuta mme mlevi na mke mlevi hapo unatarajia nini na walevi wanauzi wao wa kimasikhara
[emoji1][emoji1][emoji1]
 
Mimi nikuoe kwa kukulipia mahari kwenu alafu nisishike simu yako☹️

Hii hesabu mbona hata haikai vizuri
 
Sasa nini kifanyike mkuu. Maana lengo la kuonyana kutoshika simu ya mume au mke ni kuepusha mikwaruzano, disappointments zinazoweza kujitokeza. Mfano mkeo ana namba ya bodaboda na linamtaka kama kadhamiria mchizi atatuma mamessage ya ajabu tu. Mke labda atamblock. Wewe mume ukipita ukaona message shughuli..ukipita kwenye blocklist pia shughuli lazma utamuhisi mkeo vibaya....

Turudi kwa mke nae. Unakuta mume yuko na mipango yake, madili sijui biashara, kazini. Kote huko **** wanawake wengne. Unakuta kati yao walomzunguka kuna makurumbembe. Hayaoni shida kumtongoza mme wake. Na unakuta wana potential kimaendeleo sema tu ndo wanamtaka pia. Lazima wajitongozeshe. Mwanamke huyu akishika ile simu mara akutane na message za mahaba, ama mitongozo..au la picha za uchi za kumteka mume huyu.

Automatically ndo vita hutokea hapo. Sasa ili kuepusha haya ndo maana ikatokea hii warning maana lazima ilete mapishano ya lugha tu. Af mwishk wa siku ukute wote ni faithful. Hapa naongelea walio na uaminifu... Kimbembe kwa wale ambao ni wazinzi kweli.... Na hili nadhani lilisemwa ili kumuepusha mwanamke kuumia kila wakti kwa sabab yeye ndo yuko on the weak side..mwanaume kusepa ndoani ni rahisi lakin si mwanamke. Because mwanamke ana huruma na uchungu na watoto wake sana. Kwahiyo ili akae na amani ni heri asijue....

I think so..I dont know so!
 
Wenye akili ndogo hawataelewa hapa watakuja wamewakaa kwa fujo maana yapo kama ma agent ya uzinzi kwenye ndoa zao na ndoa za wengine kutwa kuanzisha miuzi ya uzinzi na wanaona ni kawaida

Kitu kingine unakuta mme mlevi na mke mlevi hapo unatarajia nini na walevi wanauzi wao wa kimasikhara
[emoji1][emoji1][emoji1]
Acha kuhusisha Uzi pendwa na mambo ya kijinga. We fanya Yako yanayokupasa ufànye kwenye ndoa Yako.
Ndoa za wengine hazikuhusu
 
Hivi kwa akili ya kawaida hatuwezi kujiuliza aliyesema wanandoa wasishirikishane simu alikuwa ana maanisha nini? Na baadhi wa wanandoa wanatii jambo baya kama hili ambalo lina akisi Uzinzi na Uasi ndani ya ndoa. Ndicho tulichoagizwa hadi tukaapa madhabahuni/ mbele za Mungu?. Tumepewa akili na Mungu ili tuweze kuchuja mema na mabaya, naomba Mungu atusaidie
emoji120.png
Mpwa una ugomvi na Simu? Nani kakwambia uzinzi unakaa kwenye Simu??
 
Mtaongea mengi kuhusu sijui simu sijui nini lakini bottom line ndoa nyingi zinafeli kwa sababu wanao oana hawa sifa kuu ya kuwa mke na mume nayo ni; wanapaswa kuwa hawajaonja tunda la pale kati🤣🤣🤣🤣
 
Mungu hakuwahi kuoa wala kuishi na hawa viumbe, alizalisha tu tena mchumba wa mtu na kumtelekeza akawa singo mama….. hawezi kuwa mshauri mzuri wa masuala ya ndoa.
 
Back
Top Bottom