#COVID19 Chanjo isiwe Siasa, Vigezo na Masharti vizingatiwe

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
28,070
36,058
Chanjo zote zikiwamo Janssen ya J & J hutolewa kwa maelekezo yaliyo wazi kutoka kwa mtengeneza chanjo husika.

Janssen kabla ya kutolewa kwa mtu haya yanahitajika kuchukuliwa:

1. Kipimo cha BP
2. Kipimo cha uzito
3. Kipimo cha maambukizi ya COVID-19
4. Kipimo cha urefu
5. Kipimo cha sukari
6. Kipimo cha joto mwilini
7. Nk

Yote kwa madhumuni maalumu. Vigezo na masharti vyote kuzingatiwa viko pamoja na chanjo.

Mtu yeyote mwenye maambukizi ya Covid-19, Joto zaidi ya 38.5°C, umri chini ya miaka 18 au wenye baadhi ya allergies kimsingi hawafuzu kupokea chanjo hii.

Who is "Janssen" not recommended for?

Individuals with a history of anaphylaxis to any component of the vaccine should not take it.

Anyone with a body temperature over 38.5ºC should postpone vaccination until they no longer have a fever.

The vaccine is not recommended for persons younger than 18 years of age pending the results of further studies in that age group.


Nimepokea (kama ilivyokuwa kwetu wote takribani 300 kwenye hafla hiyo) chanjo ya Janssen bila ya masharti yoyote kuzingatiwa.

Katika hafla hiyo iliyokuwa ya uzinduzi muda wa zaidi ya masaa 2 ukitumika kupiga siasa. Zoezi likiratibiwa vilivyo na mkuu wa wilaya na makada wa CCM kama kongamano la chama.

Katika siasa hizo tukiaminishwa kumpongeza Mtukufu Rais kwa kutujali mno sisi wananchi hata kutuletea chanjo bure. Kuwa ametulipia gharama zote za chanjo hii kutokea ilikotoka.

Vibwagizo vya CCM hoyeee!! Samia hoyeee!! Vikishika nafasi yake vilivyo.

Angalizo: Siasa ndani ya ugonjwa huu hazitatuvusha, bali mpango mkakati rasmi wenye kuzingatia utalaamu.
 
Kumbe chanjo kutoka Johnson & Johnson ni kwa hisani ya CCM?

Hiiiiii bagosha!
 
Back
Top Bottom