Chanjo ya saratani ya shingo ya kizazi: Kikwete anaelewa anachoongea? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chanjo ya saratani ya shingo ya kizazi: Kikwete anaelewa anachoongea?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kapotolo, Sep 28, 2010.

 1. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #1
  Sep 28, 2010
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Akiwa kwenye ziara yake ya kanda ya ziwa na kwingineko, nimemsikia jk akiahidi kutoa chanjo ya saratani ya shingo ya kizazi kwa akina mama wote. Hii nayo ni kati ya zile ahadi zisizotekelezeka za mheshimiwa huyu kwa sababu:

  1) chanjo hii hutolewa kwa watu ambao hawajapata maambukizi ya virusi vya HPV ambavyo ndio husababisha saratani hii na virusi hivi huenezwa kwa njia ya zinaa, kwa hiyo hutolewa kwa wasichana/wanawake ambao hawajaanza mahusiano ya kimapenzi. Umri unaopendekezwa ni kati ya miaka 9 - 16, kwa hiyo kusema akina mama wote watapatiwa chanjo hii si sahihi. Na hawa si wapiga kura (9 - 16), so akina mama wanadanganywa. Kama umeshakuwa na mahusiano haikusaidii kwa kuwa asilimia 90% ya akina mama tayari huwa na maambukizi wanapokuwa kwenye mahusiano.

  2) chanjo hii ni gharama sana, kwa tanzania inapatikana chanjo ambayo ni 'bivalent' ambayo dose moja ni sh 45,000/- na mtu mmoja anahitaji dose tatu kila miaka mitatu, kwa matumizi haya ya serikali ya jk ya anasa kuliko maendeleo na afya hawataweza kuafford, labda waniambie kama bush or sorry obama ameahidi kutoa chanjo hii bure, vinginevyo hiki nacho ni kiini macho.

  Ningependa kumshauri mh. Jk, aahidi ku-raise awareness juu ya saratani ya shingo ya kizazi ambayo ndiyo saratani inayoongoza kwa kuua akina mama wengi tanzania kuliko saratani nyingine yoyote na kwamba akina mama wawe na tabia ya kucheck afya zao, hii inaweza kusaidia kugundulika viashiria vya saratani hii au saratani yenyewe katika hatua za awali ambazo zinaweza kutibika tena kwa gharama ndogo kuliko hiyo chanjo.

  Jk asitumie ignorance ya watanzania kuomba kura, najua hili la chanjo ya kizazi labda kashauriwa lakini kwa mara nyingine tena kaingizwa chaka.
   
 2. Mpambalyoto

  Mpambalyoto JF-Expert Member

  #2
  Sep 28, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu nadhani kama ulivyosema JK akiongea huwa haelewi vyema anachokisema. Kwa mara nyingine tena tunawalaumu washauri wake! Alichotakiwa ni kuhamasisha na kutoa fursa ya wanawake kupima hii saratani. Na labda kwa kuwa kuna ofa ya kampeni angesema wanawake watapimwa hii saratani bure kwa mwaka mara moja. Atenge fungu kwa ajili hivyo. Pili, kuhusu hiyo ya chanjo inawezekana tukiacha anasa na pale tunapoangalia kuwa taifa linaanzia hapo kwenye kizazi.
  Pamoja na mateso mengine, ni kweli kabisa hii saratani inawatesa sana wanawake wa Tanzania
   
 3. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #3
  Sep 28, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,830
  Likes Received: 10,142
  Trophy Points: 280
  Ugomvi wangu ni kwamba hivi hakuna watu ambao huwa wanamshauri kabla ya muheshimiwa huyu kuongea kuuza chai na kahawa jukwaani kwa bei ambayo hata mtu wa "Kariakoo" ataielewa.???
   
 4. PatPending

  PatPending JF-Expert Member

  #4
  Sep 28, 2010
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 490
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Shukrani kwa elimu nzuri Mkuu Kapotolo.
   
 5. M

  Msavila JF-Expert Member

  #5
  Sep 28, 2010
  Joined: Jul 25, 2007
  Messages: 404
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Kapotolo unachosema ni kweli. Chanjo, japo kuna ubishi hata nchi za nje jinsi ya kuigharimia, ni ghali. Kinachotakiwa ni kuwataka wanaume pia wapime uwepo wa vimelea vyake, kwa kuwa ngono ndio inayoambukiza ugonjwa huu!!
   
 6. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #6
  Sep 28, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Inawezekana wanamweleza vitu sahihi ila anasahau, haiwezekani kila kitu tuwasingizie wasaidizi wake.
   
 7. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #7
  Sep 28, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,592
  Likes Received: 1,676
  Trophy Points: 280
  Well said bro!
   
Loading...