Sidhani kwa sababu sentensi ya kwanza "umesema nini?"
'nini' inawakilisha kitu/jambo alilolisema mtu X lkn mtu Y hakusikia/ haamini kama alichokisikia ndicho.
. Kuna mambo mawili hapo
1. Mtu X angemuuliza mtu Y "Umesemaje?" sentensi ya 2 ndo mahala pake kwa sababu mbele ya kitenzi sema inaweza kuwekwa N, kishazi au sentensi (na kufanya kazi kama yambwa) au kitenzi, mfano
"nimesema cheza"
"nimesema bibi anaumwa"
nimesema "tusi"
2. "Umesema nini?" ni sentensi yenye kitenzi kinachohitaji 'yambwa'
Kiwakilishi hakiwezi kuwakilisha kitenzi. Mtu Y akijibu "nimesema cheza" inaleta ukakasi. Linakuwa jibu la "umesema nifanyeje?
Ktk sentensi ya 2, mtu X anamwamuru mtu Y
Nimejaribu tu lkn. Naomba ujuzi zaidi mkuu.