Sina uelewa sana na mambo ya nchi ndio maana nimeuliza chanzo cha yote haya ni nini?
Binafsi naona chanzo cha kubinafsisha bandari labda ni kutaka kupata pesa kwa ajili ya kujikwamua baada ya hali kuwa ngumu. Mfano kupata pesa za kulipa mishahara, kuendeleza miradi, kulipa madeni ya nje na ndani, kuajiri, kununua madawa nk.
Suala la kuanguka kiuchumi huwa haliji ghafka, bali ni mchakato na inafikia kipindi unatafuta njia za kujikwamua.
Miaka ya 2010s bandari ya Sri Lanka ilichukuliwa na Mchina baada ya kushindwa kulipa madeni.
Je, sisi Watanzania tuna uhakika madeni yetu ni himilivu na tunaweza kuyalipa au tayari yalishatushinda ndio maana tunatafuta njia ya kujikwamua?
Je, kwa jinsi maisha yetu yalivyo Watanzania tunahisi tunaweza kuendelea au ndio tumeishayakanyaga? Hapa namaanisha, matumizi ya serikali yalibaki kuwa makubwa huku vyanzo vya mapato vikiwa vile vile na wakati mwingine vikihujumiwa na baadhi ya viongozi.
Je, siku kuna siku viongozi watasimama hadharani kusema nchi imefilisika kama ambavyo viongozi wa Sri Lanka walitamka hadharani ili wananchi wajue au ni Wananchi wenyewe kujiongeza tu?
Ila kwa Tanzania itakuwa tupo pazuri ndio maana ajira zinatolewa, mavi 8 yananunuliwa, miradi mipya ya barabara inaanzishwa!