Chanjo inaposubiriwa huku Uhasama Ukitamalaki

Chanjo inaposubiriwa huku Uhasama Ukitamalaki

Kuna wazazi mpaka wanawafundisha watoto wao wakiona wahudumu wa Afya wamekuja wakimbie, hivi inamaana wanaamini kabisa serikali imeamua kuua watu wake tu ?
Kalagabaho!
Wengine msipotembea na ulinzi mtakamatwa mchomwe wenyewe mpaka ziishe!
 
Mabadiliko yoyote makubwa yanahitaji Sacrifice,Mwamba na Shujaa wetu Freeman Mbowe atatuvusha.
Mwamba msimamo wake ni mwiba kwa wale ndugu. Uwezo wake wa kuongea, upande wa pili hawana match. Si uliwasikia wanaodai katiba mpya Chadema 😂😂😂😂? Haieleweki wamepotelea wapi.

Wakisikia Mbowe mitano mingine roho zinataka kuwatoka.


Kuna gharama za kulipa tunapaswa kujiandaa kisaikolojia.
 
Mwamba msimamo wake ni mwiba kwa wale ndugu. Uwezo wake wa kuongea, upande wa pili hawana match. Si uliwasikia wanaodai katiba mpya Chadema 😂😂😂😂? Haieleweki wamepotelea wapi...
Umaarufu wa Freeman Mbowe utazidi kukua kadri atavyokaa Jela,na jina lake litasikika Afrika nzima tuombe uhai tu.
 
Kalagabaho!
Wengine msipotembea na ulinzi mtakamatwa mchomwe wenyewe mpaka ziishe!

😂😂😂😂😂😂. Ng'ombe asiyetaka kurejea zizini kuliko salama hatimaye bakora humhusu:

IMG_20210720_094159_438.jpg
 
Umaarufu wa Freeman Mbowe utazidi kukua kadri atavyokaa Jela,na jina lake litasikika Afrika nzima tuombe uhai tu.

Uzuri ni kuwa:

1. Hawana magereza za kutuweka ndani hata 10% yetu.
2. Hawana uhalali wa kuchagua vipaumbele vyao dhidi ya vipaumbele vyetu sisi wananchi.
3. Hawana kauli ya mwisho kwenye lolote bali sisi wananchi.

Wenye nchi yetu ni sisi tukikomaa vipaumbele vyetu ndiyo vinasimama.
 
Naamini bwana Melo analishughulikia ombi letu. "Mamburula kama hilo wala hatupendi hata kujua kama kuna pua lilijaribu ku-poke 😂😂😂!"

Ukweli mchungu makamanda wako resigned. Hawana nia ya kumwunga Mama mkono tena...
Mkuu wangu kwani CHANJO ya Corona na umuhimu wake inahusiana vipi na kukamatwa kwa mh.Mbowe?

#TujitayarisheniNaChanjo
#JMTMilele
 
Mkuu wangu kwani CHANJO ya Corona na umuhimu wake inahusiana vipi na kukamatwa kwa mh.Mbowe?

#TujitayarisheniNaChanjo
#JMTMilele

Mbona nimeeleza kinagaubaga mjomba?
Iko hivi:

------
Kuna mambo yanakera sana. Kwa hali ilivyo SSH atajikuta amekwama matopeni:

1. CCM chawa wa mwendazake hawataki kusikia Corona, chanjo, tahadhari au yatokanayo. Pia hawataki katiba mpya.
2. CCM chawa wa SSH hawataki katiba mpya ila wanamwunga mkono, kwenye msimamo wa Corona na yote yatokanayo.
3. Chadema waliokereka na mwelekeo wa SSH baada ya msimamo wake kuhusiana na katiba mpya kukolezwa vilivyo na sakata la Mwanza na yatokanayo yake yote, hawana mpango naye tena.
4. Wengine waliobakia wakiwamo CUF, ACT, na wasio na vyama na ma liberali wasioeleweka wanataka nini.

#1 ni wengi kuliko #2
#3 ni wengi kuliko #4
#3 wanaweza kuwa sawa na #1 kiidadi.

Kwamba Chadema ni wanyonge? Labda kama mleta mada ana maana kuwa SSH amewavunja moyo na hawana sababu tena ya kumwunga mkono kwa lolote.

Huwafanyii watu ukiukwaji mkubwa wa haki zao, ukatumia polisi kuwakamata, ukawabambikizia kesi nk kisha ukategemea wakuunge mkono.

Katikati ya kuelekea chanjo ya Corona kutoka kwa beberu waliyeaminishwa wapumbavu kuwa ni mchawi wetu mwenye kutupiganisha vita vya kiuchumi, chanjo kwetu ni muhimu zaidi kwa sasa kuliko mengine yote:


Ifahamike kuwa jukumu la kwanza la serikali yoyote ni kuwaunganisha watu wake na kupata uhalali tokea katika walio wengi.

Serikali inayoshindwa kuwaunganisha watu wake na ikashindwa kupata uungwaji mkono wa wengi hupoteza uhalali wa kuwapo kwake.

Kumwacha SSH akale alikopeleka mboga hakuwezi kuitwa unyonge:


Kwetu chanjo inaendelea kuwa ni muhimu na umuhimu wake kwa sasa unaishia kwetu sisi wenyewe. SSH na washirika wake wakale waliko peleka mboga.
-----------

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Back
Top Bottom