Chanzo au asili? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chanzo au asili?

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Swahilian, May 23, 2009.

 1. Swahilian

  Swahilian JF-Expert Member

  #1
  May 23, 2009
  Joined: Apr 28, 2009
  Messages: 585
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Kwanza, salaam za dhati ni kwenu ninyi ndugu, nimetafiti kidogo juu ya neno ASILI na CHANZO lakini bado nakanganyika kimatumizi hadi inafika wakati naamua kuyatumia popote tu hali ambayo imenipa sononeko la moyo hasa ninatumia hii lugha yangu itamu ya kiswahili, nimepata kusikia mf. chanzo cha mziki huu ni... au asili ya neno hili ni.... tafadhali nipeni fasili na matumizi ya maneno hayo? tupigeni mbizi jamani bahari ya lugha ni ndefu na pana!!
   
 2. Kipala

  Kipala JF-Expert Member

  #2
  May 23, 2009
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 3,536
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 145
  Ninavyoona mara nyingi maneno yote mawili yanaweza kumaanisha jambo lilelile. "Asili" ni neno kutoka lugha ya Kiarabu (asl); "chanzo" ni neno la Kibantu kutoka kitenzi "ku-anza".

  Kama ni tofauti nahisi ni swali la mwendo. "Asili" ni kama nukta katika wakati - pale nyuma, wakati moja. "Chanzo" kina mwendo ndani yake; ni harakati ya kuanza, si "nukta katika wakati" tu bali ule mwanzo pamoja na kile kilichotoka mle.

  Kwa kutumia mifano yako: "Chanzo cha muziki" - Waarabu huimba kwa njia fulani, mtindo huu ulifika Uswahilini ukapokelewa ukawa "taarab" jinsi tunavyoijua leo. Yaani muziki si kitu imara bali staili zinakua na kubadilikabadilika. "Chanzo" kinaweza kutaja mwendo huu. Unaweza kusema pia "Asili ya muziki wa taarab" na ukisema hivyo unaangalia tu athira ya Kiarabu bila kuzingatia jinsi gani muziki huu wa Kiarabu ulibadilika kuwa uimbaji wa Kiswahili.

  "Asili ya neno hili" - asili ya "asili" ni Kiarabu "asl" jinsi inavyoonekana katika konsonanti zake. Hapo sipendi kuangalia mabadiliko mengine ya neno hili naridhika kuona kuwa neno hili la Kiswahili limetokana na lile neno la Kiarabu.

  Mfano tena: Asili ya Kiswahili iko pwani la Afrika ya Mashariki, chanzo chake ilikuwa kukutana kwa tamaduni za wafanyabiashara Waarabu na za wenyeji asilia wa pwani hili.

  Je wenzangu manonaje?
   
  Last edited: May 23, 2009
Loading...