''Chanjo'' ya shambulio la mitandaoni yatengezwa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,560
9,416
_96717384_komyutavaccine.jpg

Utengezaji wa faili moja unaweza kuzuia shambulio la mashine yote.
Hatahivyo watafiti hawajafanikiwa kupata suluhu ya mara moja itakayoweza kuzuia kirusi hicho kuenea katika kompyuta nyengine ambazo hazina kinga.

Wataalam bado hawajui shambulio hilo linatoka wapi na lengo lake ni nini.
Huku ikidaiwa kwamba kikombozi inachotaka ni cha kiasi kidogo cha dola 300, wengi wanadai kwamba shambulio hilo linaweza kusababisha madhara mabaya zaidi ama hata kutoa tamko la kisiasa.

Baadhi ya waathiriwa wa shambulio hilo ni benki kuu ya Ukraine, kampuni kubwa ya mafuta kutoka Urusi Rosnet, kampuni ya matangazo ya Uingereza WPP na kampuni ya mawakili wa Marekani DLA Piper.

Pia waliopatikana katika shambulio hilo ni hospitali moja ya Marekani katika mji wa Pittsburgh.
Lakini kwa wale walio na wasiwasi kuhusu shambulio hilo,kunaonekana kuna dawa inayoweza kudhibiti athari za kiini hicho.

Kwa kutengeza faili kwa jina Perfc na kuiweka katika "C:\Windows" folder, shambulio linaweza kusitishwa mara moja. Maelezo ya kufanya hivyo yamechapishwa katika kompyuta ya usalama na kusaidiwa na wataalam wengine.

Hatahivyo huku mbinu hiyo ikiwa ina uwezo wa kudhibiti kirusi hicho, ina uwezo wa kuzilinda kompyuta za kibinafsi ambazo faili zina Perfc. Watafiti kufikia sasa wameshindwa kupata suluhu ya kudumu itakayozuia shambulio hilo kabisa.

Ijapokuwa inaweza kuifanya mashine kuwa na kinga kama alivyoelezea mwanasayansi wa kompyuta Profesa Alan Woodward, bado inaweza kusambaza kiini hicho katika kompyuta nyengine zilizounganishwa.

Kwa watumizi wengi, kuweka Windows mpya ni suluhu ya kuzuia shambulio hilo iwapo ingetaka kuathiri komyuta yako.

Kusambaa kwa kirusi hicho kipya kunaweza kuwa kwa mwendo wa pole ikilinganishwa na kile cha mwezi ulioipita cha WannaCry wataalam wametabiri huku wachangunuzi wa alama za siri wakisema kuwa kirusi hicho hakikuwa na lengo la kusambaa zaidi ya lengo lake.

Kutokana na hilo, wataalam kadhaa wanatabiri kwamba shambulio hilo halitasambaa sana kama lilivyofanya siku ya Jumanne hadi pale kiini hicho kitakapoimarishwa.



bbc swahili
 
Hawa Hackers wanahatarisha usalama wa dunia mtandaoni,serikalini, taasisi na kwenye mashurika mbalimbali kutokana na hao Virus wanaowatengeneza
 
Kirusi chaitwaje?
Hii itakuwa ni athari za snowden na usa or USA na urusi
So perfc yazuia Vipi?
 
Mkuu umesema kweli kabisa. mimi nilisha acha kutumia windows huu mwaka wa tatu sasa. Mimi natumia Ubuntu.
Kwa hiyo unasema windows haina security??
Je antvirus kama windows defender, karspesky hazifanyi kazi??
 
Mm pia ...mwaka wa 6 sasa baada ya kuuliwa pc yangu......nikaihama window kabisa


Safi sana mkuu. Windows inatesa sana mara sijui antivirus mara sijui vitu gani. Ni hovyo kweli.
 
Back
Top Bottom