#COVID19 Chanjo za COVID-19 haziathiri DNA kwa namna yoyote

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
DNA.png


Kumekuwa na mining'ono kuhusu chanjo za COVID-19 kuathiri DNA. Lakini je, hili lina ukweli wowote?

Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), hakuna chanjo ya COVID-19 inayoathiri au kuingiliana na DNA kwa namna yoyote ile

UNICEF inaeleza kuwa chanjo hufunza seli jinsi ya kutengeneza protini ambayo huchochea mwitikio wa kinga ndani ya mwili ili kuulinda dhidi ya virusi. mRNA ni tofauti na DNA na hukaa tu ndani ya seli kwa takriban saa 72 kabla ya kuharibika. Hata hivyo, haiingii kamwe kwenye kiini cha seli, ambapo DNA huhifadhiwa.

========

Can COVID-19 vaccines affect your DNA?

No, none of the COVID-19 vaccines affect or interact with your DNA in any way. Messenger RNA, or mRNA, vaccines teach the cells how to make a protein that triggers an immune response inside the body. This response produces antibodies which keep you protected against the virus. mRNA is different from DNA and only stays inside the cell for about 72 hours before degrading. However, it never enters the nucleus of the cell, where DNA is kept.

Source: UNICEF
 
Unicef ni hao hao mabeberu ex vice president wa pfZer anasema mrna vaccine hazifai huyu alikua boss wa kampuni kwa makumi ya miaka na anakiri hivyo wewe na UNICEF yako ni nan hadi mpinge?
 
Huu ugonjwa tukiacha kuuzungumzia, unapotea. Ila tukianza kuujadili tu kama hivi, ndio unarudi tena, hivi ni ugonjwa wa aina gani huu? Halafu WHO na UNICEF zina majukumu yanayofanana hadi wawe source ya taarifa za kiafya duniani?
 
Mtachonga sana ila mimi kushawishika kuchanja bado sana
Uchanje au usichanje, kikubwa wanajaribu kujustify matumizi ya mkopo wa Trillion 2 kwenda kununua chanjo ambazo hata hivyo watu hawazitumii na hawazihitaji, ni wanaleta publicity tu ili siku wakisema tumenunua chanjo za Trillion 2 pawe na somesort of justification, kila kitu ni njaa tu, hata huyu aliyepost ni njaa tu ndio inamfanya akubali fikra zake zilawitiwe na madalali wa chanjo wenye pesa
 
Back
Top Bottom