Chanjo mpya ya HIV yatoa mafanikio

Chanjo mpya ya HIV yatoa mafanikio

Sexer

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2014
Posts
8,513
Reaction score
8,276
150123132413_boletin_ebola__640x360_ap_nocredit.jpg
Chanjo

Mbinu mpya ya chanjo imeonekana kuwakinga nyani dhidi ya virusi vya HIV ,ripoti ya wanasayansi wa Marekani imesema.

Chanjo kwa kawaida huifundisha kinga ya mwili wa mtu kukabiliana na maambukizi.

Lakini,watafiti katika taasisi ya Scripps mjini Carlifornia wamebadilisha DNA ya nyani hao ili kuzipa seli zao uwezo wa kukabiliana na virusi vya HIV.

Kikosi hicho cha wanasayansi kimetaja hatua hiyo kama mafanikio makubwa na sasa kinataka kuanzisha mbinu hiyo miongoni mwa binaadamu.

Majaribio yaliofanywa miongoni mwa nyani hao katika ripoti ya jarida la asili,yalionyesha kuwa nyani walikingwa kutokana aina yoyote ya virusi vya HIV kwa kipindi cha wiki 34.

Watafiti wanaamini kuwa mpango huo huenda ukawa muhimu miongoni mwa watu ambao wana virusi vya HIV.

Mtanfiti bingwa Professa Micheal Farza ameiambia BBC :'' tunakaribia kupata tiba ,lakini bado tunakabiliwa na vikwazo hususan katika salama wa kuwapa watu wengi zaidi.

''Tunaifurahia na tunadhani kwamba mi mafanikio makubwa,lakini tuna upendeleo''.

Chanjo za HIV zimeshindwa kufanikiwa kwa kuwa virusi hivyo hujibadilisha mara kwa mara kila vinapolengwa na dawa.

Lakini Chanjo hii mpya hulenga eneo ambalo vurusi hivyo hujibadilisha.

http://goo.gl/cD7GFL
 
Teh! Teh! Saizi ni kutindua tu make haya mamipira hayaleti utamu kamili
 
Ngoja tunoe madushe yetu.litabaki tatizo moja tu upungufu wa nguvu
 
Mimi bado nina imani kuwa dawa ya HIV itapatikana muda si mrefu sema urasimu na uchakachuaji ndo unaweza kukwamisha jitihada hii. Pia bei ya dawa hiyo inaweza kuwa kubwa!
 
Back
Top Bottom