Mkomamanga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2011
- 815
- 189
Leo baada ya taarifa ya habari ya saa moja channel 10 wameonesha kipindi maalum juu ya Press Conference ya Waziri wa Mambo ya ndani Emmanuel Nchimbi na waandishi wa habari iliyofanyika jana. Mambo kadhaa ameyataja katika hotuba yake lakini machache naona yanahitaji kufikiria kidogo.
1. Hadithi ya kumwokoa naibu waziri aliyetiwa mikononi mwa polisi kwa kuendesha kwa kasi, na pesa ikatumwa kwa M-Pesa je ndo mfumo wa siku hizi wa kukusanya mapato ya TRA?
2. Amedokeza mazungumzano ya IGP na Dr. Slaa na kuwa IGP alimsihi Dr. Slaa kama vile yeye si IGP lakini akasema avumilie kidogo mambo ya Sensa, je kule BUBUBU Zanzibar hakukuwa na sensa? Akina Kigwangala na Bashe wamefanya mikusanyiko ya wafuasi wao na kutishiana kupigana risasa sensa ilikuwa inaendelea na uchaguzi wa nazi za mikoa na wilaya kwa upande wa jumuiya za CCM pia umefanyika wakati wa Sensa wao wako juu ya amri ya serikali?
3. Amesema kipindi cha kupigania uhuru Baba wa taifa katika mikutano yake hakuna wafuasi waliowahi kuuawa! Je haoni kama anaashiria polisi wa kikoloni kuwa wastaarabu kuliko polisi wetu wa sasa nchi huru?
4. Na channel 10 kurusha taarifa yake kwa staili hii na mambo aliyoyazungumza yenye propaganda nyingi za kichama zaidi kuliko serikali hawaoni kama ni kumsaliti mwajiriwa wao marehemu Daudi Mwangosi?
Wakuu karibu jamvini tutoe mawazo yetu