Chanzo cha foleni Dar es salaam, serikali inahusika

Chanzo cha foleni Dar es salaam, serikali inahusika

Tangopori

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2012
Posts
1,628
Reaction score
1,290
Serikali ndo chanzo cha foleni jijini Dar es salaam kwa kufanya almost kila kitu kuwa hapa jijini!
  1. kuna sababu gani ya wizara ya maliasili na utalii kuwa Dar? Kwa nini isiwekwe maeneo yenye utalii kama Arusha na wafanyakazi wake wote wakae huko?
  2. kuna haja gani wizara ya kilimo kuwepo Dar? Kwa nini isiwekwe mbeya na wafanyakazi wake wakahamia huko?
  3. kwa nini wizara ya madini isiwekwe Mwanza au Shinyanga kwenye rasilimali nyingi za madini?
  4. Mbona bunge waliweza kulihamisha?
  5. Iweje uchumi wa nchi utegemee mji mmoja kwa almost 80%?
  6. kwa nini viwanda vya gesi visijengwe Mtwara?
  7. kwa nini serikali isifanye mchakato wa kuhamishia mashirika yake mengi kwenye mikoa mingine?
 
Mkuu Tangopori pole kwa kukerwa sana na foleni kama tunavyokerwa wakazi wengine wa Dar. Lakini ushauri unaotoa kuhusu kupunguza foleni za magari Dar naona kama una mushkeli kidogo.

Unataka wizara zitawanywe kuelekea maeneo yenye rasilimali husika, ni wazo zuri lakini unaamua vipi kwamba Arusha ndiko kwenye maliasili nyingi kuliko kwa mfano Mafinga(msitu wa Sao hill), Kilosa (Hifadhi ya Mikumi), Mara (mbuga ya serengeti),Kilombero (milima na hifadhi ya udzungwa + misitu ya tao la mashariki) n.k Ningekubaliana na wewe kama ungejenga hoja yako kwa misingi ya kuitaka serikali ihamie Dodoma kama ilivyoamriwa toka mwaka 1973. Hilo lingesaidia kuondoa foleni Dar es salaam na kuihamishia Dodoma.

Wizara zinatakiwa kuwepo kwenye makao makuu ya serikali kuzitawanya wizara hizi katika mikoa mbalimbali kulingana na upatikanaji wa rasilimali husika zinazohusu shughuli za wizara hizo kutaongeza sana gharama za uendeshaji wa serikali. Kwani itasababisha kila siku maafisa na magari ya wizara moja kuwa safarini kuelekea wizara nyingine katika kukamilisha majukumu yao mbalimbali. Wizara hizi hazifanyi kazi in isolation zinategemeana. Wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi inasimamia elimu ya juu na vyuo vya ufundi na ualimu, TAMISEMI inasimamia elimu ya sekondari hapo unaweza kuona mahusiano na mawasiliano ya karibu yanayopaswa kuwepo miongoni mwa wizara hizi mbili hivyo kuziweka mikoa tofauti ni kuongeza gharama za uendeshaji wa serikali kwa njia ya posho za maafisa na madereva, mafuta ya magari nk.

Pia wizara zote nchini zinahitaji kuwa na mawasiliano muda wote na wizara ya fedha, kwani ndiko iliko hazina ya serikali, pia wizara ya utumishi ambayo inahusika na maendeleo ya rasilimali watu katika utumishi wa umma. Hivyo wizara zinatakiwa kuwa katika mkoa mmoja ili kuepuka gharama na pia kuzuia muda kupotea kupitia safari kutoka mkoa(wizara moja) kwenda mkoa mwingine(wizara nyingine)
 
Tusizungumzie Dar tuu, hapa Arusha traffic police ndio chanzo kikuu cha foleni.
Police wameuwa wanafuatana wengi kama mchwa kusimamisha magari katikati ya barabara bila kufikiri mtu anatoka nyumbani kwake akiwa na ratiba na muda maalumu wa kufika anapo kwenda.
Hawa jamaa wamekuwa TRA hapa mjini, hivi kazi ya traffic ni kukusanya mapato ya serikali au ni kuelimisha watu matumizi mazuri ya barabara???????
 
Serikali yenu sikivu italifanyia kazi,tunawaletea mabasi yaendayo kasi ili kupunguza au kuondoa foleni,treni za jamaa hazijasaidia?
 
ni kweli kwa mfano mbezi asubuhi trafiki wanasimamisha malori yasiingie mjini ili kuepuka mafoleni lakini matokeo yake wanayasimamisha kienyeji wanachukua elfu 2 mbili za malori na magari ya maji na inakuwa usumbufu badala ya kutatua foleni wanaizidisha
 
Tatizo la akili za kushikiwa. Wameshasema capital ni Dom basi wahamishe Ilkulu na wizara zote waone kama balozi na mashirika mengine hayaendi Dom. Dar ibaki kuwa kibiashara na bandari zaidi. Ni hatari kwa uchumi wa nchi 80% kutegemea sehemu moja (mabaya zaidini potential kwa Tsunami)!! kidding. Wakipeleka capital Dom vitu vingine vitahama na kuboreshwa taratibu, Mfano mzuri Nairobi, Abuja nk. Sasa sisi tunamgando wa Dar Dar Dar ...stupid.
 
acha uongo

Tatizo la foleni Dar ni:

Meya wa Dar
Meya wa Ilala
Wizara ya sheria
Wizara ya mambo ya ndani
Jeshi la polisi
Uongozi mzima wa Dar es salaam City council

Taitizo letu ni kutokuwa na LAW & ORDER
Hivi how hard is it kurekeshisha fraffic lights zote za Dar?

Hivi kuna umuhimu gani wa traffic police kuwepo kwenye kila junction kama traffic lights zinafanya kazi?

nashauri tungeiga wakenya ambao wamekuja na sheria kali zaidi za barabarani na watu watakuwa na adabu

btw

Tanzania ndio nchi pekee duniani ambayo mkuu wa traffic hataki kuelezea sababu ya watu kukamatwa wakifanya U turn hata sehem ambayo hakuna alama inayokataza dereva asifanye U turn

naomba tuwe wakweli kwenye hili.
 
Kwa maoni yangu...kama sio serikali kuhamia Dodoma..basi Jiji la Dar linahitaji lifanyiwe utafiti wa kutosha juu ya hii kero ya msongamano (foleni).......kuwepo kwa barabara za kwenda kasi na polepole.....barabara za baiskeli na waenda kwa miguu...kujenga vivuko vya waendao kwa miguu aidha kujenga madaraja ya juu (manzese) au kuchimba mahandaki chini ya barabara(Iringa)....utii wa sheria za barabara ikiwemo uzito wa magari na kiwango cha kasi kilichowekwa....
 
Umedadavua vizuri!
Mkuu Tangopori pole kwa kukerwa sana na foleni kama tunavyokerwa wakazi wengine wa Dar. Lakini ushauri unaotoa kuhusu kupunguza foleni za magari Dar naona kama una mushkeli kidogo.

Unataka wizara zitawanywe kuelekea maeneo yenye rasilimali husika, ni wazo zuri lakini unaamua vipi kwamba Arusha ndiko kwenye maliasili nyingi kuliko kwa mfano Mafinga(msitu wa Sao hill), Kilosa (Hifadhi ya Mikumi), Mara (mbuga ya serengeti),Kilombero (milima na hifadhi ya udzungwa + misitu ya tao la mashariki) n.k Ningekubaliana na wewe kama ungejenga hoja yako kwa misingi ya kuitaka serikali ihamie Dodoma kama ilivyoamriwa toka mwaka 1973. Hilo lingesaidia kuondoa foleni Dar es salaam na kuihamishia Dodoma.

Wizara zinatakiwa kuwepo kwenye makao makuu ya serikali kuzitawanya wizara hizi katika mikoa mbalimbali kulingana na upatikanaji wa rasilimali husika zinazohusu shughuli za wizara hizo kutaongeza sana gharama za uendeshaji wa serikali. Kwani itasababisha kila siku maafisa na magari ya wizara moja kuwa safarini kuelekea wizara nyingine katika kukamilisha majukumu yao mbalimbali. Wizara hizi hazifanyi kazi in isolation zinategemeana. Wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi inasimamia elimu ya juu na vyuo vya ufundi na ualimu, TAMISEMI inasimamia elimu ya sekondari hapo unaweza kuona mahusiano na mawasiliano ya karibu yanayopaswa kuwepo miongoni mwa wizara hizi mbili hivyo kuziweka mikoa tofauti ni kuongeza gharama za uendeshaji wa serikali kwa njia ya posho za maafisa na madereva, mafuta ya magari nk.

Pia wizara zote nchini zinahitaji kuwa na mawasiliano muda wote na wizara ya fedha, kwani ndiko iliko hazina ya serikali, pia wizara ya utumishi ambayo inahusika na maendeleo ya rasilimali watu katika utumishi wa umma. Hivyo wizara zinatakiwa kuwa katika mkoa mmoja ili kuepuka gharama na pia kuzuia muda kupotea kupitia safari kutoka mkoa(wizara moja) kwenda mkoa mwingine(wizara nyingine)
 
mwenye nchi alisema hiyo ni dalili ya maendeleo ndo maana watu wana magari sana na foleni ndefu sana..kama siku ile tuliyofika tegeta saa nane usiku...hayo kwake ndo maaendeleo
 
acha uongo

Tatizo la foleni Dar ni:

Meya wa Dar
Meya wa Ilala
Wizara ya sheria
Wizara ya mambo ya ndani
Jeshi la polisi
Uongozi mzima wa Dar es salaam City council

Taitizo letu ni kutokuwa na LAW & ORDER
Hivi how hard is it kurekeshisha fraffic lights zote za Dar?

Hivi kuna umuhimu gani wa traffic police kuwepo kwenye kila junction kama traffic lights zinafanya kazi?

nashauri tungeiga wakenya ambao wamekuja na sheria kali zaidi za barabarani na watu watakuwa na adabu

btw

Tanzania ndio nchi pekee duniani ambayo mkuu wa traffic hataki kuelezea sababu ya watu kukamatwa wakifanya U turn hata sehem ambayo hakuna alama inayokataza dereva asifanye U turn

naomba tuwe wakweli kwenye hili.
Hapo kwenye nyekundu...Hadi leo hii taa zetu za kuongozea magari zinatumua muda kuongoza (time operated)..hakuna mahusiano kati ya taa na nyingine...wala hakuna detectors zinazoweza kujua urefu wa foleni moja ili taa ziweze kufanya kazi kwa uwiano kufuatana na urefu wa foleni... ndiyo maana kunakuwa hakuna budi lazima askari atumike kuongoza akiwa na kifaa cha mawasiliano ili uwiano wa mtiririko wa magari uwe sahihi......kama utaweza kukumbuka kuliwahi kutokea malalamiko kama hayo mwaka 2006 ....askari wa barabarani wakaamua kuacha taa ziongoze na ilipofika saa 2:30 asubuhi Dar ilikuwa imesimama...barabara zote zilijaa magari yaliosimama....hakuna sehemu ya kupita.......
 
acha uongo

Tatizo la foleni Dar ni:

Meya wa Dar
Meya wa Ilala
Wizara ya sheria
Wizara ya mambo ya ndani
Jeshi la polisi
Uongozi mzima wa Dar es salaam City council

Taitizo letu ni kutokuwa na LAW & ORDER
Hivi how hard is it kurekeshisha fraffic lights zote za Dar?

Hivi kuna umuhimu gani wa traffic police kuwepo kwenye kila junction kama traffic lights zinafanya kazi?

nashauri tungeiga wakenya ambao wamekuja na sheria kali zaidi za barabarani na watu watakuwa na adabu

btw

Tanzania ndio nchi pekee duniani ambayo mkuu wa traffic hataki kuelezea sababu ya watu kukamatwa wakifanya U turn hata sehem ambayo hakuna alama inayokataza dereva asifanye U turn

naomba tuwe wakweli kwenye hili.

Kaka kwa Dar Traffic Lights sio suluhisho.Angalia siku nyingine kwenye Traffic Lights kunatokea Jam,watu wanashonana mpaka aje traffic police, ndio awanasue.Tatizo la huo mji kila mtu mjuaji.Taa ya njano inawaka unakuta jamaa wanawahi kataa kekundu kasiwakute,wengine nao wanaunga mpaka mwenye haki inabidi asubiri.
 
watanzania tunapenda solution za muda mfupi...........

Dawa ni kuboresha miundo mbinu......
Ukiangalia planning ya barabara zetu ni mbovu tu, wameplani kama vile population inapungua na haiongezeki..... Na zaidi bembeni mwa barabarani hadi barabarani kumegeuka parking.........

Miundo mbinu haiendani na hali halisi, iboreshwe
 
hapo kwenye nyekundu...hadi leo hii taa zetu za kuongozea magari zinatumua muda kuongoza (time operated)..hakuna mahusiano kati ya taa na nyingine...wala hakuna detectors zinazoweza kujua urefu wa foleni moja ili taa ziweze kufanya kazi kwa uwiano kufuatana na urefu wa foleni... Ndiyo maana kunakuwa hakuna budi lazima askari atumike kuongoza akiwa na kifaa cha mawasiliano ili uwiano wa mtiririko wa magari uwe sahihi......kama utaweza kukumbuka kuliwahi kutokea malalamiko kama hayo mwaka 2006 ....askari wa barabarani wakaamua kuacha taa ziongoze na ilipofika saa 2:30 asubuhi dar ilikuwa imesimama...barabara zote zilijaa magari yaliosimama....hakuna sehemu ya kupita.......

kaka kwa dar traffic lights sio suluhisho.angalia siku nyingine kwenye traffic lights kunatokea jam,watu wanashonana mpaka aje traffic police, ndio awanasue.tatizo la huo mji kila mtu mjuaji.taa ya njano inawaka unakuta jamaa wanawahi kataa kekundu kasiwakute,wengine nao wanaunga mpaka mwenye haki inabidi asubiri.

watanzania tunapenda solution za muda mfupi...........

Dawa ni kuboresha miundo mbinu......
Ukiangalia planning ya barabara zetu ni mbovu tu, wameplani kama vile population inapungua na haiongezeki..... Na zaidi bembeni mwa barabarani hadi barabarani kumegeuka parking.........

Miundo mbinu haiendani na hali halisi, iboreshwe

dawa yake ni law & order

kila mtu akifuata sheria na akijua faini na adhabu ya kuvunja sheria itakuwa kubwa bas hakutokuwa na haja ya traffic barabarani

ukweli ndio huo
 
Serikali ndo chanzo cha foleni jijini Dar es salaam kwa kufanya almost kila kitu kuwa hapa jijini!
  1. kuna sababu gani ya wizara ya maliasili na utalii kuwa Dar? Kwa nini isiwekwe maeneo yenye utalii kama Arusha na wafanyakazi wake wote wakae huko?
  2. kuna haja gani wizara ya kilimo kuwepo Dar? Kwa nini isiwekwe mbeya na wafanyakazi wake wakahamia huko?
  3. kwa nini wizara ya madini isiwekwe Mwanza au Shinyanga kwenye rasilimali nyingi za madini?
  4. Mbona bunge waliweza kulihamisha?
  5. Iweje uchumi wa nchi utegemee mji mmoja kwa almost 80%?
  6. kwa nini viwanda vya gesi visijengwe Mtwara?
  7. kwa nini serikali isifanye mchakato wa kuhamishia mashirika yake mengi kwenye mikoa mingine?
Serikali ihamie Dodoma tuu mbona hiyo solution ilikuwepo since enzi ya mwalimu!!! Dodoma ikapimwa vizuri CDA ikaanzishwa lakini wapi viongozi wetu wanaogopa vumbi. Mbona kipindi cha Bunge wanaenda?? au posho zitapungua. Dawa yake kuweka road block barabara zote zinazoingia katikati ya jiji kisha yanunuliwe mabasi makubwa (icarus) yapite bure halafu kama unataka kutumia gari lako binafsi yasiyo ya abiria unalipa 100,000/= kuvuka kisha unalipa parking fee 100,000/= nyingine kwa siku. Kama huwezi upande basi, bodaboda au baiskeli. Na hii iwe kwa wote bila kujali huyu waziri au nani?
 
Nchi kama UK
9590192_03030dfafb.jpg

umeona hayo mabox ya yellow...maana yake juu kuna kamera na huruhisiwi kusimama hapo kwani utasababisha foleni na ukisimama unapigwa fine ya kufa mtu matokeo yake kila mmjoa amekuwa na adabu na anaogopa fine

tatizo lenu mnataka kutetea mambo ambayo hayateteeki
traffic-lights-led.jpg

mkiheshimu hizi taa na sheria hakuna haja ya kumwaga traffic luuki kwenye kila junction
 
watanzania waheshimu taa? si pikipiki wala magari.....si wendakwamiguu wala wapanda baiskeli.....utakuta mtu anakufanyia rafu anakuovateki halafu anasimama mita chache mbele...amefika alipokuwa anakimbilia...

kuna siku nilinusurika ajali mbaya sitakuja isahau....
nilikuwa nakata kulia, na indiketa nimewasha......all of the sudden jamaa wa nyuma yangu (stk) aliburuza lihardtop yake kuniovateki, ni malaika tu walikuwa wamenisimamia....

wabongo hawaheshimu/hatuheshimu sheria za barabarani

Nchi kama UK
9590192_03030dfafb.jpg

umeona hayo mabox ya yellow...maana yake juu kuna kamera na huruhisiwi kusimama hapo kwani utasababisha foleni na ukisimama unapigwa fine ya kufa mtu matokeo yake kila mmjoa amekuwa na adabu na anaogopa fine

tatizo lenu mnataka kutetea mambo ambayo hayateteeki
traffic-lights-led.jpg

mkiheshimu hizi taa na sheria hakuna haja ya kumwaga traffic luuki kwenye kila junction
 
Umesahau vyuo vikuu over 30 ndani ya Dar as if ardhi imeisha
 
Back
Top Bottom