Changamoto za wakulima | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Changamoto za wakulima

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by kilaza Sammy, Jun 7, 2011.

 1. k

  kilaza Sammy Member

  #1
  Jun 7, 2011
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Katika harakati za kujijengea uwezo wa baadae(near future) niliamua kutumia pesa zangu kidogo za bodi ya mkopo (mimi ni mwanafunzi mwaka wa tatu) kufanya kilimo. Nilianza na project tatu tofauti kwanza fish farming -mkenge mkuranga(Upo hatua za awali) pili kilimo cha passion,mahindi,karanga,mung'unya(butternut squash) -bupu mkuranga,na mradi wa tatu ni majaribio kilimo cha mahindi kwa kutumia mbegu hybrid-mwanzomgumu kisarawe.

  Mafanikio; mradi wa bupu umeenda vizuri sana na nategemea good yields soon

  Changamoto; mradi wa mwanzomgumu- mwaka huu kimetokea kitu cha ajabu sana mashamba mengi mahindi ama yamekufa au kudhoofu. Wakulima wanatoa hypothesis kuwa ni athali za mabomu ya Mbagala! Je wataalam wa kilimo mnasemaje?
   
 2. L

  LAT JF-Expert Member

  #2
  Jun 7, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  mkuu ... hebu nijuze zaidi kuhusu mung'unya(butternut squash) -bupu

  nashukuru
   
 3. k

  kilaza Sammy Member

  #3
  Jun 8, 2011
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu ahsante, Mung'unya linaloitwa butternut squash ni aina ya boga zenye umbo dogo na rangi kama ya machungwa. Yapo familia moja inaitwa "cucurbits" pamoja na matango,tikiti,maboga ya kawaida,n.k. faida zake ni kwamba huzaa sana kuliko boga za kawaida na sehemu inayoliwa ni kubwa (minofu).

  Bupu ni kijiji wilayani mkuranga,nice time.
   
 4. Sabayi

  Sabayi JF-Expert Member

  #4
  Jun 8, 2011
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 2,321
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  @Kilaza
  Hivi market ya hiyo Mung'unya? kwa hekari moja unaweza kuzalisha kiasi gani? Bupu ni mbali kiasi gani toka Mkurunga mjini? Vp upatikanaji wa ardhi huko?
   
 5. k

  kilaza Sammy Member

  #5
  Jun 8, 2011
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  market nategemea kuuza kisutu market na kuhuisha potential customers nipo kwenye mchakato wa kuanza mazungumzo na shoprite chains.

  mwendo wastani dk 30 or so barabara sio tarmac so it varies ni njiapanda ya Kipalang'anda unaingia ndani.
   
 6. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #6
  Jun 8, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 740
  Trophy Points: 280
  Hongera kilaza kwa kuanza mambo ya ujasiriamali katika kiwango hicho ukiwa bado chuo,ni changamoto kwa kizazi cha sasa.Keep it up....
   
 7. L

  LAT JF-Expert Member

  #7
  Jun 8, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  mkuu ....nashukuru kwa kunifahamisha .......nimeshayafahamu sasa .... umbo lake lipo kama kibuyu...! isn't it...?

  i like your marketing strategies ....kuna big supermarket chain kutoka kenya Nakumat Supermarket wanaingia rasmi tanzania na wanafungua rasmi the first branch in moshi ... nadhani hii pia ni potential target market ..... i am sure uki capitalize kwenye kupata local market at the end unaweza kupata export market .... ninashauri sana kwamba lengo kuu liwe ni export au unasemaje...?

  naomba unijulishe pia je kilimo cha zao hili la mung'unya (butternut) kinahitaji irrigation au ni mvua za misimu ... ninashamba hekari 18 lenye tittle lipo moshi three kilometers from dar main road ... the level of water table is good..... unaweza kunishauri nifanye nini... kilimo au mifugo ...currently ninalima mahindi ... je zao hili linaweza kufaa

  i wish you all the best
   
 8. k

  kilaza Sammy Member

  #8
  Jun 8, 2011
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ahsante, ila changamoto katika nchi zetu kilimo kinachanganywa na siasa, na viongozi wetu hawako serious na kilimo.

  mfano bei na upatikanaji wa mbegu bora ni ishu.
  tafiti haziwi communicated kwa wakulima
  miundombinu ya kibiashara mibovu
  maeneo makubwa ya ardhi yamehodhiwa na vigogo pasi kuyafanyia uzalishaji.

  pembejeo duni,zilizo bora bei juu (zingine zinapigwa kutu pale mwenge)
  mabadiliko ya tabia nchi n.k lakini katikati ya hayo yote TUPAMBANE VIJANA KWA UKOMBOZI WA UCHUMI!!!!
   
 9. k

  kilaza Sammy Member

  #9
  Jun 8, 2011
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yaah, ndio hayo! uko mwepesi sana ndugu. Yes exportation ndio hasa lengo langu,nashukuru mungu shule ipo ukingoni kwani nayo ilikuwa some kind ya mzigo, sasa ninaweza kuwa na muda wa kutosha kufanya shughuli zangu. Oppurtunities za market kwa kilimo ni kubwa na zitazidi kuja lakini je tumejiandaa?

  Zao hilo linaweza kustawi vizuri kwa neema za Mungu,ila kama ujuavyo irrigation is the only way to opt ili kupunguza risks.

  Yamkini, eneo hilo linaweza kufaa kwa zao hili kwani linapenda maeneo ya ki- tropics .
   
 10. Z

  Zahor Salim Member

  #10
  Jun 8, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 30
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  huko bupu ekari moja inauzwaje? ina vary kuanzia kiasi gani
   
 11. k

  kilaza Sammy Member

  #11
  Jun 8, 2011
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  Bei za huku zinaathiriwa sana na manunuzi yaliyofanyika karibuni(market trends). Kwa mfano bei ilikuwa chini ya 300 000 lkn wakaja jamaa fulani wenye pesa wakanunua eka kibao kwa 350 000, balaa na wanakijiji wengine wakatamani range hiyo.

  wanaoharibu bei ni vigogo!
   
 12. Hoppity Cywale

  Hoppity Cywale Senior Member

  #12
  Aug 28, 2014
  Joined: Aug 20, 2013
  Messages: 126
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Kuna umeme huko bupu?
  Na kwa sasa nimeambiwa hekari moja ni laki nane, ni kweli imefikia huko?
   
Loading...