Yaani hakunaga usawa, familia nyingi zenye nimeona za ndugu, babu zetu, majirani hakunaga amani kwa wake wenza adi watoto na wengi sana uahirikina unahusika kwa kina bi mdogo ni kweli usemavyo wengi wanaocoment kupingana mama/ bibi zao wanaowasema ni kina bi mdogohahah..uncomplying comments nyingi humu ni za watoto wake za pili, tatu, michepuko etc or watu walio mke zaid ya mmoja.., ok sijaja kuponda familia zenu za uke wenza ila mtambue na naamini asilimia kubwa ya familia za uke wenza zina migogoro mikubwa sana.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna babu wa kiarabu nilimzoea aliniambia ana wake watatu nikamwambia hongera uko na raha alinijibu tu katika kitu ambacho alikosea maishani mwake ni kuoa wake wengi na ktk kitu ambacho kawausia vijana wake ni wasijaribu kuoa mitala nikamshangaa sana nikamwamuuliza dini si inakuruhusu akaniambia acha tu hakuna kitu kibaya kama kuwa mtumwa wa mwili wako. Yaani wewe maisha yako unazunguka tu kutoa mapenzi kwa hao wanawake halafu wanawake wenyewe hawajatahiriwa kwa hiyo wako na ashki sana matokeo yake unachoka mwili na akili ukifika kwa huyu ukimwambia nimechoka anakujibu unampenda zaidi fulani na kumbuka wanashindana kutoa penzi matokeo yake wewe unachoka na bado watoto wanazaa wengi na wewe ndio uhudumie, usipohudumia unaonekana unapendeleaw fulani aliniambia sina hamu tena ila according tu yeye mwenyewe watoto wake wa mke mkubwa ndio waliobarikiwa kwenye maisha.na ndoa pia.
Yaani hakunaga usawa, familia nyingi zenye nimeona za ndugu, babu zetu, majirani hakunaga amani kwa wake wenza adi watoto na wengi sana uahirikina unahusika kwa kina bi mdogo ni kweli usemavyo wengi wanaocoment kupingana mama/ bibi zao wanaowasema ni kina bi mdogo
98% ya familia za mitala hazinaga amani wala maelewano kubali kataa lakini ndo ivo, ata wawe wanaishi mikoa tofauti hao wake wenza yaani hakunaga.....na wengi walio oa mara nyingi ukiongea nao lazima akwambie anajutia kuoa mke zaidi ya mmoja ni kwanini???Ooh. Sorry kwa kudhania wa kike. Though mama zetu akishamchukia mke mwenzake utaambiwa kila baya kuhusu babako achikia mbali mamako mdogo.
It is very wrong kulaani uke wenza kwa kisa kimoja tu cha nyumbani kwenu.
Ndoa za wake wenza ngumu sana ingawa sja experience iyo ktk familia yangu nimesimliwa na baba na mama wote wametoka ktk familia za wake wenza, ya mama nimeiona, ni tabu tubu babu alishafariki lakini watoto adi sasa hakunaga maelewano, baba anasema babu naye alijichanganya akachukua bi mdogo akamkamata na matunguli akafukuzia mbali, na apo mzee ni wa miaka 50 uko so msitudanganye wenye kumpinga mtoa mada izo mambo zipo toka zamani mnoooo uke wenza sio mzuri
Uke wenza wa kuishi nyumba moja sio kabisa.
Mke mkubwa aheshimiwe
Tatizo sio mke wa pili,ila baba yako hana hela na anataka kuoa wake wawili.wenzake wanajenga sehem tofauti.
Unawapa mitaji kisha unawaacha wapambane na hali zao,panapofel unarekebisha,familia zinabaki fresh tu.
Ila kama hawana kitu wote,nawe unga unga mwana,ah watakuroga mpaka ujute na ugomvi wa hapa na pale kama mashariki ya kati
Sent using Jamii Forums mobile app
Wanaume,Hamida ameshatupa somo,ukitaka kugeuka Kama kambale oa mke mmoja
hahah..uncomplying comments nyingi humu ni za watoto wake za pili, tatu, michepuko etc or watu walio mke zaid ya mmoja.., ok sijaja kuponda familia zenu za uke wenza ila mtambue na naamini asilimia kubwa ya familia za uke wenza zina migogoro mikubwa sana.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna sababu ya kuoa mke wa pili lakin sababu za kuchepuka zipo??Ilikuwa ni siku ya krismasi, Baba anamleta mwanamke nyumbani na kumtambulisha kwa lazima na madaha kwetu. Akimwambia mama "Huyo ndio mke mwenzako muheshimu".
Kabla ya hapo huyu mwanamke alikuwa mchepuko wa mzee, akazaa nae, na baadae akawa akawa ni mchepuko wa mzee, nahisi mzee alinogewa na shepu la yule mama, angali hata alikuwa ana mtoto (aliezaa na mwanaume mwingine) ila mdingi alimfanya official.
Mzee wangu alimnyanyasa sana mama yangu hata mbele yetu. Kusahau juhudi ya mama ndio ilikuwa sababu ya mzee kufika alipo (na hata pesa ya kuwa na jeuri ya kuoa mke mwingine). Alijitamba sana kuwa huyo mwanamke ndio aina ya mwanamke aliekuwa ana hitaji na kwa mama yangu alikosea step. Huyu mwanamke (mke wa pili) ili alinde nafasi yake alijitahidi zaidi katika ushirikina na vioja vingi vya kumharibia mama yangu.
Ilifika wakati mama aliondoka nyumbani. Maisha ya kuona mama ananyanyasika na baade ile hali ya kumkosa mama ilituathiri sana watoto kisaikolijia hadi katika elimu. Hatimaye biashara za mzee zilianza kufeli na mambo yake yakaanza kwenda vibaya, na ilionekana wazi kuwa baraka za huyu mzee ni kutokana na uwepo wa mama.
Wadogo zangu walikuwa wadogo sana, na malezi ya huyu mama hayakuwa original kwa wadogo zangu. So mama aliamua kusacrifice furaha yake na kuja kurudi ili akae atuleee ili hali alijua bado atakutana na kero.
Lakini yule mwanamke hakuwa kama vile mzee alivyotegemea, kama ni tabia mbaya aliionesha hata mara tano zaidi ya mama yangu. DAYS ARE NUMBERED! Yani huyu mwanamke ambae alikuwa anaonekana kama sweetheart wa mzee, Mzee alimfumania meseji za mapenzi kutoka kwa mmoja wa wateja wake na inasemakana kipindi huyu mzee alipokuwa hayupo huyu mwanamke alikuwa anaenda kujivinjali usiku na awala yake. hahah ...Mdingi alipiga akataka kuua na ilimuuma sio kawaida hadi akaita ndugu zake.
■WANAWAKE
JIULIZE, KWANINI MWANAMKE AKUBALI KUOLEWA KAMA MKE WA PILI KAMA SIO AMEKOSA UTU AU KUTAKA MTELEMKO WA MAISHA KWA KUWA WANAUME WALIOKWISHA KUOA UNAKUTA WAMESHATOKA KIMAISHA. MARA NYINGI MNAKUJA KUHARIBU MAISHA YA FAMILIA YA MKE YULE NA WENGI WENU MNAHAKIKISHA NAFASI MAALUM MNAISHIKA NYIE, SO MNAHANGAIKA KWA WAGANGA.
■MWANAUME
HAKUNA SABABU YOTOTE YA KUWA MKE ZAIDI YA MMOJA, HAWA WANAWAKE NI WALE WALE NA HATA HUYO WA PILI ATAKUWA NA MAPUNGUFU PIA. NA KWA SISI WAKRISTO TUNAAMINI KUWA MUNGU ANAFANYA AGANO NA NDOA YA MKE WA KWANZA NA UZAO WA KWANZA.
Sent using Jamii Forums mobile app
nishaoa, nafurahia na hata kama akiniudhi sioi wa pili. ukomavu wa kili sio kuoa. kuoa ni step ya maisha ..kuna watu wa umri wako hawajoa ila wana akili zaid yako.
Sent using Jamii Forums mobile app